HATIMAYE waliokuwa Maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao wanakabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasala ya Sh Bilioni 104.1, wamepangiwa masharti ya dhamana.
Masharti hayo ya dahamana, yamepangwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kupitia Jaji wa mahakama hiyo Jaji Emily Mushi. Kesi hiyo inawakabili Bosco Kimela ambaye alikuwa Kaimu mwanasheria wa benki hiyo, ambaye pia anakabiliwa na kesi nyingine ya Wizi wa fedha za benki hiyo, kupitia Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Wengine ni pamoja na waliokuwa maofisa wengine wa BoT, ambao ni Simon Jengo, Kisima Mkango na Ally Bakari. Katika sharti la kwanza, Jaji Mushi alimtaka kila mshitakiwa kujidhamini kwa kutoa fedha taslimu au hati ya mali hisiyohamishika, yenye thamani ya Sh Bilioni 13.
Aidha katika sharti la pili, Jaji Mushi aliwataka washitakiwa hao, kila mmoja kujidhamini kwa kusaini hati ya dhamana yenye thamani yaSh Biliono 13, ikiwa ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili kwa kila mshitakiwa, ambao nao watasahini hati ta dhamana yenye thamanai ya fedha hizo.
Pia washitakiwa hao, wametakiwa kusalimisha hati zao za kusafiria katika mahakama hiyo, ikiwa ni pamoja na kuripoti kila Jumatatu kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya wanazotoka, pamoja na kutotoka nje ya Mkoa wa Dar es salaam bila kibali cha Mahakama Kuu.
Masharti hayo ya dhamana ambayo yalipangwa, kwa mujibu wa kifungu namba 36, cha sheria ya kuhujumu uchumi, yatatakiwa kutimizwa mbele ya msajili wa mahakama hiyo. Awali upande wa utetezi katika kesi hiyo, uliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kupangiwa masharti ya dhamana ka washitakiwa hao.
Hatua ilifikiwa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala, ambayo ndiyo inayosikiliza kesi ya msingi dhidi ya washitakiwa hao, kushindwa kufanya kupanga masharti hayo, kutokana na sheria kutoruhusu hilo.
Katika kesi hiyo ya msingi, washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matatu, yakiwamo ya kuhujumu uchumi, kwa kuzidisha kiwango kilichowekwa na Serikali, kwaajili ya mradi wa uchapishaji noti, jambo lilopelekea Serikali kupata hasala ya Sh Bilioni 104.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. PETER NALITOLELAOctober 09, 2009

    KAKA MISUZI MIMI NAONA HAWA MABWANA WAMEONEWA TU SIZANI KAMA HIZO HELA ZA EPA WAMEZIIBA INAWEZEKANA ZIMEPOTEA KWA NDUMBA NIMEAMBIWA KUNA LIGANGA LA KIENYEJI MWANZA LIKIWEKA FEZA ZAKE ZOTE ZINAPOEAGA HUU NI UONGO HIZO FEZA HAZIJAIBIWA

    ReplyDelete
  2. Dhamana = Billion 13 in cash OR hati ya mali isiyohamishika.

    Then aidha anajidhamini au anadhaminiwa na someone else ambaye naye ni muajiriwa.

    Atakuwa katoa wapi hiyo mali??? Si inabidi na yeye mdhamini akamatwe aeleze ni wapi alipotoa hiyo mali!

    It's crazy!

    ReplyDelete
  3. MzeeKifimboChezaOctober 09, 2009

    Na we Muhidini Mkongwe mzima unakuwa kama DOGO kule JIACHIE?

    Sio hasaLa bwana. Ni HasaRa

    ReplyDelete
  4. TUNACHOJUA HAKUNA ATAKAE FUNGWA,KWANINI TUPOTEZEANE MUDA? MICHUZI WEKA STORY NYINGINE KAMA IZO ZINATURUSHIA TUU.

    ReplyDelete
  5. kama kawa, mazingaombwe yatafanyika mahakamani na kila mtu ataachiwa huru.

    JK OYEEEEEE, umekubalika mtakatifu rahisi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...