Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera akiweka shada la maua katika jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu masanja mara baada ya kutoa heshima za kwenye uwanja wa uhuru, Dar leo. Marehemu Masanja, aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake anategemewa kisafirishwa kuelekea kwao Urambo, Tabora, ambako imepangwa mazishi kufanyika siku ya Ijumaa.
Waombolezaji wakiwa wameibeba mwili wa aliyekuwa meneja wa uwanja wa Uhuru, Celestine Charles Masanja wakati wa kutoa heshima za mwisho zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru, jijini Dar mchana wa leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. huyu michuzi anapaswa ahojiwe uraia wake aisee kwa mtindo huu wa uandikaji "waombolezaji wakiwa wameibeba mwili wa....

    ReplyDelete
  2. bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake libalikiwe.
    Huu msiba umenifunza sana kuanzia leo naapa nitaacha tabia ya kumfungia mume wangu geti na kumpokonya mlinzi funguo....huwa akirudi anapaki gari nje thn anapanda juu ya gari anaruka ukuta kuingia ndani sasa nimeona ninachokitafuta ni kama hiki kilichotokea au kumvunja miguu baba wa watu na ni mnene kweli.

    ReplyDelete
  3. RIP bro Massanja

    mdau.

    ReplyDelete
  4. Pamoja na kwamba kila mtu ana siku yake na style yake ya kufa,hii kwangu imenigusa na kunifanya kuwashutumu wanawake wote ambao wanawafungia waume zao milango na kulazimika kuruka mageti wakati wapo bwiii,huyo kafa wapo wanaoteguka viuno na miguu na hata kupata majeraha!!Acheni wanawake,sipati picha huyu mke wa marehemu anavyojisikia baada ya tukio hili.

    ReplyDelete
  5. wanandoa tujirekebishe, hamna haja ya kutaka kuonyesha mke wa masanja ana makosa, sawa nenda kwenye pombe zako ila kurudi kwako usiharibu starehe ya wengine, na kwa nini aruke ukuta, kwani si kuna funguo watu uchonga mbilimbili...... jumatatu unarudi nyumbani mida hiyo na hakuna sababu maalum ya kukweka nje nikimaanisha kazi...... tubadilike wanandoa, inaumma sana pale unapoona watoto wadogo walioashwa, ila ndio mungu naye anafundisho kwetu sote

    ReplyDelete
  6. wanawake wengine mnajifanya mabaunsa hapo sasa tabia hiyo ni mbaya sana sijui mnafanyaga kitchen party cha nini kule mnafundwa jinsi ya kuishi na husbando yoo ho yani muwatunze waume zenu tena muwapende na kuwabembeleza manake wanaume ni kama nyau jifuzeni sana manake ujane si mchezo hasa kwa wale magolikipa ni ngumu sana

    ReplyDelete
  7. Nadhani msisahau tu kuwa tumezaliwa na kufa ni lazima, asingeanguka ukutani lingempata lingine tu na akafa maadam tarehe na saa yake ilifika. tuwe na imani kufa ni lazima na wote ndio njia yetu ila kifo lazima kiwe na sababu ukisema hata usitoke ndani siku hiyo ukilala tu israeli huyu hapa anachukua chake mchezo umekwisha cha muhimu tusafishe njia zetu maana hatujui siku wala saa. tuombeane na tujiombee wenyewe pia. kaka masanja Mungu akuweke mahali pema wewe umeshamaliza yako kazi kwetu tuliobakia na style yetu ya kuondokea itakuwaje siri ya Mungu. Pumzika kwa amani ndugu yetu.

    ReplyDelete
  8. ManufacturerOctober 21, 2009

    Hi dhana ya kuzalau wanawake mama wa nyumbani (na kuwaita magolikipa) mimi binafsi inaniuma sana. Nimekuwa katika familia ambayo baba amefanya kazi ya kuajiliwa miaka yake yote na mama kazi yake ilikuwa ni kutulea sisi mpaka tumekuwa. Ninahisi watu wengi (ingawa si wote) tuliozaliwa miaka ya 1970's na kurudi nyuma wamekuwa katika mazingira ya aina hii. Nikiangalia nyuma, sioni kitu chochote ninachotaka kubadilisha, na kama ningeambiwa nichague kwamba mama naye angekuwa mfanyakazi wa kuajiliwa au awe anatulea sisi nyumbani, ningechagua awe anakaa nyumbani kutulea sisi. Ingawa kwa kusema hivyo simaanishi kwamba ni makosa kwa wanawake kufanya kazi, isipokuwa nataka kuelezea pia si makosa kwa wanawake kuwa mama wa nyumbani. Kulelewa na mama ni tofauti sana na kulelewa na yaya.
    Baadhi ya nchi zilizoendelea zimeanza kuitambua kazi ya wanawake wanaokaa nyumbani kama kazi ya kawaida (Full-time employment).

    Kina dada, kama wewe unafanya kazi ni vizuri kwako lakini hiyo isikufanye ukajiona eti wewe ni bora kuliko mwanamke asiyefanya kazi (mama wa nyumbani). Binadamu tupo tofauti na kila mmoja ana mapendekezo yake.

    Na wewe uliyesema kuwa tumezaliwa ili tufe, na hiyo dhana yako ya kufa kazi ya mungu usituletee hapa. Hii dhana ya kufa kibwegebwege na kumsingizia mungu ndiyo inayotufanya waafrika tuwe tunakuwa ovyo wakati wazungu hawafi ovyo ovyo kama tunavyokufa sisi. Sasa kama ni kazi ya mungu, mbona huyo Mungu anatupangia sisi tuu vifo vya kibwege bwege?

    Kwahiyo watu wenye kufanya ngono nzembe wakapata ukimwi na kufa kama kumbikumbi nao unataka kusema Mungu ndo kawapangia siku yao ifike wafe kiivyo?

    Vifo vya kizembezembe vinaepukika

    Tujifunze kuchukua majukuma ya matendo yetu na siyo kila kitu kumsingizia mungu.

    ReplyDelete
  9. Kilimbey Ole MbayaniOctober 21, 2009

    Mamufacturer I agree with you. There are 4 reasons to cause death:-
    1) Old age:
    (This cause multiple organ failure and hence death.)

    2) Untimely accident:
    (Getting killed like in a car crash, getting shot, work related accident, etc etc.)

    3) Severe/chronic desease: (Diabetes, Cancer, etc.)

    4)Reckless behaviour and self abusing life style:
    (Excessive drinking, bad diet, promiscuosity, drug abuse, etc etc)

    Haya mambo ya kulewa kisha kupepesuka barabarani ukagongwa na kufa, hiyo siyo kazi ya mungu.

    Kuwa na wanawake/wanaume wa nje kupata ngoma na kufa, hiyo siyo kazi ya mungu.
    Kujidunga mpaka kufa hiyo mungu hajakupangia. n.k

    pyuuuuumbaffffff

    ReplyDelete
  10. mungu aiweke roho ya marehmu masanja mahali pema.Nakumbuka kipindi kile anarudi kutoka Cuba timu ya kwanza kuwa kocha ilkuwa timu yetu ya Akiba kwa kweli alikuwa kocha mzuri sana.Nilistuka sana kusikia habari za msiba wake.Rip

    ReplyDelete
  11. Pole sana Devota na watoto! Castro, selestine, moreen na bernadetha Mungu akupe nguvu na mungu akutangulie katika kipindi hiki kigumu ulichonacho, mwenyezi mungu akupe uvumilivu mkubwa sana, yatasemwa mengi Mwenyezi Mungu ndo mwamuzi wa yote yenye ukweli na ya uongo. RIP

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...