Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) inakukaribisha katika Disco la kuwachangia Bw Abuu na Bi Tatu ambao walipatwa na janga la nyumba yao kuungua moto wiki chache zilizopita.
Disco hili takayofanyika katika ukumbi wa Tropican Pub (zamani Taitec-Area51, simu: 0476-78-0560) ulio karibu na kituo cha train cha Sagamino (Sotetsu line) siku ya Jumapili ya tarehe 11 mwezi wa 10, 2009.
Mheshimiwa Kaimu Balozi atakuwa mgeni rasmi siku hiyo.
Katika shughuli hiyo Dj mzoefu Pembe aka Dj Zee atawapatia Watanzania na wahudhuriaji wengine muziki safi wa aina mbali mbali. Kingilio: 1500Yen.
Tafadhali ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio. Kwa maelezo zaidi kuhusu shughuli hii tafadhali wasiliana nasi simu zifuatazoo:
080-3097-5744,
080-3458-8786
Ahsanteni na karibuni sana
Uongozi wa Jumuiya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. what happened on this one? feedback please

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...