Marlow akiwatumbuiza wakazi wa jiji la A-Taun wakati wa tamasha la fiesta 2009 na wimbo wake wa Pipii katika viwanja vya Equator hotel usiku wa kuamkia leo
Mkurugenzi wa Clouds Fm/Prime Time Promotions Joseph kusaga akizungumza na wasanii kutoka nchini Uganda, mara baada ya kufanya vyema katika tamasha la fiesta usiku wa kuamkia leo
Alikiba akiimba jukwaani kwenye tamasha la fiesta one love 2009 lililofanyika usiku kuamkia leo katika uwanja wa hotel ya equitor,mjini Arusha.Baada ya kufanyika mjnii Arusha tamasha la fiesta linaelekea jijini Mwanza ambapo litafanyika jumamosi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. - mmnh, anko nanihii, pole mwakwetu..naona wamekupa 'cha lukaya' hapo darajani..ndo ukubwa huo, kaka!..Hivi hebu nambie, yule Vermaelen amenunuliwa kuziba pengo la Toure ama la Adebayor, me nachanganyikiwa, sasa!..

    ReplyDelete
  2. Ali kiba nakukubali katika kuimba kwako lakini kutepesha trauza mpaka chupi au bukta ya ndani ionekane sikuungi mkono kabisa ni ushamba wa kuiga yasiyopendeza wala yasiyo na maendeleo.

    Ali,Michu na waTz wenzangu samahani kwa kutumia hii lugha kali.

    ReplyDelete
  3. KULIPOKUWA NA MITINDO KAMA ULE WA KUCHANA AFRO AMBAO SASA UMERUDI, SISI WATU WAZIMA TULIKUWA TUKIELEWA ULIKUSUDIA KUMTANGAZA MWAFRIKA NA NYWELE ZAKE.
    SASA HUU MTINDO WA KUPOROMOSHA SURUALI UNATUSHINDA KUUPA TAFSIRI.
    JAMANI WADAU WENZANGU NISAIDIENI, MAANA KWA MKAO HUU HUYU ALI KIBA NAONA KAMA ANATANGAZA U KAKA POA?
    HATAMANISHI KWELI HUYU?
    ASHAKUM SI MATUSI
    MDAU LEICESTER

    ReplyDelete
  4. Ali nenda ukanye kwanza halafu urudi kuimba !! Hii aibu sana kuigiza mambo ya wamerikani wapumbavu weusi, hii tabia inapigwa vita marikani, mpaka walitka watu wapewe faini wakionakena wanatembea barabarani na kuonyesha chupi. Tuigize mazuri na ya maana - hii ni aibu na wala haleti mavutio, suruali za kuteremla hizo wasili yake ni utumwa na waliofungwa jela, watumwa walinyimwa mikanda ili washindwe kutoroka kwa kukimbia wakati suruali inaporomoka, na wafungwa walinyimwa mikanda huko marikani ili wasiitumie kujinyonga au kunyonga wenzao. what next? same sex marriage in Tanzania?

    ReplyDelete
  5. annon hapo juu (Sun Oct 04, 10:04:00 PM) na kuunga mkono. Du huu mtindo wa kuonyesha bukta/chupi unatia aibu. sijui tunaelekea wapi?

    ReplyDelete
  6. Anon wa 5;22Pm mbona muongo. Watu kama hamjui vitu bora muache kutungatunga uongo ili mradi mmeongea.Yeah,napinga huu uvaaji lakini tukumbuke kila kitu kina wakati wake na sehemu yake,kama Ali Kiba anavaa hivi hata uraiani ni vibaya sana,lakini kama anafanya hivi jukwaani haina neno.Hivi ukivaa Suti na tai inaashiria maendeleo?
    Kuna mwaka watu walikuwa wanampiga madongo Rais Mkapa kwa kuvaa mkufu wa dhahabu,wabongo bwana.Tusubiri tuone Rais Jk atakapovaa ROLEX wabongo watakavyo mnyonga kwa maneno.

    ReplyDelete
  7. Mbigiri hapo juu angalia hii,

    http://answers.yahoo.com/question/index?qid=20070502084928AAan3tx

    ReplyDelete
  8. Mbigiri, unajua nini "Role Model?"
    Akiba ni fahari yetu ya TZ na wapo watoto wengi wanataka siku moja wafike alipo na hivyo wako tayari kumuigiza tabia na mavazi. Mfano wako wa kuvaa suti na Rolex haina maana yo yote kwenye mjadala huu.
    Jaribu wewe uwende kuomba kazi wakati suruali yako ipo chini ya matako !!! wanawake huwa wanoanyesha maziwa kuwavutia wananaume, sasa kuna maana gani mwanamume aonyesha matako yake? ndio itamvutia mwanamke hiyo? basi wacha suruali nyumbani watembee na chupi tu !!!
    haitoshi wanaume wanvaa viherini na mikufu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...