Hivi wadau kwa nini kila siku tunaona wa nigeria, south africa na mwaka huu ndugu zetu wa kenya wanachukua hizi tuzo za muziki ( MTV, Channel O) zaidi. Yaani kila mwaka wanawekwa wao tu, angalia nominees wa mwaka huu wamejazana kibao ktk vipengele vyote.
Au ndo hawa MTV na Channel O wanajikosha kwa vile hizo nchi zina pesa (naamini sasa msemo wa Profesa Jay fedha inaongea).

Ni kama vile hakuna wasanii wakubwa nchi nyingine na wanaotesa vizuri tu ndani ya bara la Afrika, wengine wanasema sababu ni lugha ya kiingereza, hao wasanii wanaoshinda tuzo hizo kila mwaka wanatwanga lugha ya kiingereza, yaani badala kutoa tuzo kwa wasanii wanaotema lugha zao an wenye vipaji zaidi ya hao ili kuwapa moyo, wanaendelea kukandamiza vipaji vyao.
Mimi nilidhani hizi tuzo zitabadilika baada ya mwaka wa kwanza lakini ninachoona sasa ni tofauti, mimi nafikiri hizi tuzo zisiitwe "Africa Music Awards" bali "Nigeria & SA Awards".

Yaani hata sijui kama hawa watu wa mtv na channel o wanajali nchi nyingine zaidi ya Nigeria na SA. Nakwambia Afrika kuna wanamuziki wakali sana lakini hizi tuzo kubwa wamelalia sana fedha zaidi ya kipaji.

Ushauri wangu watoe tuzo ili kukuza vipaji vya wasanii wa nchi tofauti na sio kwa baadhi ya nchi tu.

Msibane Habari Hii!
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. mdau uko sahihi kabisa kwa kuangalia mambo kimantiki. lakini kumbuka katika dunia ya leo inayotawaliwa na 'cowboy capitalism' ambayo Bw Michael Moore anaiita "capitalism is evil" na Hayati Baba wa Taifa JKN aliita "ubepari ni unyama" kinachpewa uzito ni faida nono hata kama hiyo faida itakuja kwa gharama ya kuacha umebamiza vipaji vingine. SA, Nigeria, na Kenya ni viwakala vya 'cowboy capitalism' vinavuyoongoza barani africa. Kwa hiyo haishangazi kuona mambo yako kama unavyoyaona!!!!

    ReplyDelete
  2. Mataifa hayo yameanza kujipromoti muda mrefu kwa hiyo wanapeana ushindi kwa mazoea. Siri ni wasanii wetu kuendelea kuchegama na kutumbuiza kimataifa. Wakizoeleka basi nao wataanza kukomba tuzo hizo. If you can't beat them, join them. Ushikwapo shika mana.

    ReplyDelete
  3. ili ushinde ni lazima upige kura. Je uliwapigia kura washiriki unaotaka washinde au unasubiri something to happened from nothing? acheni ujinga, they win because their support have the gut to pick up the phone and call! simple

    ReplyDelete
  4. Tusivunjike moyo tuchapekazi sikuzote wenyeji wana haki...

    ReplyDelete
  5. INATEGEMA NA MAJAJI PIA, HEBU WEWE FIKIRIA MAJAJI HAWAELEWI KIBANTU HICHO UNACHOIMBA HUKU WENGINE WANAIMBA LUGHA YA KIINGEREZA NA MAJAJI WENYEWE WANAJUA LUGHA HIYO SASA NANI ATAKUWA NA CHANCE KUBWA YA KUSHINDA? JIBU UNALO.

    ReplyDelete
  6. Lengo la tuzo ni kushindanisha wasanii. Aliyeshinda ndiyo anaonyesha kuwa ni bora kuliko wengine. Sasa nyie mnataka ashinde, Juma Nature? Kwani hizo nyimbo zilizoshinda hazina ubora? Washindi hupigiwa kura, sasa kwa nini mnawalaumu waandaaji badala ya wapiga kura?
    Watanzania kwa kutafuta visingizio!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. anonymous wa kwanza na wa pili mnaweza kututajia wanamuziki wakali wa kibongo wanaoweza kushindana na hao wa Nigeria na SA?? tuelezeni kimuziki siyo wanaopiga kuiga kuiga tu midundo ile ile ya akina T-pain. maana track kama No one like you ya P-Squire ni muundo mpya kabisa wa R&B. tunataka vipaji hivyo siyo yale yale mamidundo ya kila siku.

    ReplyDelete
  8. Watanzania tuna tabia ya kulalamika na kutaka mambo ya ushindi na tuzo yaende KWA ZAMU! ni utamaduni wa kivivu. Kabla ya kulalamikakwamba Nigeria au Sauzi wanapendelewa kwenye tuzo jaribu hii: Chukua wasanii 10 kutoka bongo, 10 kutoka Nigeria na 10 kutoka Sauzi. Wapandishe Stejini mmoja mmoja. halafu nipe matokeo yake. I'm VERY SURE wabongo watachukua nafasi kuanzia 18 kwenda mbele. Tatizo la watu wetu ni UVIVU na kutokuona mbali, na kulewa tujisifa kutoka kwa mashabiki wasojua muziki. Tuna Safari ndefu. na hii utainona katika kila kitu. Tuamke. Mungu Ibariki Bongo ...NA WABONGO WENYEWE. (Nadhani wimbo wa Taifa ulikosewa) . Louis, DSM

    ReplyDelete
  9. Ukweli sio sababu wanaimba kiengereza ila sisi Tanzania hatupigagi kura kwa Ma-star wetu iwe kwenye Mitindo au Muziki, Hapa wala tusitafute kisingizio. Tunaweza kutuma msg na Ku-beep lakini kupiga kura hatuwezi, Tunachoweza ni lawama na kukosoa watu. Tunahitaji kusifia wasanii wetu kwanza kabla ya Kuwaponda.

    ReplyDelete
  10. Insider: Hapo mdau haongelei bongo tu na hao waandaji hawaangalii kura, yaani hizo kura ni biashara tu (wanapata hela kupitia txt message), hizo decision za winners wanakuwa nazo tokea siku walipotoa nominee list.

    Lugha za kibantu zisiwe tatizo kabisa kwa sababu mmeshaita hii Africa Music Awards. angalia wenzetu wa asia, south america wanajali sana lugha zao.

    ReplyDelete
  11. Na kitu kingine kinachoudhi, utamweka vipi msanii wa afrika apambane na msanii wa marekani halafu unaita hii mtv africa awards. Muweke kwa mfano "best out of africa act" kwa ajili ya hawa wasanii wa nje ya afrika

    Kwa sababu kuna wasanii wengine wengi wa AFRIKA inabidi wapewe nafasi pia kuwa nominated.

    Mimi kila siku I am amazed by these so-called awards that brag about being african awards.

    ReplyDelete
  12. mkiambiwa kiingereza kina umuhimu mkubwa mnabisha. Kanumba amekwenda sauzi akakanumba ya kufa mtu aibu tupu mkamtetea! haya sasa mnaona!! hamuwezi kubisha kuwa guyz if at ll we wanna go international, if at all we are gonna conquer the international market if at all we want to flourish then it's obvious that we can't afford to do without it really!!i mean english
    wewe huyo AY english baba mkwe tumemmuona anahojiwa na yule dada sporah aibu tupu english hamna kitu nyimbo zoote kibongobongo watu hawamuelewi anaimba nini!! mbaya zaidi basi ni bora nyimbo zake zingekuwa danceable, nyimbo za huyo bwana hazichezeki so watoto wa kibongo wanapenda sababu anakamua kwa kiswazi wanachokielewa lakini when it comes to dancing them they ain't danceable. sasa hebu fikiria majaji hawajui kiswahili lugha iliyotumika kwenye nyimbo hawaijui muziki wenyewe hauna mvuto wala hauchezeki and all sasa watampaje ushindi wakati kuna mashine kama Koko master D'banj(fall in love) dude kwanza liko kwa kiingereza ambacho wengi wanakisikia halafu linachezeka kinoma sasa hiyo miwaya AY ataikanyaga ataianzia wapi?? tuache tu kulalamika bila kufikiri. halafu hao wanaigeria ukiangalia miziki yao jamaa wako creative to the maximum, wanapiga kwa radha mpya ya ubunifu hawaigi mapigo ya marekani, sasa sisi sikuhizi wanabongo flavor wanaiga midundo ya kina Jigga, Akon, Brown and all yani kila kitu hawana jipya.
    wanastahili sana kushindwa warudi nyumbani wafikirie upya lakini kwa nionavyo mimi AY anaimba LAKINI si kwa kiwango cha kushinda MTV award na kuwabwaga jamaa wa Nigeria naija boys au wasouth.
    Macmuga.

    ReplyDelete
  13. Anony wa 2.55 oct 12: na wengine wote ambao mnaona kiingereza ndo kila kitu kwa nini hamuwi proud na lugha yenu???sijakataa kuna ile basic english ambayo mtu inmpasa ajue kwa ajili ya mawasiliano na watu wa diaspora wengine LAKINI isiwe ndo kisingizio cha kukosa award. huyo debanj wa nigeria aliyescoop artist of the year na nyimbo zake sijui sugar banana sweet potato hata haileti maana. quality of the songs matters the beats vocals videos pia zinamata sana. wasanii wengi wa bongo wanaproduce vitu not for the outside market mostly ni for the tz market kwa kweli.kwa hiyo hata kushinda inakuwa ngumu.
    besides mtu apate ilibidi kura nyingi zitoke kwenu na sio kulalamika tuu. wenzetu wakenya wana solidarity ya kufa mtu wanapigiana kura mno tz mnakaa tu mnategemea mtu ashinde kwa njia ya osmosis.hata kwenye tusker project fame waliokuwa wanafuatilia tumewalostisha wale wadada esp iluminata tungepiga kura kwa wingi angebaki bado mnalalamika eti kuna upendeleo
    pamoja na hayo, PEOPLE YOU SHOULD BE PROUD KWAMBA ANGALAU WAMEKUWA NOMINATED ITAWAPA MOTISHA YA KUFANYA KAZI ZAIDI.

    ReplyDelete
  14. KAZI YETU NI KULALAMA TUU,MBONA HATA CHEMSHA BONGO YA ZAI VYUO VIKUU TUNASHINDWAGA (NISEMEGE KWA KINYAMWEZI) WANYUMA NI WANYUMA TU, TUJITAHIDI BADALA YA KULALAMIKA KWANI HAKUTUSAIDII KITU.KAMA UMESOMA HABARI YA MWANZO INAYOHUSU KENYA, UGANDA NA TANZANIA BASI NINAAMINI UMEELEWA NAFASI YETU ILIPO AU NA HIYO HABARI UTAILALAMIKIA?

    ReplyDelete
  15. hili suala la kiingereza wala haliingia kwenye akili za watu makini.wasanii na nyimbo zao wakishakuwa nominated maana yake wana nafasi sawa ya kushinda bila kujali wanaimba lugha gani.sivyo wasiwe nominated at first place kama kiingereza ni moja ya vigezo.tuunge mkono wasanii wetu zaidi ndio suala la msingi hapa

    ReplyDelete
  16. Nadhani ukweli kuhusu mziki wa Tanzania utaanza kujilikana kidogo kidogo. Naweza kusema mziki uliopo kwa sasa siyo real, umebambikizwa kwa watanzania na wanaomiliki shughuli ya mziki Tanzania. bahati mbaya sana kutokana na mlolongo wa vi FM radios vyetu navyo vinaingia katika mtego huo huo. Mimi najua zipo studio ambazo ziko mbali na Dar Es Salaam zimekuwa zikitengeneza miziki kutoka kwa wasanii wasiojulikana, miziki ambayo ni mizuri lakini kwa kuwa hujawafurahisha wenye biashara yao hauwezi hata kupigwa au kusikika mahala. Inabaki kina Ali Kiba, Ali Kiba. Hakuna muziki hapo. Kwa sababu usanii hamna, vionjo hakuna, uimbaji hakuna, mdundo hauchezeki. Mziki wote Tanzania ni wa kusikiliza na kutikisa kichwa ambao umejazwa ladha ya zouk. Nani anataka zouk. Nimewahi kukaa Africa Magharibi, miziki yao inachezeka. huwezi kuamini mpaka leo kuna nyimbo za Mr. Nice au Kanichambua kama Karanga ya Saida Karoli zinapigwa mpaka leo. Ukiwaambia wasanii wetu, maproducer wetu hawakuelewi, kwa sababu wenye biashara yao wanataka hali hiyo iendelee. Akina AY, yes wao ni hiphop hakuna mziki hapo, unachezwa kwa kurusha mikono na ujumbe mkali (hapo haja ya kutumia lugha inayoeleweka inakuwa muhimu) lakini kama ni dance hall, ni mdundo ili wacheze, ujumbe siyo muhimu. Safari bado ni ndefu inabidi TBC iache kutaka kushindana na kina Clouds or Channel 5, waelekeze nguvu kwa wasanii wa kweli wanaopatikana na mchakato wa kweli, Tanzania nzima. Kisha wa produce kazi zao kwa quality nzuri na gharama nafuu. Mtaona mabadiliko na ukweli utajilikana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...