Na Sunday Shomari wa VOA
Rodgers Mtagwa aliingia Madison Garden akipeperusha bendera ya Tanzania usiku wa Jumamosi na huku mpinzani wake Juan Lopez akiingia na reggae tong kwa mpambamo wao Rodgers ambaye aliingia akipewa nafasi finyu ya kufanya chochote ameacha gumzo kubwa miongoni mwa washabiki wa ndondi hapa Marekani.
Huku mashabiki wakizomea na wengine kushangilia Rodgers Mtagwa aliuthibitishia Ulimwengu wa Ndondi kwamba yeye si mbabaishaji na hakupewa jina la "Tiger" bure kwani Juan Manuel Lopez alikuwa hajawahi kupigana zaidi ya raundi 10 katika mapambano yake yote yaliyopita isipokuwa hili.
Juan Manuel Lopez aliibuka mshindi katika pambano hilo na kutetea taji lake la WBO kwa pointi 116-111,115-111,114-113 Katika ukumbi wa Wamu Theatre uliojaza watu takriban 3152. Ama kwa hakika Juan Lopez alianza kwa spidi kama kawaida yake na kutoa mashambulizi ambayo kila konde alilorusha alipata majibu yake, na kumwangusha Rodgers Mtagwa katika raundi ya pili lakini ambapo Mtagwa aliamka haraka na kuendelea na pambano kitu ambacho yeye Rodgers anasema kuwa haikuwa chochote kwani Lopez alimpiga kwa kumsukuma kwa nyuma ya kichwa na refa pia hakuhesabu huko ni kuangushwa.
Pambano hilo liliisha kwa majaji wote watatu kumpa ushindi Manuel Lopez wakidai alipigana vizuri katika raundi za mwanzo hasa ya kwanza hadi ya sita. Lakini jinsi mpambano huo ulivyoendelea ndivyo bingwa huyo alivyozidi kuchoka na Mtagwa kuzidi kuongeza kasi ya mashambulizi hasa konde lake la kulia ambalo lilitia dosari kubwa kwenye uso wa Lopez.
Katika raundi ya saba Mtagwa alionyesha cheche kwa kuingiza makonde ya kushoto na kulia( Left and right hook) ambayo yaliingia vizuri usoni kwa mpinzani wake na kwa mujibu wa hesabu za computer Compu Box aliongoza raundi hiyo mpaka 8 kwani alikuwa nyuma kwa pointi.
Juan Manue Lopez ilibidi abadilishe staili na kumkalia mbali Mtagwa ambapo alikuwa akiingiza ngumi chache halafu anakaa mbali maana aligundua akikaa karibu anapata matatizo. Rodgers naye alionywa na kona yake asiruhusu mpinzani wake kukaa mbali bali aendelee kuingia ndani na atumie nafasi ya kujibishana makonde (pound for pound) ambayo ilikuwa ni ngumu kwa mpinzani huyo kufanikisha.
Baadhi ya watu waliokuwa wakimshangilia Lopez tangu mwanzo wa pambano walielekea kubadilisha kibao na kuanza kumshangilia Rodgers kwani katika raundi ya 11 ambapo Lopez alikuwa hoi kabisa akimshika Rodgers ambaye alikuwa akirusha makonde mengi ambayo yaliingia kwenye uso wa mpinzani wake na kumpasua juu ya jicho la kushoto na ilikuwa ni kengele iliyomuokoa Lopez katika raundi ya 11.
Katika raundi ya 12 Mtagwa aliendelea kuwasha moto na huku mpinzani wake Lopez akiendelea kupigana kwa kujihami alimanusura aanguke ila alitumia mbinu na ujanja wa kila aina kumshika Mtagwa na kumkumbatia,kumsukuma na kurusha makonde machache mpaka raundi hiyo ilipokwisha. Watangazaji waliita staili ya Mtagwa ni "Dirty Fight" wakisema bondia huyu wa Tanzania anapigana staili ya Philadelphia ambako ndiko makazi yake.
Baada ya mpambano huo haikuwa wazi nani mshindi lakini baada ya majaji kutangaza baadhi ya watu walizomea kwa kuona Rodgers kaonewa hata yeye mwenyewe alipohojiwa alisema haelewi kwa nini kashindwa pambano hilo .
Naye Lopez kwa upande wake alimsifu Rodgers kuwa ni bondia hatari na lilikuwa ni pambano gumu si kama alivyofikiria na kudai kuwa alichoka kidogo mwishoni mwa pambano hilo.
Watangazaji wa PPV walimsifia Rodgers kwamba ni bondia ambaye ameweza kuonyesha moyo mkuu na hivi sasa watu wengi zaidi watamfahamu na pia anastahili kupewa nafasi nyingine kwani ameonyesha kuwa na uwezo mkubwa hivyo wanafikiria atapata nafasi ya kuwania taji lingine la dunia au pambano kubwa.
Promota wa Lopez Bob Arum alipoulizwa kama atampa nafasi ya marudiano Rodgers alikataa na kudai bondia wake amepata ushindi wa wazi na hahitaji marudiano na Rodgers Mtagwa.
Katika pambano jingine la utangulizi la Ubingwa wa WBA (Feather) Yuriokos Gamboa wa Cuba alitetea taji lake kwa TKO katika raundi ya nne dhidi ya Whyber Garcia wa Puerto Rico. Hivi sasa wanaaangalia uwezekano wa kumkutanisha mcuba huyu na Juan Lopez.
Huku Gamboa akidai Lopez hana kitu, Lopez amemwambia akajaribishe moto wa Mtagwa aone kazi yake.
that was the fight of the year indeed.
ReplyDeletekazi nzuri Mtagwa.
we are going to hear a lot about you from now.
Cheers
Kujikwaa si kuanguka bali ni kwenda mbele. Shida ya mchezo wa ndondi ni kuwa pointi zinatolewa kwa kuangalia mshindi wa raundi. Kwa hiyo kama pambano ni la raundi kumi, ukishinda sita unabakiwa na kazi ya kuhakikisha haulambi zulia wala kunyang'anywa pointi ili uibuke kidedea.
ReplyDeleteBig up Mtagwa, endelea kuwakilisha.
Judges wamem'beba Lopez, baada ya kipigo cha round ya 11, 12 haiwezekani ameshinda.
ReplyDeleteUkumbi mzima ulishikwa na duwaa na kipigo.
Wabongo tulikuwa wachache sana, lakini tumepeperusha bendera vilivyo.
Go Rogers!!!
Mdau NY.
Tz tunaelekea kuzuri,kwanza haheem sasa mtagwa
ReplyDeleteMaelezo toka ESPN
ReplyDeleteBut that almost all came apart because Mtagwa (26-13-2, 18 KOs), whose record does not show how tough he is, was undeterred. He displayed the best attributes of toughness and relentlessness of the fighters from the places he calls home: the African nation of Tanzania and Philadelphia, where he has lived since 2000.
Mtagwa made it a street fight, constantly stalking forward while Lopez tried to keep him off.
Eventually, Lopez -- who scored a flash knockdown in the fifth round and appeared to score two others in the first round that referee Eddie Cotton ruled slips -- couldn't anymore.
Mtagwa hurt Lopez with a series of shots late in the 10th round and never stopped swinging.
He sent Lopez staggering into the ropes at the end of the 11th round. Lopez only avoided a knockdown because he grabbed the ropes to keep himself upright and Cotton didn't see it as the bell rang.
Then the real drama started when the bell rang to start the 12th round.
Lopez came out of his corner on unsteady legs and you just knew it would be a race against the clock.
Could Lopez last three minutes?
He did, but just barely.
Mtagwa was all over him. Lopez was desperate to survive. He had no defense and could barely hold on and throw the occasional punch to stay in the fight as the crowd was standing and going wild.
It was like boxing's version of legendary basketball coach Dean Smith's four corners. Lopez was desperate to reach the finish line.
Mtagwa was pounding him, outlanding Lopez 36-9 in the final round, but he just wouldn't go down as the countdown was on for the final bell.
"The last round I was very tired, really tired," Mtagwa offered as a reason he could not finish Lopez off. "He's not a strong puncher but he's a good fighter. In the 12th round I see in his eyes that he is finished."
Once Lopez (27-0, 24 KOs) made it to the end of the fight, there was little question he had won because of the large early lead he had built.
Sure enough, the official scorecards had him ahead 116-111, 115-111 and 114-113. ESPN.com scored it 115-111 for Lopez as well.
"He's a very strong guy," said Lopez, who suffered a cut over his left eye in the third round from an accidental head butt, one of many Mtagwa hit him with, with just one warning from Cotton. "Sometimes it's very difficult to fight guys like this because they have nothing to lose and I have a lot to lose."
Mtagwa made his case for a rematch.
"It was a very close fight, a good fight. Why not a rematch? I don't believe he won the fight," he said.
Don't count on it, though.
Arum intends to go through with the Jan. 23 card with Lopez facing either fellow junior featherweight titlist Celestino Caballero or featherweight titleholders Steven Luevano or Elio Rojas.
"Caballero's people are being very difficult with the amount of money they want for the fight," Arum said. "We've offered him 150,000 and if he doesn't want it, that's fine."
Arum still has designs on Lopez facing Gamboa.
"I thought Lopez fought a stupid fight," Arum said. "He can't fight a stupid fight against Gamboa. I give this [Mtagwa] kid credit, though. He stayed in there and didn't get discouraged and at the end had 'Juanma' reeling, so you have to give him props. 'Juanma' didn't have to make it that difficult."
Gamboa (16-0, 14 KOs), who knocked out Whyber Garcia in the fourth round on the undercard, said he looks forward to facing Lopez.
"I don't think Juan Manuel Lopez is better than me," Gamboa said. "He's not a challenge for me. If we fight, I will show that. [On Jan. 23], I think I should be the one carrying the card with Lopez because I am a better fighter than him. He's not better than me. Look at our records. Look at our amateur records. I was better than him in the amateurs and I am better than him as a professional."
Lopez dismissed Gamboa's words.
"Let's see him knock out Mtagwa," Lopez said. "I'll knock Garcia out like he did. Let's see what he can do with Mtagwa."
Dan Rafael is the boxing writer for ESPN.com.
Hi Mtagwa and Michuzi,
ReplyDeleteAISEE MTAGWA WEWE UNATISHA, UNAJUA TOKEA NIKUONE KTK BLOGS ZA KIBONGO NIMEKUWA NIKIJARIBU KUFUATILIA KTK YUOTUBE ILI NIONE THE WAY YOU DO.YAANI HUYU JAMAA NI BALAA, UNAJUA JAMAA NI SUGU MBAYA, ANAWEZA PIGANA KWA MUDA MREFU SANA BILA KUCHOKA, KUNAKIPINDI ALIPIGANA NA VILLA, KWAKWELI SIKUAMINI KABISA MACHO YANGU, KWANI MTAGWA ALIANGUSHWA MALA KAMA MBILI AU TATU LKN HAUWEZI AMINI VILLA ALINYOOSHA MIKONO KUASHIRIA KUWA ANAOMBA PAMBANO LIISHE, YAANI ROGERS NI SUGU MBAYA, HATA HUYU DOGO LOPEZ ANAWEZAKUWA KAPENDELEWA, WE SI UNAWAJUA WAZUNGU TENA NA ROGERS ANAONEKANA NI MBONGO, TENA MBONGO LIVE HATA RANGI YA KISHKAJI HANA.
ROGERS HEE MI NAKWAMBIA UTAFIKA MBALI, HIVI SASA NAFUATILIA NILIONE PAMBANO LAKO NA LOPEZ JAPO KWENYE YUOTUBE, JAMANI KAMA KUNAMDAU ANAJUA NIFANYAJE NAOMBA ANIJULISHE KWENYE muddynice20@gmail.com
BIG UP ROGERS NA WABONGO TUWAUNGE MKONO HAWA JAMAA ZETU KAMA KINA HASHEEM NA WENGINEYO, NA KWENYE MASHINDANO KAMA HAYA WATANZANIA MAARUFU KAMA KINA HASHEEM THABIT WAWE WANAKWENDA ILI KUONYESHA UMOJA WA WATANZANIA MUISHIO NJE.
Regards,
Muddy Nice
Muddy umetoa point muhimu, Lopez amebebwa. Bahati mbaya Rogers hakuweza kumtoa kwa TKO, kwa sababu hiyo ingemaliza ubishi, mtu mweusi, dark skin, marekani hapa bado ngumu sana kukubalika, hata within black community. Jamaa hawataki kumpa hata chance ya rematch kwa sababu wanajua kuna uwezekano mkubwa wa kumpiga mpuero rico.
ReplyDeleteMtwagwa kama utapata message hii nakupa pongezi, nafasi nyingine ya kuchukua mkanda itakuja tu, na mimi nakukahikishia nitafanya juhudi kukusanya watanzania at least 25 wa new york, hata ikibidi ticket ninunue niwauzie kwa discount tuje kukushangilia, hiyo ni ahadi. Ulituweka kifua mbele watanzania, nililishuhudia pambano ndani ya MSG.
Mtagwa nilivyomuona mimi ni kama wamemtumia sana kuchuma pesa. inaelekea amepiganishwa mapambano mengi sana bila kupewa muda wa mwili kurecover.
ReplyDeleteniliona pambano moja ambapo ni kama alikuwa anajaribu kusurvive tu. mpinzani wake alifanya kosa moja raundi ya mwisho na Mtagwa akammalizia mbali kwa knockout. hilo ni pambano la ajabu kabisa ambalo nimewahi kuangalia maishani mwangu.
pia nasikitika kusema haya, lakini nadhani career yake ndiyo inafikia ukingoni wakati jamaa wamemtumia tu.
nadhani hii ni achievement kubwa sana kwa jamaa kupewa nafasi ktk PAY PER VIEW fights.