Section of liner stolen last night -
Eneo liliobwa usiku wa tarehe 4 oktoba
Repaired section of liner stolen on 3/10/09 -
Eneo lililokarabatiwa baada ya wizi wa tarehe 3 oktoba

Mgodi wa North Mara unasikitishwa kuwataarifu kuhusu wizi wa tandio la plastiki la kuzuia maji machafu kwenye mabwawa ya maji.

Majira ya jumamosi asubuhi tarehe 3 Oktoba ilibainika kuwa mita za mraba zaidi 90 ya plastiki lilikuwa limeibiwa kama inayonekana kwenye picha DSCN1258, yenye thamani ya USD $ 1800. Mgodi ulifanya jitihada za haraka kurudishia plastiki hilo na kukamilisha kazi hiyo jumapili jioni.

Hata hivyo jana usiku wahalifu waliingia mgodini tena na kuiba mita za mraba 110 za plastiki hizo, yenye thamani ya USD $ 3300, kama inyvoonekana kwenye picha DSCN1262. Mabwawa hayo yamekuwa chini ya ulinzi wa kikosi cha polisi cha FFU tangu matukio ya wizi kusababisha uvujaji wa maji machafu mwezi wa tano mwaka huu.
-----------------------------------------------------------------

The North Mara Gold Mine reported theft of pond liners on October 3rd and 4th 2006. On Saturday morning the mine's security team established that 90 square meters of pond liners were stolen from leechate ponds.

Efforts to replace of the stolen liners was undertaken immediately after the theft on Saturday and completed by Sunday. However another theft occurred again last night on October 4th, when 110 square meters of the liners were stolen.

The ponds have been under 24hour surveillance of the FFU since vandilism incidents cause seepage in May this year. The FFU's whose hideout can be viewed from the stolen section of the liners.

The total value of liners stolen is estimated at USD $ 5100.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wahujumu sio wezi wa Tandio bali na hao wanaiba dhahabu ya nchi pamoja na viongozi wa kitanzania walioshirikana nao.

    wahujuma ni hao wanachafua mazingira kwa kisingizio cha kuweka tandio la karatasi kuzuia uchafuzi wao, tena karatasi la plastic ambalo haliozeki, Hao ndio wahujumu.

    Wahujumu wanatuathiri na makemikali ya zahabu zao vizazi na vizazi vijavvyo vya watz wanaishi maeneo ya North Mara na hata tz kwa ujumula wake

    ReplyDelete
  2. Hawa jamaa wa mgodi wa mara hapo ndipo wanapokosea. Kuweka price tag ya TANDIO, si hata ambaye aliyekuwa hajui kuwa lina thamani atataka kuja kuiba.

    Wajiandae kwa mawili, kuuwa watu wataokuja kuiba kwa risasi au waweke mlinzi aje auwawe na wezi huku tandio likiendelea kutanduliwa kwa uzembe wao.

    Huwezi weka Price tag inayoonesha kitu kinalipa na kipokipo tu halafu wananchi wakusalimishe.

    ReplyDelete
  3. Kama mnaona mmeibiwa msituambie sisi, wafikishieni taarifa hizo Polisi.
    Yaani kakipande kadogo hivyo kanatosha kununua mkweche. Mnapata wapi hela za kununulia maplastiki ya bei mbaya hivyo???? Au ndio wajinga ndio waliwao?

    ReplyDelete
  4. marketing strategy.

    ReplyDelete
  5. Naona tangazo sasa limekuja bila jina la mtoa taarifa wao (Kipaaza Sauti aka PRO). Kama lengo la kuweka bei ni kutaka public sympathy hapa imegoma. Kama lengo ni kuonesha wananchi ndio wanahusika na umwagikaji wa sumu kwenye maji, pia tangazo haijaleta mvuso. Kaka Trio na anony 09:35 thumbs up!
    A million $ question: Kama hao jamaa wa North Mara wanapata hasara, si waondoke huko mgodini, kwa nini bado wanaendelea kuchimba basi?

    ReplyDelete
  6. Wadau mi naona hawa jamaa wa mgodi huu wanatuchezea akili.. tena bila aibu wanasema kuwa Tandio limeibiwa wakati likilindwa na FFU na walinzi wa mgodi... sasa hapa wasije kuwasingizia wananchi.. maana mtu huwezi kuiba askari wakiwepo.. kaka michuzi hebu hawa jamaa watupe ukweli.. nadhani ni strategy yao kuonesha kuwa wananchi ni wabaya.. au pengine FFU ni wachovu.. hata sielewi nia yao..

    ReplyDelete
  7. Mdau wa Tue Oct 06, 01:13:00 AM

    Nakubaliana na wewe 100%, Hawa jamaa wanataka kuweka publicity kuwa wanatumia pesa nyingi sana katika kulinda mazingira, yaani wanazuia harmful chimicals kuingia ardhini ili siku wakiondoka na kutuachia mashimo halafu wananchi wakianza kuugua magonjwa ya ajabu tusiwashitaki kwani wao walichukua pre-cautions zote kulinda mazingira kwa gharama kubwa.

    Huu nao ni uongo wenye asili ya kifisadi kabisa, watatuambia Tandio linatoka Paris.

    ReplyDelete
  8. Wao wanaiba dhahabu ya million of US$, halafu wanazungumzia kuibiwa kwa makaratasi ya nailoni.

    Hawa jamaa wanachafua sana mazingira.

    Tatizo ndiyo hivyo wanakula na wenye nchi

    ReplyDelete
  9. Sasa hivi biashara ya dhahabu 'hasara' kweli. Cheki mwenyewe hapa: http://finance.yahoo.com/news/Sector-Snap-Gold-miners-soar-apf-668988377.html?x=0

    ReplyDelete
  10. ehe wafanye ulinzi tu tena hao ffu walipwe kwa hela za mwekezaji,mbona dhahabu haibiwi kirahisi walipaswa wafanye uchunguzi kabla ya kuja kuwekeza waache excuses ambazo hazina maana na viongozi wetu wakuwa ...... sana inatia aibu kubwa kwa nchi

    ReplyDelete
  11. these people a fat liars, they are trying to hide something, they are pretending they bought that liner to cover up something, hope government will catch them if people from that area drink the water theres a risk of getting cancer.

    ReplyDelete
  12. its all politics and corruption there, they took that liner themselfs to pretend was stolen,

    ReplyDelete
  13. Nyie North Mara acheni usanii wenu! Lazima mwa wajua hao wevi au ni nyie wenyeweee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...