JK akisalimianan na baadhi ya Maaskofu wa kanisa la African Inland Church Tanzania(AICT) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Kirumba, jijini Mwanza leo, ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini Tanzania.
akihutubia wanachi walishiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) katika uwanja wa michezo wa Kirumba jijini Mwanza leo asubuhi
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka mia moija tangu kuanzishwa kwa kanisa la Africa Inland Church Tanzania leo katika uwanja wa michezo wa Kirumba jijini Mwanza leo asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. FOR YOUR INFORMATION ONLY...! NEXT COMMANDER IN CHIEF HIS EXCELLENCE JM!

    The John Mashaka Charitable Foundation is a 501 (c) (3) entity established and funded by John Mashaka, in order to fulfill his dream and desire to use the fruits of his blessings, to help people living under massive poverty, get clean water, and also provide assistance to those living with HIV/AIDS virus get free medical attention they would not otherwise obtain.

    The Foundation is also focused on raising environmental conservation awareness in the remote villages of Tanzania (Mara Region) that are suffering environmental degradation. The JMF will also provide humanitarian assistance to the persons in need in the State of North Carolina, and elsewhere where there is need. John Mashaka Foundation hopes to make lives of the people in these regions more rewarding, and worth living. The Board of Directors of the John Mashaka Charitable Foundation seeks to further John Mashaka’s dream by providing humanitarian relief assistance through.

    Assisting the inhabitants of the remote villages in Mara have access to clean water

    Provide resources (support) to the HIV\Aids victims would not afford the antiretroviral

    Provide, the necessary awareness, education and resources to people in the region on effects and importance of environmental conservation in Tanzania

    Assist at Risk children (orphans), obtain basics of life such a shelter, education, food, and clothing

    96% of all donations go directly to JMF’s charitable projects, administered by JMF Tanzania and monitored by JMF- USA.

    The Foundation operates to help the disadvantaged, the at-risk and the needy, whether these conditions have arisen because of financial, medical or other circumstances. The Foundation strives to help this target population help themselves to make better and more meaningful lives for themselves and for their families.

    Please join us in the effort to “fight for the common good of man".

    Thank you,

    JMF

    ReplyDelete
  2. Michuzi huku dsm leo kumekuwa na kauvumi kanakosemwa semwa kuhusiana na ugeni huo huko Mwanza. Kuna ukweli wowote au ni kauvumi.Can u confirm. Dar ni too much for being jiji la uvumi a.k.a rumorvillet

    ReplyDelete
  3. Bwana michuzi mada yangu ya "My vision for Tanzania" utaiweka lini kwenye blogu ya jamii ili nami nipate nafasi ya kuwakilisha umma. ama ndio kapuni..naomba unianikie mada yangu ili nami nipate feedback za watanzania wenzangu kama ilivyo kwa john mashaka.

    ReplyDelete
  4. uhuru wa Yesu....ni wa milele

    ReplyDelete
  5. Eee bwana Michuzi eti naniliu, eti hapo leo JK alianguka jukwaani na kuzimia akakimbizwa hospitali eti ni kweli au radio mbao tu?

    ReplyDelete
  6. Ingependeza zaidi kama tungeona heading apo juu kua JK APATA SULUHISHO LA MGAWO WA UMEME, au JK ATOA SULUHISHO LA KISIASA VISIWANI, na kadhalika

    ReplyDelete
  7. Anonymous wa Tarehe Sun Oct 04, 09:35:00 PM,

    Umenibariki sana na hiyo msg ya Uhuru wa yesu...Yani unikumbusha AIC Magomeni kutumia Tenzi za Rohoni na nyimbo za sifa......Amani ya bwana...ni ya milele....Gete gete


    Mwana harakati

    ReplyDelete
  8. Mhola ya sebha! Mu Yesu.
    Miaka mia si mchezo kwa kwelu uhuru wa YESU ni wa milele
    Amen

    ReplyDelete
  9. Raisi wetu ni mgonjwa,unasumbuliwa na tatizo la ku-zimiaX2 ghafla(a nerve problem on part of his brain)tatizo ambalo amekuwa nalo hata kabla hajawa Rais wetu.
    Inasemekana Raisi wetu ameshauriwa kwa mara kadhaa kuwa tatizo hili lahitaji upasuaji,lakini amekuwa mzito kuukubali ushauri huo wa kitabibu.
    Uongozi wa nchi una presha na mikikiX2 ya kila aina,kampeni 2010 zipo ukingoni,twajua mswala ya Afya hufanywa siri ktk utamaduni wa-kibongo,ila Rais wa nchi ni muwakilishi wa wananchi, kwa maana hiyo naelekea kufikiri kuna kila sababu ya kujali/kujua afya ya Rais wetu.
    HAKUNA MAANA YA FAMILIA/WASAIDIZI WAKE(haswa tabibu wake)KUFANYA SIRI JUU YA TATIZO HILI.
    Raisi mstaafu Mkapa alisumbuliwa na tatizo la mguu,umma ulielezwa akafanyiwa upasuaji,Dr.Shein kwa kushirikiana na viongozi wenzake alikaimu Uraisi wa Nchi yetu vema kabisa!!
    RAISI KIKWETE TAKE SOME TIME OFF THE OFFICE DUTIES,GET YOURSELF SOME MEDICAL TREATMENT BEFORE IT IS TOO LATE!!!-we love you.

    ReplyDelete
  10. He fainted??!!!! apumzike basi ili atupunguzie gharama tunazomlipia, anapiga sana misele!

    soma hii;

    Uchovu wamlemea Rais Kikwete


    Rais Jakaya Kikwete

    Rais wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete leo amelazimika kukatiza hotuba yake ghafla akionekana mchovu, na kuomba kuhutubia akiwa amekaa, jambo ambalo hata hivyo alilikatiza na baadaye kuondolewa kwenye jukwaa katika uwanja CCM kirumba mjini Mwanza na kwenda chumba maalum kwa ajili ya mapumziko mafupi.
    Hali hiyo imetokea wakati Rais Kikwete akihutubia maelfu ya waumini wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania katika madhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kanisa hilo nchini. Rais Kikwete alikatisha hotuba yake baada ya kutojisikia vizuri huku sauti yake ikisikika kudhoofu kama mtu ambaye amepatwa na matatizo.
    Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu DAR ES SALAAM kwa vyombo vya habari imesema Rais Kikwete alilazimika kupumzika kutokana na kuzidiwa na uchovu kufuatia shughuli nyingi mfululizo katika siku za karibuni. Hata hivyo baada ya mapumziko ya muda aliendelea kushiriki katika shughuli hizo hadi mwisho.
    “Nguvu imerudi…napenda sasa kuchukua nafasi hii kuzindua rasmi uchangiaji wa shughuli za Kanisa lenu na mimi naanza na mchango wa sh. 1,000,000,” Rais Kikwete aliwaambia maelfu ya waumini wa AICT huku wakimshangilia kwa nguvu mara aliporejea jukwaani.
    Rais Kikwete alianza kusikia uchovu wakati akisoma hotuba yake mbele ya maelfu ya waumini wa Kanisa hilo. Rais huyo amekuwa na shughuli nyingi na hajapumzika katika miezi kadhaa iliyopita kutokana na kazi nyingi na ratiba ya shughuli za mfululizo.
    Aidha ndani ya siku 15 zilizopita, Rais Kikwete amekuwa New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, na kwa siku mbili zilizopita alikuwa mjini Arusha kabla ya kwenda mjini Mwanza na leo kuhudhuria maadhimisho hayo ya Kanisa la AICT.
    “Kwa kweli mshituko huu wa leo ni matokeo ya ubishi wangu. Nilishauriwa na wasaidizi wangu nipumzike baada ya kurejea nyumbani kutoka Marekani. Niliambiwa nisiende Arusha ama kuja hapa. Lakini nikakataa. Siku nyingine nitawasiliza zaidi.”
    Rais Kikwete aliondoka kwenda Marekani kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) Septemba 20 na tokea hapo hajapata kupumzika. Alirejea nchini kutoka Marekani saa saba usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya kuwa amesafiri kwa zaidi ya saa 19 na asubuhi ya Ijumaa akasafiri kwenda Arusha kufungua Mkutano wa 55 wa Wabunge wa Jumuia ya Madola.
    Rais alikuwa amepangiwa kurejea Dar es Salaam baada ya shughuli ya Arusha, lakini akalazimika kwenda Mwanza kwa shughuli ya Kanisa la AICT kwa sababu Waziri Mkuu aliyekuwa amepangiwa na Rais kushiriki shughuli hiyo alipewa kazi nyingine na Rais.
    Hii ni mara ya pili rais Kikwete kupatwa na hali kama hiyo. Mara ya kwanza hali kama hiyo ilijitokeza wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka 2005 katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam. Wakati huo Rais Kikwete alikuwa akihutubia mikutano ya kampeni huku akiwa amefunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
    Kwa jijini Mwanza hili ni tukio la pili kumtokea Rais Kikwete akiwa katika uwanja wa CCM Kirumba baada ya mtu mmoja kumvamia alipokuwa katika mkutano wa kampeni 2005 wakati akiomba kura kwa wakazi wa Mwanza. Mtu huyo alishtakiwa na kufungwa baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia mgombea urais wakati wa kampeni.
    Wakati huo huo, Ofisi Binafsi ya Rais (OBR) imetangaza kuwa itaangalia upya ratiba ya Rais wa Tanzania kwa lengo la kumpungumzia mlundikano wa shughuli.
    Ofisi hiyo ndiyo husimamia kupanga ratiba za Rais. Baada ya tukio la hilo imetangaza rasmi kuwa inaangalia upya ratiba nzima ya matukio yajayo ili kuyapunguza na kumpa muda zaidi wa kupumzika.

    http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2009/10/091004_kikwete_health.shtml

    ReplyDelete
  11. sebha akojiwe.....Amen
    Mhola ya Sebha.....Yesu

    ReplyDelete
  12. JK ufisadi wake sio kama EPA yeye anakusanya kidogo kidogo,posho za safari.

    ReplyDelete
  13. Pole sana Rais wetu.

    ReplyDelete
  14. Mhola ya Seba,
    Myesuuu'
    Lina la Yesu likojiwe

    Wabeja sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...