JK akimlisha keki Mama Salma Kikwete katika hafla fupi ya kifamilia iliyofanyika ikulu jijini Dar jana jioni kusherekea hepi besdei ya miaka 59 ya kuzaliwa kwake.
JK akipongezwa na wanawe Rashid Kikwete Chodo (aliyemshika mkono),Khalfan Kikwete,( wapili kushoto) na Lulu Khalfan Kikwete ambaye ni mtoto wa mdogo wake.Aliyekaa pembeni nyuma ya Rais akiangalia ni Mama Salma Kikwete aliyeandaa hafla ya kifamilia ya kumpongeza Rais kwa kutimiza umri wa miaka 59 jana.

JK akizingumza na aliyekuwa Rais wa Ireland Mhe.Mary Robinson ambaye sasa ni Rais wa Taasisi ya Realizing Rights,wakati Bi.Robinson alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.
JK akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana(picha na Freddy Maro)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. happy B`DAY mr president!!for ever JK.

    ReplyDelete
  2. Jamani makochi hayo ya ikulu yamechakaa. Tokea enzi ya mchonga nini? Halafu huo ukuta ni matofali au? Madhari sio nzuri kabisa

    ReplyDelete
  3. mama yetu salma basi hata busu kumpa hubby wake? na watoto wameshindwa kumpa baba yao "bear hugs" ni wanamwogopa au? manake JK anaonyesha ni mtu ambae unaweza kuchat nae bila ya kuogopa. enewei kwa umri aliofika anaonekana bado ni kijana sana, michu raisi wetu anakula nini? manake angekuwa mtu mwingine ni angekuwa kachoka kabisaaaaaa au ndio hizo safari za kila leo anapata kupumzika sana.

    Happy B'Day our President

    ReplyDelete
  4. afu raisi wetu ana mke huyu huyu hana mwingine?? au ndio huyu leo kavua vitenge? sielewi hebu nifahamisheni. nakumbuka raisi wetu mwinyi alikuwa nao wawili, sasa je JK

    ReplyDelete
  5. Makochi hayo yanaonyesha wanachezea watoto. Si unaona watoto bado wadogo,watoto wadogo kama kawaida yao wanarukaruka sana kwenye makochi. Nyumba nyingi zenye watoto wadogo makochi yanachoka tu.

    JK hongera kwa 59. Nakutakia Afya njema.

    Pambana na mafisaidi. Watanzania wanakutegemea wewe uwaandalie mazingira mazuri ya kufanya kazi ili kuinua kiwango cha maisha yao.

    ReplyDelete
  6. Kheri ya sikukuu yako ya kuzaliwa, JK!Mh, lakini hao watoto kama wajukuu vile. Teh, teh, teh, mzee mzima!

    ReplyDelete
  7. Congraturation our President ! happy birthday to you and to your family (Tanzanian family )baba akila keki anaakikisha wato wake wameshiba ubwabwa!pita mitaani njaa kali baba......kuhusu picha na watoto haiko presentable kuwekwa kwenye media maana picha ya raisi inabidi kufanyiwa kazi before publication isije ikaleta mtazamo mwingine kwa audience..huu ni ushauri wa bure as Journalist ,maana hii blog inaangaliwa na watu wenyewe mitazamo tofauti......
    In general happy birthday to you!
    Mtu wa safari...

    ReplyDelete
  8. mbona simuoni Bwana Mohammed hapo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...