Kocha Mkuu wa Yanga, Mserbia Kostadin Papic akisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuinoa timu hiyo katika hoteli ya Movenpick jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Shoto ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Iman Madega na kulia ni Katibu Mipango, Patrick Fata.
Juu na chini ni kocha mpya wa timu ya Yanga, Mserbia, Kostadin Papic, akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo wakati wa mazoezi kwenye viwanja vya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST). Kocha huyo ameanza kazi rasmi baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hivi kwa nini timu za Tanzania hususani Simba na Yanga zinapenda kuchukua makocha kutoka Serbia...wadau ningependa mnijuze juu ya kiwango cha soka cha huko Serbia na ujuzi pia wa hao makocha. Na je timu iyo akipewa Mkwasa nakupewa mshahara mzuri na support haitaweza kufanya vizuri??Mimi hawa makocha wananipa kichefuchefu tu..haaaaaaa!!!!Madega mwanasiasa bora ukagombee ubunge uko Chalinze...pumbavu watu wanaingia kwenye uongozi wa michezo kwa malengo ya kisiasa...nyambafuuuuuu

    ReplyDelete
  2. Hahaha! washaona moto unakuja na hauepukiki, wanajua wakichapwa watasema kocha bado mgeni!!!! good 4 us Simba SC. Kweli mna chairman anayeona mbali!!!

    ReplyDelete
  3. mwanangu hii pic ya pili,hawa dogo's wanaonekana ka wala hawamuelewi huyu fundi BOMBA toka Serbia anasema nini,Lugha nadhania huwa inakua boooonge la shida huko kambini kwao.

    ReplyDelete
  4. Huyo kocha amejitayarishaje na yaliyomkuta mwenzake Kondic, maana alianzia New Africa, akaenda valley view na akaishia klabuni achilia mbali mambo ya mshahara na gari ambapo sasa anatembelea basi la timu!!! hiyo ndiyo bongo, karibu sana msebia naona wewe shughuli yako itaisha mapema mwishoni mwa mwezi huu.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza Serbia ni sehemu ya iliyokuwa Yugoslavia. Timu yao ilishiriki katika mashindano ya kombe la dunia ya 2006, japo hawakufurukuta. Wameshajikatia tiketi kwa ajili ya mashindano ya mwakani.
    Uzuri wa kocha hautokani na alikotoka bali anachoweza kufanya. Miongoni mwa makocha waliofanya mambo makubwa Tanzania kwa miaka ya karibuni ni James Siang'a ambaye ametokea Kenya tu hapo. Kiwango cha soka Kenya na Tz havipishani sana. Kwa upande mwingine King Abdallah Kibaden mputa amefanya mambo makubwa nchini kwa kuifikisha Simba fainali za CAF na ni kocha mzalendo. Dragan Popadic alikuwa Myugoslavia (sijui kama alitokea Serbia, Croatia au Slavia) naye alifundisha soka likaonekana. Lakini kuna kocha kama Micho ambaye mpaka anaondoka ilionekana kama ameleta usanii tu. Kondic naye alionyesha kujua kushinda ligi ya ndani tu, timu yake ikiona waarabu inatandikwa thelatha mpaka hamsa.
    Mwachieni nafasi Papic aonyeshe ujuzi wake, kama mweupe tutajua tu.

    ReplyDelete
  6. U-Kanumba unapanda hapo, au ndo lugha za kibubu tu zinazotumika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...