DAKIKA ZAYOYOMA NA SASA NI WAKATI WA MAJERUHI NA MFADHILI WA MDAU WA MILIONI 7 BADO HAJAPATIKANA. UKIANGALIA HESABU CHINI KABISA KULIA UTAKUTA DAKIKA ZAHESABIKA KABLA HESABU HAIJAGOTA MILIONI 7. NAONA SAFARI HII ZEGE LINALALA....
- MICHUZI
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Michu,
ReplyDeleteMie ndo mdau wa milioni saba!
SAC
Bro michuzi hii nilihisi kabisa ni mimi kumradhi japo bado mfadhili hajapatikana ila itakuwa ni mimi mdau wa milioni hizo bana!kazi njema!
ReplyDeletebreaking news: mie nikishinda itabidi uniapishe niwe mkuu wa wilaya ya nanii.
ReplyDeletehatimaye nimeibuka mdau wa milioni saba baada kuitafuta kwa muda. Kiambatanisho kimetumwa kwenye barua pepe..! Lakini ndio hivyo tena ng'ombe wa masjikini hazai, akizaa limezaliwa dume.
ReplyDeletenimeibuka mshindi michuzi nimepiga picha hizo namba sasa je email yako mbona hujaweka ntatumaje ili u prove
ReplyDeletemkuu wa wilaya uza hilo shangingi ili tuendeleza utamaduni wetu wa zawadi kwa kila milioni inapogonga.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteMara hii nitakuletea proof kukuonesha kuwa mshindi wa anaweza kuwa zaidi ya mmoja. Nakumbuka last time nilikwambia lakini ukabisha sana.Sasa mara hii nimekusanya vizibiti vyote ili nikuoneshe kuwa zoezi hili ni kiini macho.Mie ndio mshindi wa milioni saba.Picha za screen nnazo na video pia nimechukua.
- imekula kwako!..
ReplyDeleteHuyo Mashaka unayembandikia maujiko yake hapa kila kukicha yuko wapi?! Acha Ubakhili bw. Mashaka, hebu toa mshiko kunakshi blog hii muhimu!
ReplyDeleteBalozi Michuzi,
ReplyDeleteUkiacha kubana maoni ya wadau (self-censorship) ambao hawachafui hali ya hewa, pengine blog yako itapata traffic zaidi. Naona hata wewe mwenyewe ukiangalia utakuta watu wachache sasa wanaacha maoni yao, mmoja wao ni mimi kwa kuwa hatusumbuki tena kukupelekea maoni wakati wewe unabana kwa sababu zako wewe binafsi.
Pili, hali ya uchumi ni mbovu. Sio rahisi kupata fedha hata kama ni dola 1000 kirahisi. Ushauri wa bure ni kuanza kuchaji wadau kama wale wanaotangaza biashara. Bongo siku hizi kila mtu ana uwezo wa kuwa na credit card au namna moja au nyingine ya kukulipa hata wakiwa nje (paypal, etc).
CHEKA UNENEPEZZZZZZZ
ReplyDelete..[ mlio wa simu ya mezani unasikika toka ndani, inaita]**N'gree!!, N'gree!! N'gree!! N'greeeee!!!**
**Aloooo?'**
**Hallllo, hujambo, mama!..'apo salama, mwanangu?!**
**salama. sh’kamo’ Daddy!**
**Marhaba, mpenzi..mama'ako yu wapi, yupo hapo karibu?**
**'apana, Daddy**
**Mama yuko na Anko Paulo..kasema anaenda mwonyesha kitu chumbani kwenu, huko juu'**
..pumzi inapanda-pumzi inashuka..kimya kinatawala, halafu,
**' Anko Paulo?!!!! Paulo yupi, mama?..mna Anko Paulo, nyinyi?'**
**'Ndio, Anko Paulo huyu huyu, daddy..na hapa nikwambiavyo wapo na
Mummy chumbani, huko juu'**
Kitambo tena! ..huku bado pumzi inapanda-pumzi inashuka..
**'Mmnh,haya!! Sikiliza mwanangu mpenzi, acha simu hapohapo mezani,
kimbia hadi juu, mgongee mama'ako na sema kwa sauti kuubwa ili
wakusikie chumbani "mama!, Daddy amefika, ndo anapaki mbele ya nyumba.'**
**'aya! sawa Daddy, naja!'**
punde, binti anarejea kwenye simu, pumzi zimempaa:
**'memwambia, Daddy!!!'**
**'good girl! Halafu, mpenzi?' **
*'Yaani, imewashtua sana!! Baba, mama katoka chumbani 'uchi wa
mnyama'..kakimbiiiia ovyo..kajikwaa, daddy..kagonga kichwa chini,
mama yu kimyaaa..hatingishiki, daddy..hanijibuuu!!!!'**
**'Oh my God!!! Na Anko Paulo wako. Yu wapi?'**
**'Naye si akaruka nje ya dirisha, vilevile alivokuwa! hana hata upande
wa khanga, wazii..naona alilenga atumbukie mwenye swimming pool pale
nyuma. Sijui hakufahamu kua limetolewa maji lisafishwe? Masikini, nahisi
kafa, daddy - kichwa chaakee, Kichwa chake, daddy, kiko
'meng'emeng'e!!.'**
kimya tena,
halafu kimya, jiiiiii
halafu kimyaaaaaaaaaaaaa, kingi, zaidi
Halafu,- t-a-r-t-iiiiiibu, kwa ki-gu-gu-mi-zi cha taharuki, kauli ya kupima, neno moja likimdondoka na kufuatiwa na jingine, Daddy anauliza: 'Swimming pool!!!!!!!???, pool ipi? gani???...... kwaniii, kwan' hapo..hapo niiiiii Tegetaa, nambaaa
2172335-oooooooo?'
Kabinti kanajibu, kwa sauti ya kukokoteza, iliojaa wasiwasi, huzuni na kilio:
**apanaa, sivyo, daddy.. umesahau kwetu, kwaaako, daddy?....'apa
Masakiii.......
..ghafla bin vuuuu, simu inasikika ikikatika ‘kata!!!!!'..
daahh!! kitita kimeangukia kwangu
ReplyDelete