Mkuu wa Yacht Club Comodere Spiros (kushoto) akimkabidhi kikombe cha ushinda wa uvuvi wa kutumia boti Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo yaliyofanyika katika Kisiwa cha Sinda katika Bahari ya Hindi jumla ya nchi Nne zilishiriki Mashindano hayo,mwishoni mwa wiki.
Washindi wa shindano la kuvua samaki kwa kutumia maboti wa Timu ya Black Widow wakiwa katika,picha ya pamoja baada ya kuibuka washindi (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, Linda Wiechers Raoul Dippenaar,na Christo Human wakiwa na vikombe vyao katika kisiwa cha Sinda kilichopo katika Bahari ya Hindi,Mwishoni mwa wiki.
Samaki mkubwa aina ya Papa mwenye kilo 157 aliyekuwa mkubwa zaidi baada ya kuvuliwa na Len Botha wa Afrika Kusini katika shindano la Maboti ya kuvua samaki akipimwa kwenye muzani katika kisiwa cha Sinda, shindano hilo lilizishirikisha Nchi Nne yakiwa yamedhaminiwa na Vodacom Tanzania,Mwishoni mwa wiki.



Watoto wakiwashangaa samaki waliovuliwa jinsi walivyokuwa wakubwa.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. KISIWA CHA SINDA KIPO NCHI GANI. (SERIOUS)

    ReplyDelete
  2. Walikuwa na kibali cha uvuvi?

    ReplyDelete
  3. Watoto wakibongo wako wapi?

    ReplyDelete
  4. Ndio maana wavuvi haramu walikuwa wanavua upande wa Tz. Bado tuna hazina kubwa sana baharini

    ReplyDelete
  5. wewe mtoa maoni Tarehe Mon Oct 05, 04:14:00 PM acha uvivu hapa hebu google hicho kisiwa upate habari.

    ReplyDelete
  6. This is cruelty against Animals! Shame on you those wazungu. They should catch and toss back in the ocean!

    ReplyDelete
  7. Wanapelewa wazungu kuvua, wangepeleka wazee wa gezaulole waone ni kiasi gani cha samaki kingepatikana. na vimitumbwi vyao vya kulalia upande lakini wanapata samaki kibao sembuse wangetumia hayo maboti ya kisasa.

    ReplyDelete
  8. kaka trio dar yatch club ni members tu na asilimia kubwa ni wazungu ndo sababu huoni watoto wa kimatumbi ni hayo tu by the way hata wewe unaweza kuwa memba mshiko wako tu

    ReplyDelete
  9. Naunga mkono maoni ya Mobit.. kuwa wangevua hao samaki, wakawapiga picha kisha wawarudishe baharini.. huwa naangalia documentary za "National Geography" .. ndivyo huwa inafanyika katika nchi mbalimbali.. na si kuwavua na kuwaua.. nadhani idara ya uvuvi wanatakiwa kutoa angalizo hili.....

    ReplyDelete
  10. Hii Yatch Club ipo tangu enzi za mkoloni na kuwa mwanachama ilikuwa lazima uwe na 'yatch'.

    Marehemu Mzee Mwakitwange alikuwa mojawapo wa ma-'member' hivyo wapo waswahili wenye interest/ hobby ya 'angling' na 'yatching' ambao ni wanachama.

    Pia hao samaki baadae huwa 'barbeque' safi, yaani 'ndafu' kwa wanachama ktk klabu yao hivyo hakuna haja ya lawama ya ukatili wa wanyama, hicho ni kitoweo.

    Tanzania tuna vivutio kibao vya watalii na wakazi wa Tanzania kupumzikia, ila tu wabongo hatuna interest ya kuvichangamkia.

    Michuzi hizo picha za Bilila Kempinski Serengeti na masuala ya 'yatching and angling' ktk pwani ya bahari ya Dar-es-Salaam ni kielelezo Bongo ni tambarare.

    ReplyDelete
  11. HIVI SISI WABONGO TUMELAANIWA NINI? MBONA WAVIVU WA KUFIKIRI NA KUFANYA TAFITI?? UVUVI WA AINA HII UMEPIGWA MARUFUKU NCHI NYINGIIII SIE NDIO KWANZAAAA TUNARUHUSU!

    ReplyDelete
  12. Watanzania tuache kuigiza, ooh National Geography documentary' hutupa au kurudisha samaki majini.

    Sisi hatuchezei chakula ndio maana samaki hao wataliwa na member wa Yatch Club na mahotelini.

    Mbona Japan wanaendelea kuvua nyangumi kwa faida zao za kiuchumi.

    Na Watanzania tuendeleze kuvitangaza vivutio hivi kwa ajili ya utalii na chakula bora.

    Gail Saltz.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...