Mama Maria Nyerere aliyevaa (nguo ya kijani) akipokea zawadi ya picha ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka kwa Dk. Costansia Rugumamu (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa . Picha hiyo ni moja ya vionyesho vilivyotayarishwa na bodi hiyo wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana yanayomalizika leo kijijini Butiama katika wilaya ya Musoma mkoani Mara. Kilele cha maadhimisho ya wiki hiyo kitakwenda sambamba na sherehe za kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru pamoja na kumbukumbu ya miaka kumi tangu kufa kwa Baba wa Taifa zitakazofanyika katika kijiji hicho.
Bibi Albina Nzagalila kutoka wilayani Sengerema mwenye umri wa miaka 89 akiwa anasali kwenye kaburi la Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo katika kijiji cha Butiama wilayani Musoma mkoani Mara. Bibi huyo ameenda katika kijiji cha Butiama kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka kumi tangu kufa kwa Baba wa Taifa kwani mwalimu wakati wa uhai wake alikuwa anamtunza na walishirikiana katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Wasanii wa Kikundi cha Waelimishaji rika Jamii kata ya Kiriba (KIWAJAKI) wakicheza ngoma ya Munenguro ya kabila la Waruli. Kikundi hicho kilikuwa kinawaburudisha wananchi wa kijiji cha Butiama kilichopo wilayani Musoma mkoani Mara wakati Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika kijiji hicho jana kwa ajili ya kuuwasha mwenge wa Mwitongo.Mwenge huo unatarajiwa kuzimwa leo katika kijiji hicho huku ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya miaka kumi tangu kufa kwa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Waruli hongereni sana. Wanajiita watoto wa kosti ni wacheshi sana hawa! Wapi ule mzuka wa jombole siku hizi?

    ReplyDelete
  2. wabahati wangekuwa wakati wa MCHONGA mwenyewe na hizo nguo za bendera ya taifa wangeena "lupango"kabla ya shoo yenyewe au unasemaje ankonaniiiiiiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...