Mshindi wa Bongo Star Search 2009, Paschal Cassian, katikati akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Mil.25 toka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Ephraim Mafuru na Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Productions Madame Rita Paulsen baada ya kuibuka mshindi katika fainali zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Shinadno hilo ambalo limefana sana mwaka huu limeandaliwa na Benchmark na Kudhaminiwa na Vodacom kama wadhamini wakuu
Paschal Cassian akiwapagaisha mashabiki wake wakati wa fainali za BSS.

Kanda ya Ziwa imeendelea kutesa katika anga ya burudani ambapo juzi usiku mshiriki wa shindano la kusaka vipaji la waimbaji (Bongo Star Search) kutoka Mwanza, Pascal Cassian aliibuka kidedea katika shindano hilo.

Ikiwa ni siku ya 12 baada ya kumalizika kwa kinyang’anyiro cha kumsaka mnyange wa Tanzania (Vodacom Miss Tanzania 2009), kutoka Mwanza Miriam Gerald kung’ara katika mshikeshike huo imeweza kuiwekea historia mkoa huo kutoa washindi mfululizo ndani ya mwaka huu.

Kutokana na ushindi huo Miriam aliyetwaa taji hilo na kunyakua zawadi zenye thamani y ash mil. 61 ikiwa ni gari ya thamani ya mil.53 pamoja na fedha taslim sh mil.9.

Aidha kutokana na ushindi huo Cassian amezawadiwa mfano wa hundi ya fedha yenye thamani kiasi cha sh.mil. 25 toka kwa wadhamini wakuu wa fainali hizo Vodacom Tanzania.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa mshiriki kutoka Kigoma Peter Msechu ambaye amepata zawadi y a sh mil.5, mshindi wa tatu ni Kelvin Mbati aliyepata kitita cha sh mil3.5.

Huku katika hatua nyingine mshiriki kutoka Tanga Jackson George aliyepata sh mil.1.5 na wa tano ni Beatrice William aliyepata sh mil 1,huku washiriki waliofanikiwa kuingia kumi bora kila mmoja akiibuka na sh.400,000.
Mbali na Vodacom, BSS mwaka 2009 imedhaminiwa pia na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro, Family Health International, Tansoma Hotel na Maji ya Kilimanjaro.
Mwisho.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. against all odds. PAVAROTI hatimaye ameshida

    ReplyDelete
  2. wanazilipia Tax hizo pesa walizoziingiza lkn hao..au ndio magumashi tena

    ReplyDelete
  3. Popular choice! Nadhani Kelvin atakuwa down sana, make alisifiwa saaana kwenye mchakato lakini hatimaye mambo hayakwenda vizuri.
    Rita, big up, ila fanya marekebisho yafuatayo ili ya mwaka kesho iwe nzuri:
    1. Judges wapate seminar na waangalie vipindi kama hivyo elsewhere. Majaji wote walikuwa na mapungufu. Rita was highly predictable, yaani alikuwa ni kusifia na kutia moyo tu. "You are good, you are a star, big up man...."
    P-Fanki alikuwa mtambo. He was not humerous, he was just rude! na kuwafanya waimbaji wapoteze confidence.
    Master J alikuwa anaongea kwa sauti ya fitina. Ile ni burudani sio kuponda.
    Salama alikuwa sio funny, she was like Kungwi fulani kama vile youko pale kutoa ushauri badala ya kujaji
    Kitine ndiye alikuwa jaji ki-ukweli.

    So, pia kwenye benchi awekwe mtu ambaye ni mwimbaji anayefahamika, sio producers and radio djs tu. Tusker ilikuwa credible zaidi b'se of Juliana Kanyomooooooooooozzii.
    Otherwise, great show, congrats Benchmark.

    ReplyDelete
  4. NI kweli he reminds me of Luciano Pavaroti, akiimba opera ananifurahisha sana japo Master Jay alikuwa mwanzo hamuelewi. Mwakani waende na mikoa ambayo hawakupita kama huko kwa wamang'ati(Barabaig) na watindiga (wahazadbe) kuna vocals pia.

    ReplyDelete
  5. Kelvin aliponzwa na Rita, she was just too much for him hata akifanya vibaya siku hiyo. Sasa wapiga kura tukaboreka.Mgema akisifiwa tembo hulitia maji. He created a false confidence.

    Catherine was a star ila wabongo hawaelewi uimbaji wake angeingia Tusker Fame project labda ingekuwa ndiyo level yake.

    ReplyDelete
  6. Mzee Michuzi naona umeniangusha. Nilikuomba unitolee tangazo la kutafuta business partners kwenye mambo ya burudani, especially wa kusaka vipaji, wiki mbili zilizopita.

    Nilikuwa natarget baadhi ya vijana hawa. Naweza kukutumia tena labda ilipotea njiani au ulisahau tu, mimi siyo tapeli mzee.

    ReplyDelete
  7. USHAURI KWA WAANDAAJI; MMEFANYA VIZURI KUONYESHA JINSI KURA ILIVYOKUWA ZINAENDA WAKATI ONYESHO LINAENDELEA LAKINI HIYO KITU WANATAKIWA WASHINDANI WASIJUE. MMEWAVUNJA MOYO SANA WASHIRIKI WENGINE BAADA YA KUJUA WANA KURA CHACHE.
    PILI; SI VIZURI SANA NA INAPUNGUZA MSHAWASHA KUTAJA WASHINDI MMOJA MMOJA KUANZIA WA TANO MPAKA WA KWANZA. NI VIZURI KUANZA WALE WA TANO MPAKA TATU NA KUWABAKIZA WAWILI WA JUU NA KUWAWEKA ROHO JUU KWA MUDA, HALAFU MNATAJA MSHINDI WA KWANZA TUU. MSHINDI WA PILI ATAKUWA AUTOMATICALLY AMESHATAJWA.
    MSIFANYE MAMBO YAWE SO PREDICTABLE

    MZOZAJI

    ReplyDelete
  8. Duh Hongera sana Madam Rita na genge lako la majaji zingatieni usauri mliopewa nextime ijayo

    ReplyDelete
  9. Mzozaji
    Nakubaliana na wewe kabisa, Host wa show ali haribu alipo sema wale top 2 warudi backstage,wengi tulitaka kuona reaction ya Pascal anapotangazwa mshindi, miaka yote waliyo fanya mshindi analikua anatangazwa akiwa kwenye stage , hiyo iliharibu excitment kabisa.

    Kwa mara ya kwanza nimeenda kwenye show nimetoka ni kiwa happy , uandaaji ulikua mzuri na fairness tumeiona, mimi nilikua mshabiki wa Kevin , lakini hali nilio iona live mle ndani nakubali kabisa Pascal ana stahili , na dhani asinge tangzwa yeye kunge tokea vurugu maana ushabiki wake mle ndan ulikua sio wa kawaida , kwenye TV ilikua huwezi ona hilo.

    ReplyDelete
  10. michuzi sisi tulio nje ya nchi tunawezaje kuona hata kipande kidogo anachoimba huyo mshindi na wengineo>naomba update basi youtube jamani please

    ReplyDelete
  11. pascal made me cry. his baritone voice and the way he manipulates it proved master J wrong. J himself conceded. go pascal! this shouldn't be the end.

    ReplyDelete
  12. Kweli Kelvin Martin anaimba vizuri ila aliponzwa na Madam Rita kwa kumsifia sana.

    ReplyDelete
  13. Nampongeza saaana madame Rita, ingawa nina wasiwasi na majudge aliowatumia. Hii imezungumzwa na mtoa comment moja hapo juu. Nampongeza sana sana mshidni wa bss 2009 Paschal Cassian, kweli alitoka mbali na kweli alikuwa anazingatia comments za majudge ingawa nyingine zilikuwa za kumvunja moyo sana hasa alizokuwa akitoa Salama Jabir. nakumbuka kuna siku Salama alimwambia Paschal hawezi kushinda bss na kama atashinda..... Salama knows what words she used.unapokuwa judge uwe judge wa ukweli, kweli kukosoa kupo lakini pia kama professional judge lazima ujue na kumtia moyo mshiriki.Kilichokuwa kinatokea kwa baadhi ya majudge ni kuwaponda sana washiriki hasa Paschal alipondwa sana na kuambiwa ana sauti za marehemu. Mh hongera Paschal na pole kwa yote, but hongera sana sana manake ulivumulia huku ukijifunza na kubadilika siku hadi siku hata umekyuwa mshindi.

    Madame Ritha na wewe kwa kelvin, mmmmmh ulishindwa kuhimili hisia zako, next time do not commit yourself kwenye game ya kumwagia mtu masifa kama ulivyofanya kwa kelvin, na hasa pale unapotegemea last judgement itoke kwa public.

    Kama noma na iwe noma, hiyo nimekwambia bibie.
    Hongera zako Paschal.

    ReplyDelete
  14. Mashindano yalikuwa mazuri, big up madame Rita na kundi lako. Ila ushauri wa bure kwa Kelvin na Catherine ni kwamba uimbaji wao ni wa juu sana kwa bogo star search, wao ni watu wa Tusker fame, pop idiols na kwingineko ambako wanaimba nyimbo international, sio bongo star. Msikate tamaa nyie ni internationals.

    ReplyDelete
  15. aisee kweli mmenena;
    1.catherine
    2.cassian
    3.kelvin (kidogo japo)

    uimbaji wenu ni wa KIWANGCO CHA JUU sana sana sana asa Catherine,watu wa kawaida tu ambao ndo walipiga kura kuchagua mshindi walikua hawaelewi na wasingeweza elewa,kiwango chako cha uimbaji ndo maana uyo mzungu anataka akubebe Belgium sijui!!
    awa ndo waimbaji wa kimataifa wal'lai vile...me mshindi ingekua kati ya catherine vs cassian

    ila catherine anaimba saaana yan ni wale ron kenoly/don moen/aretha fraklin/celin deon nk...ana kipaji cha asili kabisaaa...only P-FUNK ndo amegundua kiukweli

    hongera cassian wana mwanza twakupongeza hureeeey

    ReplyDelete
  16. Hingera Paschal kwa Ushindi mimi mwenyewe ulikuwa unanifurahisha,but kwa uimbaji wa Ukweli kabisa ni Catherine na Kelvin,sema si unajua watanzania tunapenda quantity na sio quality,ndio maana Paschal Kashinda.But he was good tho,
    Kuhusiana na mpangilio mzima wa kuwapa zawadi washindi kwa kweli walichemka pale walivyosema washiliki wawili wa mwisho waende backstage.that was bad,
    yaani ilitoa mshawasho kabisa hatukuona Paschal alihamaki vipi alivyotangazwa Mshindi, ni bomba kama mnawaona washiriki wakiwa pale juu wawili then anatangawazwa Mshindi kama mdau hapo juu alivyosema,

    Pili,
    Kuonesha matokeo,
    kuonesha matokeo ni noma sana siku ya mwisho na inapunguza hamu ya kuendelea kuwepo hapo,kama ndio jamaa yako anashiriki na anakura ndogo kuliko wote unaweza kuamua kwenda kulala tu,kuepuka kuumia.

    Hata mnaweza kufanya hata wale washiriki kushidwa kutoa burudani ya kutosha siku iyo.

    Kwa ujumla nawapa hongera waandaaji na majaji wote kwa kweli Mwaka huu mmetufurahisha sana.

    ReplyDelete
  17. aisee yaani ni kama nataka kurudia tu kwani yote niliyoyafikiria watu wameongea.
    1. Cassian was good kwani hata nami nilimfurahia but watanzania tucheki vipaji vya ukweli rem Catherine Ntepa ..that bint alideserve kuwa katika fainali
    2.Kelvin was good also but Madam anatakiwa atake lesson that asirudie kosa hilo ..alishindwa kuficha feelings zake kwa kijana kiasi ambacho ikawa inabore so tukajikuta tunamchukia Kelvin kwamba anabebwa so ikampunguzia mno kura
    3. ilikosa msisimko kwani mshindi alijijua aft yale matokeo ya kwenye screen washiriki wengine walivunjika kabisa moyo thats why round ya pili nyuso zao zilikuwa zimepwayaaaa....na hata alipotajwa winner haikuwa kama ya kina misoji au jumanne iddi ya unawaza mmh nani winner ao hapo hatukuona mshtuko wa winner kabisa
    4.otherwise majudge walikuwa ok mi nadhani am not so sure na wanaosema p funk hakuwa mzuri kwani alikuwa anaongea kilicho cha kweli mara zote

    ReplyDelete
  18. oooh nilisahau hapo juu na Msechu kilichomponza ni sifa ...sasa wabongo wakalinote hilo....usicheze na wabongo

    ReplyDelete
  19. maoni yangu ni kuwa, vyovyote iwavyo, iwe kujua au kutojua, ukweli ni kwamba yule jamaa wa mwanza alikuwa juu ya wote. ninani anasema huyu muimbaji ni bora? ni washabiki au majaji? ukienda kibiashara zaidi washabiki ndio wanajua ukweli, kwanza hawajuani, pili wao ndo wanunuzi wa kazi sokoni, ndio wahudhuriaji matamasha na ndio wanaoomba nyimbo radioni nk.

    Kwa msingu huo Cassian ni the best, Kilvin si lolote, ana pose za haza na pale lakini kimuziki hakubaliki ndo maana akapata kura chache. Naamini Cassian akiingia sokoni atauza juu ya kelvin. Watu wengi wanao muona kelvin bora ni wale wenye upeo wa kuona sehumu zingine, na wanamfananisha na huko. lakini hii ni tanzania, tunajua nini tunakipenda, nini kizuri na nini kibaya. madam ritha na salama na master j wanachojua ndicho walichokosea, walikuwa wa tatu tu, hivyo wao ndo walikokosea kujua kipaji halisi.
    Jamaa alistahili kushinda hakuna swali.

    ReplyDelete
  20. to me catherine was best,hata majaji walilijua na ndio maana wakampa nafasi nyingine ili watu wajitahidi kumpigia kura,nilichogundua kua watu walikua wanaangalia mahandsome boy na uzuri wa sura za watu but,pia nimegundua watu wengi wanaweza kumshabikia mtu bila kumpigia kura

    si kwamba cassian hajui kuimba ila sio mbunifu kama msechu ,kilichomsaidia kassian ni kupatia zile nyimbo alizokua akizichagua kuziimba na kudence hata ule wimbo wa mchizi mox,

    kelvin pia anajua kuimba sana ila nyimbo za kiingereza pia kudance tatizo,aliponzwa na maddame ndio maana watu hawakumpa kura za kutosha,
    msechu ni mbunifu saaana na ni msanii mzuri sana stagini pia anabuni utunzi wa nyimbo zake,

    majaji
    wasiponde wakosoe na wasiingilie personal issues mfano mavazi na wasimkatishe mtu tamaa mfano paschael alipondwa mno mara sauti ya marehemu,mara wewe sio mshindi wa mwaka huu wa bss ,mara lisauti lako likoje

    mwishowe watu wakampigia kura kwa hasira zote esp wa mwanza

    ReplyDelete
  21. Anafanana na zito kabwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...