
Balozi wa taji la bodi ya utalii anayefahamika kama Miss Domestic Tourism, Sia Ndaskoi, wa pili kulia, akipokea zawadi ya kompyuta kutoka kwa Mkurugenzi wa bodi ya utalii Peter Mwenguo leo jijini Dar. Mbali ya kompyuta mlimbwende huyo alikabidhiwa hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2 ikiwa ni mtaji wake wa kusambaza ujumbe wa umuhimu wa utalii wa wananchi. Shoto ni Mwandaaji wa Miss Tz Hashim Lundenga na kulia ni Mkuu wa Itifaki wa Miss TZ papaa Makoye. Katikati ni mama Mmari afisa mwandamizi TTB.
BALOZI wa taji la Bodi ya Utalii anayefahamika kama ‘Miss Domestic 2009’ Sia Ndaskoi jana alikabidhiwa zawadi zake pamoja na mikoba ya kutumikia rasmi taji hilo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Peter Mwenguo ndiye alimkabidhi zawadi hizo Malkia wa taji hilo huku akimuasa kulitumikia vyema kwa kuutangaza utalii wa ndani kwa warembo wenzake pamoja na vijana wa rika zote.
“Kutokana na kugundua watanzania wengi hawafahamu thamani ya Utalii ambao ni rasilimali iliyomo nchini mwao tumeamua kujikita kwa kuwekeza kwa miaka miwili katika shindano hili la Vodacom Miss Tanzania kutokana na umuhimu wa utalii” alisema Mwenguo.
Kutokana na ushindi huo Mrembo huyo amekabidhiwa zawadi zenye thamani y a sh milioni 3.3
Wakati akimkabidhi zawadi hizo Mwenguo alisema “ leo nina furaha kumkabidhi rasmi zake Balozi wetu wa kukuza Utalii wa ndani ambazo zitamsaidia na kumpa motisha ambazo ni Kompyuta ya Laptop aina ya Toshiba yenye thamani ya sh mil1,1030,000 pamoja hundi yenye thamani y ash mil.2,172,000”.
Alisema kama mtakumbuka Bodi ya Utalii (TTB) ikishirikiana na na Hifadhi ya Taifa (TANAPA), na Mamlaka ya bonde la Ngorongoro (NCAA) ilidhamini mashindano ya mwaka huu kwa gharama y ash mil 108 na fedha zenyewe zilituka katika kugharamia safari za warembo wote 30 waliotembelea Hifadhi za Serengeti, Geti la kwanza kupanda mlima Kilimanjaro- Marangu na bonde la Ngorongoro.
Mrembo huyo atatumika ipasavyo katika kutangaza Utalii wa ndani kwa njia mbalimbali kama kwenye vipeperushi na mabango mbalimbali ytakayotumika katika kampeni za kutangaza Utalii wwa ndani.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa Kamluni ya Lino International Agency ambao ndiyo waratibu wa shindano la Miss Tanzania Hashim Lundenga alimuasa mrembo huyo kuliheshimu na kulilinda taji hilo kwa hali na mali na asiwatie aibu.
“Sia wewe umepewa dhamana kubwa ya kuwa balozi wa kutangaza utalii wa nchi hivyo mimi na kamati yote ya Miss Tanzania tunatarajia utalitumikia kwa heshima hadi muda wako utakapomalizika japo kuwa natambua kwamba udhaifu wa kibinaadamu upo lakini kuwa makini”.
Naye Sia aliwashukuru TTB , Kamati ya Miss Tanzania na kuahidi kuto kwenda kinyume na taratibu za mila na desturi ya Mtanzania.
,
naomba kuuliza hivi ukuu wa itifaki ndio cheo cha aina gani ? msaada tutani
ReplyDeleteKweli huyu ni miss Domestic wao,kwani haya mambo huwa mnayafanya vp????.
ReplyDelete