Mgambo wa jiji wakiwa wamewafunga mashati wafanyabiashara ndogondogo baada ya kuwakamata wakichakarika katika eneo la posta mpya jijini Dar leo asubuhi.
Globu ya Jamii inalaani vitendo hivi kwa nguvu zote na kuwataka viongozi wa jiji, kuanzia Meya Alhaj Kimbisa hadi viongozi wa serikali za mitaa wajiulize upya endapo kama zoezi hili la zimamoto kila siku lina tija. Hao mgambo badala ya kulinda uharibifu wa mazingira bustani ya mnazi mmoja gaden ambayo inapigwa kufuri kila siku kwa kisingizio eti wamatumbi watachafua, kazi kuu waijuayo ni kunyanyasa machinga.
Hivi yale majengo waliyotengewa machinga pale Ilala mkabara na uwanja wa Karume mbona hayafuguliwiiiiiii??? Hawa ndugu zetu machinga wameacha kukaba watu na kujitafutia riziki mitaani, na wanaishia kwenye adha kama hii, wakale wapiiiiiii???
HAWA WATU WANACHEZA, TANZANIA INAKUJA KUPASUKA HIVI PUNDE. HABARI NDO HIYO, MAFISADI ATEMBEE NA MAGARI YA AC, WANAOTAFUTA CHAKULA WAFUNGWE, MBWA HAWA NAYANG'AU JONI MASHAKA HUKO WAPI, ANDIKA KITU KUHUSU HUU UJINGA ni kwa nini, DAKITARI SHAYO NA WEWE huko wapi? kama nyie ndow atetezi wa wanyonge, basi muonyeshe ujasiri wenu
ReplyDeletejamani jamani, hao ni walala hoi tu, jamaa ngoma zao ngumu na ndio maana wanaangaika. mafisadi na wauza unga wanaachwa mitaani, wachakarikaji wana laliwa. this iz no good
ReplyDeleteKweli mnyonge hana haki!!!!!!!! Mbona wala rushwa na mafisadi mnawaacha!!!!! Kwenu zenu huko hamna lolote nyie mgambo.
ReplyDeletehawa jamaa hata siwaonei huruma..Kwanza wanakimbia vijinini kuja mjini bila ya kazi...Pili katika wao ndipo wanazaliwa vibaka..Tatu wanawahifadhi vibaka na kuwajengea mazingira mazuri ya kuiba.
ReplyDelete..Mgambo kazi nzuri.
HAKIKA HUU NI UNYANYASAJI WA HALI YA JUU KUMBE WAKALE WAPI?? MBONA HAO MGAMBO WASIENDE KAMATA VIBAKA WANAO BAKUA MALI ZA WATU,WANAWANYANYASA WAMBACHINGA WANAO TAFUTA HELA YA KUWEKA UGALI MEZANI KWA WATOTO WAO NA FAMILIA ZAO??? TANZANIA TUTAAMKA LINI JAMANI? TUNANYANYASANA WENYEWE KWA WENYEWE SASA HII HUONI NI TAABU KUBWAAA?? VIONGOZI WAKOWAPI? VIONGOZI WANAOJIITA VIONGOZI WAKWAPII ?? SASA HAO WANAPELEKWA MAABUSU KWAAJILI YA KUTAFUTA MAISHA BORA KWA KUUZA VIFAA BARABARANI HUONI WATANZANIA TUMEKOSA ADAMU NA HATUHESHIMU UBINADAMU??? HUU NI UBAYA TENA NI KUVUNJIANA HAKI KABISAAA ZA BINADAMU.
ReplyDeleteHuo ni uonevu ambao umekuwa ukiendeshwa kwa miaka sasa na askari wasio na mafunzo yanayostahili, wasiojua sheria wanazozilinda na walio na tamaa ya kupata riziki toka kwa wanyonge wanaowakamata. Mbaya zaidi, yote haya yamekuwa yakifanyika hali ya kwamba hao wakubwa zao - mabosi wa jiji na pengine hata ngazi za juu zaidi wakijua bayana jinsi wanyonge wanavyonyanyaswa!!!!
ReplyDeleteserikali imeshindwa kuwaangalia raia wake ndani ya nchi,hawa vijana wameamua kujitafutia riziki kwa kufanya biashara na bado waadhibiwa labda na bidhaa zao zimeporwa. TUTAFIKA KWELI
ReplyDeletekuna watu wengi wanalalamika na kutetea hi tabia ya wamachinga kutembea na kuuza bidhaa,lakini wanasahau kwamba miongoni mwa hawa wanaojiita wamachinga kuna kundi la vibaka ambao huzunguka na kucheki maeneo ya kupora kwa mwavuli wa umachinga! mimi nimewahi nusura kuibiwa pale kariakoo na haohao unaowaita wanajitafutia riziki.leo hii unawatete wajazane hapo bongo lakini siku wakitafuta riziki mfukoni kwako unakuwa wa kwanza kubeba tofali na tairi. ni bora wapewe kibano na wengi wana nafasi nzuri tu ya kujiendeleza wakirudi makwao kwakuwa ni vijana na nguvu bado wanayo.lakini wakianza ujinga wa kuzagaa mitaani mwisho wanakosa cha kuuza wanaanza kupora na kuuza kwa bei za chini,na si hivyo tu pia wengine ndo wasambazaji bangi na madwa hayo mnayo yalaumu kuwa yanaingizwa na mapapa wakubwa. hivyo basi kama mtu anaingia mjini ni bora anachokifanya kiwe kinaeleweka na sio kujibananisha kisha kufanya uhuni kwa style ya umachinga.wengi ndio wanauza vitu vilivyoibiwa ktk maduka makubwa unadhani unaweza kuwatofautisha kirahisi yupi bora na yupi si mkweli?matokeo yake ni kujenga wezi wazoefu ambao sasa wana advance na kufanya makubwa zaidi.
ReplyDeletesitetei ujinga huu kabisa,kama ni ridhiki kalime mchicha,matikiti maji n.k kisha vije kuuzwa mjini watu wapate mchicha bora na sio unalimwa ktk bonde la msimbazi ka kusababisha saratani baadaye.
Nyie mnaolalamika ni wale wale mnaowapigia makofi CCM kila siku hapa.
ReplyDeleteTanzania haitaendelea kama watu mtanyamaza tu kila siku. Hamna nchi hata moja iliyopiga hatua mbele bila ya kumwaga damu. Serikali inaendeshwa na mafisadi, hawana muda wala akili ya kuleta maendeleo kwa wananchi, lakini nyinyi mko tu kila siku mnapiga makofi.....Kaeni na Bongo yenu, kweli tambarare!!
NI KUWACHOMA TU HAWA WANYANGANYI.
ReplyDeleteMAFISADI OYEE!!!
HIYO BANGO HAPO NYUMA INATAKIWA ISOMEKE...
ReplyDelete"NOBODY UNDERSTANDS YOUR NEEDS LIKE MAFISADI'S"
TANZANIA HATUWEZI KUNUNUA PINGU,MPAKA WANANCHI WAFUNGWE MASHATI?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????HALAFU TUNAPEPERUSHA BENDERA
ReplyDeleteKATI YA VITU VINAVYOKERA DAR NI WENGI WA MACHINGA. HATAKIWI KABISA HAPA JIJI.
ReplyDeleteUNASEMA WANATAFUTA MAISHA? NANI KASEMA MAISHA YANATAFUTWA KWA KUFANYA BIASHARA BILA MPANGO? KWANI NCHI NYINGI MBONA HAKUNA WAMACHINGA NA MAISHA YANAENDELEA.
WAKAE MAENEO MAALUM WAFANYE BIASHARA SIO KUTEMBEA KILOMETA ZAIDI YA ELFU MITAA KILA SIKU.
HII YOTE NI KUKOSA USATARABU KATIKA MAISHA. PIA NI KUVUNJA SHERIA ZA NCHI.
WAMACHINGA WAPINGWE MAARUFUKU KABISA NCHI ZIMA. HAWASAIDIE CHOCHOTE KATIKA UCHUMI KWANI HIVYO VITU WANAVYOUZA WATU WANAWEZA KWENDA KUNUNUA MADUKANI.
MLALAMIKAJI AU MTOA MADA KUHUSU MACHINGA HAJUI MADHARA YA MACHINGA. NCHI HAIJENGWI NA MACHINGA, HATA KAMA UTAWAACHA MITAANI HUWA HAWABADILIKI MBALI NA KUONGEZA MSONGAMANO KWENYE MITAA HIYO NA HATIMAYE KUWAPA NAFASI VIBAKA KUFANYA MAMBO YAO. AKUMBUKE PIA MACHINGA NI CHANZO CHA KUKWEPA KODI KWA KUWA HAWAKO KWENYE MFUMO WA UCHUMI UNAOSOMEKA. JE, HAJAONA SASA VILE VIBANDA VILIPOBOMOLEWA JIJI NA NCHINI IMEKUWA SAFI NA YENYE BIASHARA ZINAZOELEWEKA BADALA YA MACHINGA AMBAO BEI ZAO HAZIELEWEKI, INATEGEMEA MTEGA UNA BEI GANI? UKIWAONDOA MACHINGA NI RAHISI PIA KUDILI NA BIDHAA FEKI KWA KUWA MWENYE DUKA ANAPOKAMATWA NAZO HATAKUBALI TENA KULETA BIDHAA HIZO AMBAZO ZITAMSABABISHIA HASARA YA KUHARIBIWA. KUWAONDOA HAO HAKUNA NJIA NYINGINE ILA NI NGUVU!!!! KWA KWA TAARIFA YA MTOA MADA, SI TANZANIA PEKE YAKE, NI PAMOJA NA NCHINI NYINGINE ZOTE ZINAZOTUZUNGUKA NA HATA NCHI ZA ULAYA NA MASHARIKI YA MBALI WANAWAPIGA VITA. TENA WAO NI KWA NGUVU KUBWA ZAIDI NA HATA KUWAFUNGA!!!! TUSIPINGE KWA KUSIMAMA UPANDE WA PILI WA KILA JAMBO LILILOPO, BALI TUFIKIRIE NAMNA BORA ZAIDI YA KUFIKIA TUNAPOPATAKA. TUNAWEZA.
ReplyDelete