Assalam aleykum Brother Michuzi,
Brother, naomba uniwekee hii katika globu yetu.
Naomba kuwauliza wadau kama kuna anayefahamu taratibu za upimaji DNA na wapi zinafanyika kwa Dar-es-Salaam na Zanzibar? Bei yake je?
Asante sana,
Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Ushalizwa nini?

    ReplyDelete
  2. Inategemea ni type gani ya DNA unaihitaji. Inabidi utoe maelezo zaidi; kwa sababu zipo sehemu zinazochukua DNA.

    ReplyDelete
  3. Mambo ya kusingiziwa hayo.

    ReplyDelete
  4. bei sio kubwa usihofu, ila ulizia na ni vizuri kupima kwani wanawake wengine wazuri kuongea mdomoni lakini waongo wakubwa unaweza kukuta mwana si wako.

    ReplyDelete
  5. Hahaah.....nenda ofisi ya mkemia mkuu karibu na Ocean Road Hospital....lakini si umlee tu huyo mtoto?!

    ReplyDelete
  6. Ulishalizwa yakhee....wewe kuwa mpole tu na ulee mtoto, watoto wote ni sawa - ndiyo ukubwa huo.

    ReplyDelete
  7. wachuke watoto kimya kimya usimwambia mkeo unaenda kuwapima DNA, ukimaliza ukapata jibu sio sahihi usikurupuke siku ya pili mwambie mkeo oh! my sweet twende tukawapime watoto uone reaction yake. atakwambia ah! unajua kabla ya ... ikawa...unajua dah!..sasa...mwaj aliniunganishia nana..alinipa ushauri.

    ReplyDelete
  8. mtoto ana fanana na jirani nini?

    ReplyDelete
  9. kama amekubambikiza mimba na amezaa mpime na ikigudulika sio wako kula kona usiangalie nyuma.

    ReplyDelete
  10. haya ni matatizo ya kujificha kwenye mashimo bila kuvaa soski.

    ReplyDelete
  11. usichelewe mwanakwetu usiogope ulizia tu kupima DNA sio gharama kubwa, hakikisha kabla ya kukubali ndoa ya mkeka DNA muhimu.

    ReplyDelete
  12. kama demu ni kicheche utamkamatia kwenye DNA haingopi haikosei bandugu.

    ReplyDelete
  13. JE UNAJUA KAMA UNA WATOTO WATATU UNAWEZA KUKUTA MMOJA SI WAKO CHUNGUZA PIMA DNA WOTE.

    ReplyDelete
  14. TRUE STORY MMOJA,YA DEMU MMOJA, MWENYE WATOTO WATATU, ALIHUDHULIA TRAINING YA MASOMO YA NDOA NA UAMINIFU, DAKTARI ALITOA LECTURE YA NGUVU MPAKA YULE DEMU AKALIA, KWENYE ILE TRAINING, DAKTALI AKAMWITA PEMBENI AKAMWOJI SANA MASWALI, NDIPO AKAMJIBU UNAJUA DAKTARI HUYU MTOTO WA KATIKATI SIJAZAA NA MME WANGU NA AKIGUNDUA LEO SIJUI NITAFANYAJE...AKAENDELEA KUSEMA AMEZAA NA MPANGAJI WA JIRANI YAO, SASA DAKTALI AKAMWAMBIA SASA NIFANYAJE.... MIMI KAZI YANGU ILIKUWA NI KUFUNDISHA UKWELI WA MAMBO NA DNA HAINGOPI NIKIMDANYA MME LEO KESHO AKAGUNDUA AKENDA KUPIMA KWINGINE SI MIMI NITAONEKANA DAKTALI FEKI, SASA NJIA YA KUKUSAIDIA NITAMWAMBIA MME MKAPIME KWINGINE.

    ReplyDelete
  15. Hiki kipimo hakiko huru kama unavyojisikia kwenda kupima malaria. Taratibu ni kuwa unatakiwa uwe na barua ya mahakama au mwanasheria wa serikali inayokupatia ruhusa ya kufanya hicho kipimo.Barua yenyewe inakuwa na masharti ambayo wewe (na ikibidi na mwenzako) unatakiwa kuyakubali hasa pale matokeo yanapokuwa tofauti na ulivyokuwa unafikiria.

    Sehemu za kupima nafahamu kwa mkemia mkuu wa serikali pale karibu na ocean road hospital Dar

    Bei nafikiri kama kilo moja (laki) hivi lakini sina uhakika

    Ushauri: Kama unahisi umelizwa, kupima hakutatatua tatizo lako hata kama ikidhibitika kuwa ni kweli umelizwa. Sana sana utajiongezea wasiwasi na mashaka katika maisha yako na hivyo kupunguza umri wako wa kuishi. Hivyo bora usiende kupima

    ReplyDelete
  16. Achana na DNA mkuu Kitanda hakizai haramu atii yakhe. Ukianza kupima DNA za watoto wako mwishowe utaanza kupima na ya kwako na una machi na ya Babako, huta ishia hapo utapima uone kama kweli mamako ni mamako kweli manake utaanza kufikiria labda uli adoptiwa halafu wazee labda hawakutaka kukambia!

    ReplyDelete
  17. kwa dar ni ofisi za mkemia mkuu wa serikali zipo ocean road hospital,gharama 200,ooo

    ReplyDelete
  18. Hivi Nyie watu mnaelewa kiswahili kweli au??? huyu mdau alichouliza ni JE KUNA ANAEFAHAMU TARATIBU ZA UPIMAJI DNA NA WAPI ZINAFANYIKA KWA DAR ES SALAAM NA ZANZIBAR? NA BEI YAKE.
    Sasa cha ajabu baada ya kumjibu mnamwambia alee mtoto sijui mtoto kasingiziwa, wapi ALIPOANDIKA KAMA ANATAKA KUMPIMA/KUWAPIMA WATOTO WAKE???? hivi sisi tutaendelea kweli? maana baada ya kumjibu mnampa maelezo yasioyo ya maana na wala hayatomsaidia kupata jibu la swali lake, WELL mi binafsi niliskia DNA inafanyika Ocean Road Hospital ila sina uhakika, jaribu kuulizia

    Mdau Amsterdam

    ReplyDelete
  19. WABONGO NI WASHAMBA NA WASHENZI KUPITA KIASI, HAWANA MENDELEO HATA KIDOGO, GET TO THE POINT, ANSWER THE QUESTION KAMA LILIVYOULIZWA, JAMAA AMETAKA KUSAIDIWA DNA INAPIMWA WAPI? NA INAGARIMU KIASI GANI? FULL STOP.
    SASA INAKUWAJE MUNAANDIKA MANENO KIBAO NAAMINI SIO PEKE YANGU WADAU WENGINE HAPA PIA WAMEWASHANGAA. MHHHHMH! KUENI NA USTAARABU JAMANI. MSICHAFUE MTANDAO WA MICHUZI HAPA, INAONEKANA BAADHI YENU HAMNA KAZI YA MAANA MNASHINDA TU KWENYE COMPUTER NA HAMNA LA MAANA ILA MNAISHIA KUANDIKA UPUUZI.

    ReplyDelete
  20. Babu wataka kupima vina saba?
    kaazi kweli kweli hapo.

    ReplyDelete
  21. Asante sana mdau Anony wa 07:15:00 Am. Nashukuru kwa msaada wako. BaarakAllahu feek,
    Mdau aliyeuliza swali.

    ReplyDelete
  22. Duu!! sijui huu ndo uswahili wenyewe au ni kitu gani... Majibu yanayotolewa ni tofauti kabisa na swali, watu wanajibu kwa jinsi akili zao zinavyofikiria sio muulizaji alichotaka. Pole swahba hao ndo waswahili... teh teh teh, mimi ningekushauri uende kuulizia hilo kwenye hospitali yoyote iliyo karibu nawe.
    - Yosi

    ReplyDelete
  23. WE KUBALI TU KULEA MTOTO HUYO....WATU KIBAO WANAJUA KAMA WANABAMBIKIWA WATOTO...WEWE SI WA KWANZA.200,000 YA DNA SI MJAZE MSOSI NDANI.MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  24. Wadau wawili (12.01 na 02.37)wanawalaumu wachangiaji kwa kutoka nje ya mada. Mimi nafikiri kutokana na unyeti wa hiki kipimo na kwa kuzingatia haki za kibinadamu katika kutoa maoni yake, sioni kama hao watu wengine wanastahili kulaumiwa kwa maswali au maoni yao waliyotoa ambayo hayajibu swali moja kwa moja bali wanaonyesha mtizamo wao kuhusu kipimo husika na mazingira yanayolazimu mtu kufanya hiki kipimo. Hii ni forum ambayo kila mtu anaruhusiwa kujiachia anavyotaka ili mradi isitumike lugha isiyostahili. Jibu langu la msingi liko 07.15

    ReplyDelete
  25. Kwani DNA mara nyingi inatumika kwa ajili ya nini?
    1)kutambnua kama mtoto ni wako
    2)kutambua muuaji au mbakaji
    3)kutambua mabaka ya mtu aliefarika na hatambuliki
    4)nakazalika

    Kwa ivo muuliza swala ni lazima atakuwa na maswaibu yamemkuta na kwa vile hajasema ni maswaibu gani hayo yanayomfanya atafanye DNA, basi watu wangi wanazani ni kwamba ana wasi na mtoto wake!

    ReplyDelete
  26. HI
    DNA test kwa Tanzania inafanyika kwa mkemia mkuu , ofisi ziko ocean road.
    sampuli moja ilikuwa ni sh. 250, 000/=, unahitaji uwe na barua kutoka mahakamani au advocate au Doctor mkuu ikieleza sababu ya kupima DNA.
    kama unataka kujua mtoto ni wako au ulipotelewa na ndugu au maiti haijulikani, sampuli ya baba, mama na mtoto au hiyo maiti zitachukuliwa na kupimwa. kwa maelezo zaidi wasiliana na ofisi ya mkemia mkuu. kila la kheri

    ReplyDelete
  27. HOSPITAL WANAWEZA KUFANYA HIVYO KWA TANZANIA HADI SASA, HATA HUKU ULAYA KULE POLISI WANAOCHUKUWA SWAB NI MADAKATARI PIA KWA KIPOLISI USIWAONE WAMEVAA KIPOLISI WAMESOMA UDAKITARI PIA SO NENDA HOSPITALI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...