KAKA MICHUZI,
NAOMBA MSAADA KWENYE MATUTA HAYA MAWILI. MIE NATAFUTA
1. CIVIL ENGINEER (DEGREE HOLDER) NA UJUZI WA MIAKA 5 KUFANYA KAZI OMAN , MSHAHARA NA BONUS NI MZURI.
2. WOMAN TEACHER IN ENGLISH AND MATHEMATICS KUWAFUNDISHA WATOTO WANGU DARASA LA 7 NA 8 HAPA ABU DHABI.
KILA KITU JUU YANGUYAANI ATAISHI KAMA FAMILIA NA LEAVE MWEZI NA NUSU KWA MWAKA MSHAHRA MZURI PIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. why woman teacher?...lol

    ReplyDelete
  2. MBONA HAUJITAMBULISHI KAMA WEWE NI MWANAUME AU MWANAMKE? BADALA YAKE UNATUWEKEA MWAKA ULIOZALIWA! KUWA MUWAZI UNAPOTANGAZI KITU AMBACHO HAKINA USIRI NDANI YAKE, MIMI NINAKUTILIA MASHAKA.

    ReplyDelete
  3. Washkaji kama mtakua interested na hizi kazi muwe makini, vijana wengi wa kibongo wapo huku Oman wanateseka, wanaishia kuwa mahouseboy na mahousega, na dada zetu wengi wamekua machangudoa wa kisirisiri kwa kuuzwa kwa waarabu. ukija huku kwa kazi kama hii hakikisha jamaa anakutumia mkataba kabisa na mkubaliane vitu vya msingi. Kwa ufupi vitu muhimu kufahamu kuhusu oman ni kuwa:
    1. Kupanga nyumba ni ghali ukilinganisha na bongo, room nzuri kuanzia rial 100 kama tshs. 350,000 kwa mwezi yenye choo na bafu. hapa naona anasema utaishi kwake kama familia, hii sasa si kazi ya ualimu bali ni u housegirl. ni muhimu akulipie nyumba.
    2. Mishahara ya huku kwa mtu mwenye degree haiwi chini ya rial 1000 kima cha chini kwa watu wa Africa, ila wengi ni rial 1500 hadi 2000 kutegemea na uzoefu.
    3. Usalama Oman ni wa juu sana, hivo hakuna hofu ya kuibiwa kitu wala nini, mi naishi kwenye nyumba ambayo hata mlango sijawahi funga na kila kitu nakikuta salama.
    4. Hali ya hewa haitabiliki, kuna miezi ya joto sana, hadi 50 degrees centigrade na pia kuna miezi ya baridi kali.
    5. Watanzania (or rather East Africans)tuna heshima zaidi huku kuliko watu wa Asia ya kati, India, bangladesh na pakistan, hivo hata mishahara ya hawa jamaa pia ipo chini.

    kama kuna mtu ambae atazitaka hizo kazi na angependa kujua zaidi kuhusu maisha ya huku, wasiliana nami kupitia blog hii.

    ReplyDelete
  4. wewe unamtaka civil Engineer!!una kampuni?ebu taja jina la hiyo kampuni na tuone kama ni hai,Mjomba nanihii usikubali watu ovyo ovyo tu watoe matangazo yao kwenye blog hii ya jamiii.

    ReplyDelete
  5. kwa nini hutaki mwalimu wa kiume????

    ReplyDelete
  6. PETER NALITOLELAOctober 08, 2009

    IAM MOST QUALIFIED...........!
    MIMI NINAITWA PETER NALITOLELA NIMEMALIZA MUZUMBE KULE MLOGOLO NIMESOMA ECONOMICS NA FORM SIX NILIKUWA MUKALI WA KINGELEZA NA HISABATI, PIA NIMEJIFUZA UINJINIA WA KUTENGENEZA FRIDGE SIJUWI KAMA UTAFITI KWENYE CIVIL ENGINEER LAKINI ANY HOW I AM QUALIFIED FRIDGE ENGINEER. YOU CAN OFFER ME A JOB I PROMISE MY GOD I CAN NOT LET YOU DOWN, I LOVE YOUR CHILDREN AND I WILL DO EVERY THING TO KEEP THEM HAPPY. SIR/ MADAM HELP ME TO TAKE CARE OF YOUR CHILDREN AND I PROMISE TO DO SOME ENGINEER JOBS OR EVEN TAUGHT THEM ENGLISH AND MATHEMATICS. I USED TO LIVE AND WORK AND STUDY ABROAD CANADA THUS I SPEAK AND WRITING FLUENT ENGLISH FROM BOTTOM OF MY HEART HELP ME GOD. I AM DOWN TO YOUR KNEES SIR HELP ME.

    ReplyDelete
  7. Yawezekana anataka mwalimu wa kufundisha binti zake. Wadau mbona hamna imani?

    ReplyDelete
  8. Daktari wa familia unataka? Na awe wa jinsi gani?

    ReplyDelete
  9. jamaa anatafuta beki3(housegirl)mwenye degree !!kudadeki wallah kweli jamaa kapania

    ReplyDelete
  10. tatizo lenu mnataka teacher wa kike halafu mumgeuze mke na jamaa zenu pia waponee hapo hapo, hii noma, kwanini hutaki teacher wa kiume? au hao watoto wako ni wa kike? sasa ndo unajihami mapema? ukiona mtu anajihami ana watoto wake mapema ujue nayeye ni mbaya sana kwa vya wenzake.

    ReplyDelete
  11. Kichwa KigumuOctober 09, 2009

    Jamaa, ameandika vitu vya maana sana katika mtandao ili kusaidia watu, nyinyi mnachangia uoza.
    Jamaa anaonekana ni MTZ, ambaye aidha ana kampunia au ana network ya kujua kampuni. Na ameamua kuwasaidia waTZ wenzake wenye elimu hiyo ili waje kufanya kazi OMAN.
    Huyu jamaa hakushiwndwa kuwaajiri wahindi au wapakistan waliojazana OMAN, tena wenye elimu hiyo, ameamua kuwasaidia WATZ wenzake nao wabahatike kuendelea. Na kutumia mtandao ni jamabo alilofanya ki-maana. Kama wewe unahiyo degree na uzoefu basi muandikie mail na mtajibiana hadi kukamilisha mahitaji yako.
    Hii process ni kubwa sana, kwa kuwa atawapatia hao watu kibali na visa ya kufanya kazi OMAN, ambayo sio rahisi kuipata hivi hivi.
    WATZ mara nyingine tushukuru tunapoombwa kwani ni mlango amefungua na anayetaka mwenye shida aingie.
    Haya ya kusema mara kwa nini mwanamke, hayana maana. Huji nchi za watu nje ni rahisi sana kumfunga mtu, kama akikutaka kimapenzi. Kwani ni kupig tu simu na polisi wanakuja kufanya uchunguzi wa awali huku jamaa akiw ndani. Nchi za watu bwana, kulala na mwanamke ni lazima akubali yeye, kumbaka, au kumpa pombe na kulala naye ni kujitakia matatizo baadaye, ya kuwekwa jela miaka 2.
    Hii sio TZ ambapo msichana akiingia tu kwako, then umebaka.
    Ni kweli mwalimu lazima asaidie n akazi nyingine, maana neno multitasking ndo linkuja hapo.
    Tumezoea neno mwalimu ni kufundisha tu, nchi zingine, asubuhi ni mwalimu na usiku ni mfagiaji katika mabenki, au muendesha magari ya kuuza maua jioni. Ilimradi fedh inaingia kibindoni.
    WATZ , mnaotaka changamkia tenda.

    ReplyDelete
  12. Hizi ni sound tu. Kazi za civil huwa haitangazwi kienyeji namna hiyo.Kama ni kweli basi aweke information na specification zote zinazohitajika.
    1 Aweke jina la kampuni na shughuli zote ambazo kampnu inafanya.

    2 Hii itarahisha hata kwa muombaji kwani atakuwa anajua anachokifanya.

    3 Vipi kuhusu mkataba, maana kumtoa Engineer bongo na kumpeleka Oman sio swala rahisi kama anavyofikiria, kuna mambo mengi ya kufanyika hapo kati na gharama zake ni kubwa.

    4 Engineer anatakiwa aandaliwe makazi yake na familia yake, je ataweza ?

    Nafikiri ni rahisi akachukua engineer huko Oman, kwani hakuna engineer atakayekuja kufanya kupitia jina lako (kienyeji), engineer atakuja kwa kupitia kampuni ili kuhakikisha ana security ya kutosha.

    Pia kuhusu mwalimu, nafikiri ni suala lisilo na msingi, kwani Oman mashule (intrenational ni mengi na yana walimu bora, hivyo peleka watoto international kama kweli una hela.

    Nadhani huyu jamaa anatafuta house girl tu , baadae ni ngono isiyo salama kisha anakufukuza at the end.
    Huyu ni tapeli tu hana uwezo wowote wa kuajili mtu, yeye naye ni choka tu huko Oman

    ReplyDelete
  13. Tafadhali tizama video hii:
    http://www.mzalendo.net/videogulf-labour-laws-fail-to-halt-abuse

    Kabla hujaamua kuenda kujiunga na familia hapo arabuni.

    Mdau Zenji

    ReplyDelete
  14. MBONA EMAIL YENYEWE INAKATAA UKIMTUMIA NI FAKE NINI? EBU ATULETEE EMAIL SASHIHI, EBO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...