
Katika juhudi zao za kukarabati mfereji wao wa Umwagiliaji, wanakijiji wa Masaera, Kata ya Kilema Kusini, kwa ushauri wa Wahandisi Wasio na Mipaka wa Marekani,[EWB-USA] waliomba na wamesaidiwa utaalamu wa ulipuaji na Mheshimiwa Padri Ladislaus Segewart wa Seminari ya Maua Kilema.
Padri Segewart ni Mswiss wa Shirika la Makupuchini na alikuja Tanzania mwaka 1954. Hivi sasa Padri Ladi ana miaka 86 na inaaminika ndiye mtu mzee kuliko wote duniani mwenye leseni hai ya ulipuaji kwa baruti .
Leseni yake ni hai hadi 2014 na anapendelea kulipua mawe kwa Magnumbuster na huiwasha kwa dynamo aina ya Beethoven! Kwa Taarifa zaidi wasiliana nami kwa simu au mtandao!
-------------------
In their effort to rehabilitate their irrigation canal te villagers of Masaera in Kilema Kusini ward , at the advice of Engineers without Borders USA, [EWB-USA] sought and were assisted in blasting by Reverend Father Ladislaus Segewart from Maua Seminary, in Kilema, Kilimanjaro region in Tanzania.
Father Ladislaus Segewart [pictured] is a Swiss of the Capuchin order who came to Tanzania in 1954. Father Ladi is 86 years old and it is believed that he is the oldest person alive with a valid blasting licence.
His licence is valid until 2014 and he prefers to blast rocks with Magnumbuster setting off the ignition using a Beethoven dynamo!
For more contact me via phone or email
Canute Temu,
Coordinator,
Masaera Traditional Irrigation Canal Rehabilitation Program.
Freelance journalist based in Rural Kilimanjaro.
Canute Temu,
Development Consultant, Translator, Editor, Documentalist;
Residence: Vanilla Farm ,
Masaera Village,
P O Box 270
HIMO,
KILIMANJARO,
Tanzania.
Phone: +255787258877 and +255754282101
Do good and do it well. Fanya mema na yafanye vizuri.
Ahhhhhhhhh kumbe ni hivyo... Nilifikiri huwa anawasaidia wabeba box huku ughaibuni kujilipua.. Nilitaka kumtafuta maana na mimi na-plan kujilipua.
ReplyDeletekeshajilipua bongo, sasa amekamata makaratasi ya kibongo, shauri lenu mnaojilipua huko ughaibuni.
ReplyDeleteHuyu Padre amenifundisha Maua 1990 na tayari alikuwa mzee. He is such a good man japo ni mkali sana -strict. Proud to see that he is still good at his work
ReplyDeletea great thank to Michuzi, yaani hata kijijini kwetu kuule mbali u can make a follow up of what is going on!!!! big Up
ReplyDeleteMzee ni mchapakazi saaana. Nimekuwa nae kwa miaka 4, nafurahi badi yupo na ana nguvu maana ni zaidi ya miaka 14 sijamwona.
ReplyDeleteAsante mdau
woh! jamani huyo padri kanikumbusha mbali kweli, mwaka 1996 nilimuona Maua Seminari kule Marangu Kilema, mkoani Kilimanjaro nakumbuka alikuwa mwalimu na wanafunzi walisema ni mkali hapendi ujinga au mchezo kwenye masomo. Dah ama kweli mithupu we si mchezo. Abel, Felix, Sule, na wadau wengine wa maua Seminari mnamkumbuka father ladi???????
ReplyDeleteAma kweli mavi ya kale hayanuki.
Wadau wa seminari ya Maua, mnamkumbuka Father Ladislaus aka Mbundu? JIna la Mbundu ndio lilikuwa zoeleka zaidi kwa wanafunzi...
ReplyDeleteHuyu padiri ni mchapakazi hodari aisee kwenye swala zima la kufanya kazi hana utani...
Mungu akubariki father ladislaus umeweka mifano mingi kwa vijana wengi tuliopita katika mikono yako pale Maua seminary.
Be blessed.
DD
Duh Baba Lad ni mzima nakumbuka stori zake alipokuwa anafundisha Kasita Seminary, mzee huyu alikuwa ana shamba la miwa lakini wezi wakubwa ktk shamba lake walikuwa wanafunzi wake. Kwa kukomesha alikuwa anajificha shambani lakini wanafunzi wakagundua ujanja wakawa wanamuita kabla ya kuingia shambani akiita wanasema kuna mtu anataka kwenda ktk kitubio. Ila ni mchapa kazi sana mzee huyu...Mdau Wa KASITA
ReplyDeletePD. LADI AKA MBUNDU, sijawahiona binadamu anachapa kazi km huyu mzee. Naamini asilimia 2 tu ya watanzania tungekua na bidii yake tungekua tumeshasahau umasikini. Mungu akubariki sana Pd. Ladi aka. Mbundu aka Mashkapu.
ReplyDeleteKijijini Ruwa/Maua walimuita Mashkapu kutokana na uwezo wake wa kubeba mizigo mizito na kutembea mbali wakati mwingine hadi km zaidi ya 10 na umri wake mkubwa.