Mbunge wa Rorya, Prof Philemon Sarungi akimpongeza Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar kufuatia nishani ya Umoja wa Mataifa ya Ushujaa wa Kutetea Haki za Kijamii (World Hero of Social Justice) aliyoipokea kwa niaba ya Baba Taifa na kukabidhiwa na Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa nchini Marekani hivi karibuni. Mama Maria Nyerere ni mzaliwa wa Jimbo la Rorya. Kushoto ni mai waifu wake Prof Sarungi, Veronika.
Mbunge wa Rorya, Prof Philemon Sarungi (kulia) mai waifu wake Veronika wakipiga picha na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, walipokwenda kumpongeza nyumbani kwake Msasani jijini Dar kwa kupata nishani ya Umoja wa Mataifa ya Ushujaa wa Kutetea Haki za Kijamii (World Hero of Social Justice) aliyoipokea kwa niaba ya Baba Taifa na kukabidhiwa na Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa nchini Marekani hivi karibuni. Mama Maria Nyerere ni mzaliwa wa Jimbo la Rorya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Kaka Nanihii tunaomba kwa Ihsani yako ututolee coverage ya Sheikhe Sharifu ambaye inadaiwa na baadhi ya globu kuwa ameritadi(ameokoka) amekanusha habari hiyo habari hii inachanganya watu sana .Tafadhali tunaomba ututolee hapa kwa ihsani yako Muheshimiwa.Tunaomba namba yako ili tukufuate uweke usahihi wake humu globuni(Tunaiamini blogu yako kaka)
    Asante
    Ustaz Mwinula

    ReplyDelete
  2. hii ni kumwongezea jina nyerere, wamesahau huyu jamaa aliuwa demokrasia tanzania, nyerere alikuwa mfalme asiyekuwa na katiba, ingekuwa bora awe mtemi wa wazanaki sio tanzania nzima, bado tunahangaika na sera zake!!!!

    ReplyDelete
  3. wewe anony hapo juu,alicho kifanya nyerere hutakaa ukielewe undani wake hadi hapo utakapo kuwa na uondokane na mtizamo wako wa kiganjani ndipo utaelewa!
    kwa taarifa yako hadi sasa zaidi ya 85% ya watanzania hawajui nin wanahitaji,si ktk ngazi ya familia tu bali hata ktk ngazi ya taifa.je unategemea wakati nyerere anaingia madarakani hali ilikuwaje?huwezi kujenga msingi wa nyumba juu ya majani au kujenga nyumba unayo tarajia ktk msingi usiofahamu aliye ujenga alikuwa na malengo ya kujenga nyumba ya quality gani.
    wengi wanaropoka sana lakini hata ukiwapa leo hii kundi la raia milioni moja tu ili waliongoze kwa miaka 10 tuone mabadiliko ya maisha yao hawataweza kufanya hilo na huu ni mwaka 2009,je 1961 ni aje?si ku challenge sana ila kwa mtu mwenye busara hakwepi kuutizama ukweli,na mara nyingi majibu unayoweza kudhani ni magumu sana yanaweza kuwa ni mepesi kuliko udhaniavyo ikiwa tu utalitazama swali hilo tokea pande tofauti!kumbuka ukiwa nje ya uwanja mchezo ni rahisi sana,ila ukiwa unaufukuza mpira au riadha,mtu aliye kutangulia kwa sentimeta 10 unaweza kumaliza energy yako yote kutaka umpite na usiweze tangu mwanzo hadi mwisho!walatin wanasema unicuique sunt vitia suarum virtutum!!kila mmoja anasaliti mapungufu yake mwenyewe. kwa mfano wewe ukiwa mzalendo umefanya nini kwa nchi yako?basi najua utaanza kulaume wengine kuwa ndio chanzo,lakini je wewe umefanya nini basi hata pale mtaani unakoishi?
    mdau*****

    ReplyDelete
  4. Ama kweli watanzania hamna shukrani, Huyu mzee wa watu (JKN RIP)alipokua anaingia madarakani alikuta nchi haina wasomi, engineers walikuwa 8 na madaktali 2 nchi nzima, Hawa naongelea wazaleondo. Nchi haikuwa na viwanda miundo mbinu ndo hakuna kabisa, alisomesha wananchi wake bure toka elimu ya msingi mpaka chuo kikuu. Leo mnamuona mchinga, Haya niambieni haya MAFISADI yenu yamefanya nini ? na yote yalisomeshwa bure kipindi cha mwalimu

    ReplyDelete
  5. it does not matter, elimu ya bure? tulikuwa tunakwenda kulima shamba la shule kila siku, tunalimishwa siku nzima juani bila hata kunywa maji. umesahau kukariri nguzo za tanu, imani za tanu. kwa taarifa yako jumba la ccm dodoma ilikuwa kila biashara hata wauza maharage sokoni walitoa shilingi mia tano ili kulipia ujenzi wake,sisi watoto wa shule za msingi tulipelekwa kuchimba mitaro ya msingi wake. alipofisadi uchaguzi wa mwaka 1980, i never look back, left bongo for good, now i just come to visit kila mwaka, nashangaa hawa jamaa wataamka lini?

    ReplyDelete
  6. michuzi kweli natoka nje ya majaa ya picha hii lakin hata na mimi pia nataka kujua kama ni kweli huyu sheikh shariff karitad please kama una habari hii tueleze please.

    na na muunga mkono sana aliyetoa madaa at 5:41 pm umesema kweli tupu na umepiga msumari wa moto kwenye fullstop yako.

    kweli kama mzalendo umefanya nini wewe ndugu yangu mtanzania uliye nje au ndani ya nchi basi hata mtaani kwenu umeshindwa kuleta maendeleo ya jamii yako?
    nakupa big up na heko mdau wewe wa 5:41

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...