Na Sunday Simba Shomari wa VOA
Prof.Mshomba anafundisha uchumi katika chuo kikuu cha La Salle huko Philadelphia na hivi karibuni alipata tuzo ya hali ya juu ya mkufunzi bora wa mwaka 2009 ijulikanayo kama "Lasallian Educator" ambayo hutolewa kwa wafanyakazi bora wa La Salle ambao huonyesha uaminifu wao kwa mambo yenye umuhimu kwa La Salle na utamaduni wa La Salle katika maisha ya kila siku.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwake na Rais wa chuo hicho Br.Michael J.Mcginnis FSC,Ph.D na mshomba alitoa shukrani zake za dhati kabisa kwa chuo hicho kumpa elimu, nafasi ya ajira na sasa tuzo na kuuliza nini zaidi mtakachonipa?
Mshomba ni mzaliwa wa Arusha Tanzania na alikulia na kupata elimu ya msingi katika kijiji cha Sinoni mkoani humo. Mshomba alirudi kufundisha chuoni hapo mwaka 1991 katika idara ya Uchumi, kwa karibu miaka 20 sasa amefanya kazi chuoni hapo na amekuwa sehemu ya familia ya chuo hicho.
Mshomba pia anachangia makala katika gazeti la Arusha Times. Mshomba amejaaliwa mke na watoto watatu na huwa wanasafiri kila mwaka kwenda kijijini kwake Arusha Tanzania ambapo wanafanya shughuli mbali mbali za maendeleo kijijini humo.
Prof.Richard Mshomba si jina geni miongoni mwa wasikilizaji wa Sauti ya Amerika kwani ni mmoja wa wachambuzi wanaochangia mada mbali mbali za uchumi, biashara na siasa katika idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Washington Dc.
Prof.Mshomba anafundisha uchumi katika chuo kikuu cha La Salle huko Philadelphia na hivi karibuni alipata tuzo ya hali ya juu ya mkufunzi bora wa mwaka 2009 ijulikanayo kama "Lasallian Educator" ambayo hutolewa kwa wafanyakazi bora wa La Salle ambao huonyesha uaminifu wao kwa mambo yenye umuhimu kwa La Salle na utamaduni wa La Salle katika maisha ya kila siku.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwake na Rais wa chuo hicho Br.Michael J.Mcginnis FSC,Ph.D na mshomba alitoa shukrani zake za dhati kabisa kwa chuo hicho kumpa elimu, nafasi ya ajira na sasa tuzo na kuuliza nini zaidi mtakachonipa?
Prof. alijiunga na chuo hicho akiwa kijana mdogo tu wa umri wa miaka 27 kwa kupata full scholarship kutoka chuoni hapo na alimaliza masomo yake kwa matokeo ya hali ya juu mno ya mtihani "Maxima Cum Laude" na Major mbili ya Uchumi na Falsafa. Baadaye alikwenda kuchukua Masters katika Chuo Kikuu cha Delaware na baadaye PhD katika Chuo Kikuu cha Illinois.
Mshomba ni mzaliwa wa Arusha Tanzania na alikulia na kupata elimu ya msingi katika kijiji cha Sinoni mkoani humo. Mshomba alirudi kufundisha chuoni hapo mwaka 1991 katika idara ya Uchumi, kwa karibu miaka 20 sasa amefanya kazi chuoni hapo na amekuwa sehemu ya familia ya chuo hicho.
Mwaka 2000 Prof.Mshomba alitoa kitabu kiitwacho "Africa in the Global Economy" (Lynne Rienner publishers), ambacho kilichaguliwa kitabu bora cha wanafunzi. Baada ya hicho alitoa kitabu kingine kiitwacho "Africa and the World Trade Organisation" (Cambridge University Press) kilichapishwa mwanzoni mwa mwaka huu. Ambacho alikitoa kwa heshima ya De La Salle Christian Brothers kwa utoaji wao wa elimu duniani kote.
Mshomba pia anachangia makala katika gazeti la Arusha Times. Mshomba amejaaliwa mke na watoto watatu na huwa wanasafiri kila mwaka kwenda kijijini kwake Arusha Tanzania ambapo wanafanya shughuli mbali mbali za maendeleo kijijini humo.
hongera Prof. Karibu UD japo kwa semester moja uje utupe nasisi darasa kwenye Uchumi.
ReplyDeleteWewe Sunday Shomari kwenye hii paragraph Umekosea. Hebu rekebisha kabla Prof. Hajaona
ReplyDelete"Prof. alijiunga na chuo hicho akiwa kijana mdogo tu wa umri wa miaka 27 kwa kupata full scholarship kutoka chuoni hapo na alimaliza masomo yake kwa matokeo ya hali ya juu mno ya mtihani "Maxima Cum Laude" na Major mbili ya Uchumi na Falsafa."
SIO "Maxima Cum Laude" Bali ni "Summa Cum Laude"
Wewe Tarehe Mon Oct 05, 07:50:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteUwe unasoma na kuelewa, sio kukurupuka tu. Nimesema Prof. alipata "Summa Cum Laude" na SIO "Maxima Cum Laude".
Kiswahili wagumu kuelewa, Kiinglishi hakipandi, sasa sijui tuwasaidiaje?
Soma na kuelewa kabla hujajibu swali. Ndio maana watu wengi Bongo huwa wanafeli mitihani kwa sababu hawajaelewa swali tayari wameshaanza kujibu.