nyota wa muziki enzi za mwalimu walikusanyika na kuunda bendi moja ya muda kutunga nyimbo za kuhamasisha umma katika kuchangia maafa mbalimbali. hapo ni hoteli ya mbowe wakati wa tizi. wenye data tunaomba stori pamoja na majina. mie naanda na dj seydou aliyebana nyuma kabisa kulia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Duuhh hapa kazi ipoo,maana mimi hapa nimewamanya wawili tuu.Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu waliofatana upande huu wakulia.

    ReplyDelete
  2. Namuona mzee Mwalimu Gurumo kulia kabisa inaonesha kipindi hiko alikuwa muitikiaji tu. Sasa ndio manager wa msondo ngoma.

    ReplyDelete
  3. Namimi naongezea wa kwanza kulia ni mjomba Muhidin maalim Ngurumo aka kamanda

    ReplyDelete
  4. mwenye shati la kitenge sio Fresh Jumbe enzi za sikinde!

    ReplyDelete
  5. Yaani enzi za Mwalimu bwana!

    Yaani MAIKI zilikuwa za KUSHEA! Si unacheki hapo Gulumo anangoja Marijani amalize na yeye atumie Maiki hiyo hiyo. Halafu hao kulia kwa Marijani pia wanashea maiki.
    Siku hizi maiki za kumwaga tu.

    Khaa! Kweli tumetoka mbali

    ReplyDelete
  6. "usipowajibika ole wakooo!"

    ReplyDelete
  7. Do! Enzi zile jamani !kulikuwa mziki sio mchezo,hapo Muhidin Gurumo alikuwa yupo yupo tu,na sauti yake ya ubabe ubabe,marehem Marijan Rajabu mwana Manyema ndie alikuwa jogoo la mjini.

    ReplyDelete
  8. Namuona Gurumo kulia, anafuatia marijani Jabali, nyuma ya Jabali nadhani ni Max Bushoke, halafu anafuatia Nana Njige mtoto mzuri ambae anaimba pamoja na Zahir ali Zorro (mwenye miwani ya juwa).
    Kulia kwa Zahir ni Fresh Jumbe wakati huo akiwa bado kinda lakini matata sana. Anaemfuatia Jumbe ni Rahma Shally aliyekuwa muimbaji wa mwenge jazi, halafu wa pili toka kushoto ni mwanajeshi wa bendi ya mwenge Jazz PASSELEPA Mabruki. Wa mwisho kushoto simuoni vizuri sijui ni nani huyo. Hizi zilikuwa ni enzi za mzee rukhsa Mwinyi na si enzi za mwalimu. Nakumbuka niliwakuta pale mbowe wakila tizi chini ya Jabali ambe ndie aliekuwa kiongozi wao. Enzi hizo muziki ulikuwepo bwana si mchezo...we acha tu.

    ReplyDelete
  9. Ni mwaka 1986 walipomkabidhi fagio la chuma Ali Hasan Mwinyi

    ReplyDelete
  10. Tena hii bendi pia walikuwepo wahindi wale kina yunus VARDA ARTS. Mbona hapa siwaoni?.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...