ANGALIZO. Hiyo si "tatoo", ni maandishi juu ya picha. Picha kwa hisani ya

www.memphisbluebears.com

Hasheem Thabeet, usiku wa kuamkia leo alifungua pazia la kushiriki mechi ya kwanza ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA pale alipoichezea timu yake ya Memphis Grizzlies dhidi ya Washington Wizards katika mechi ya kwanza kati ya mapambano ya kujipima nguvu kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa 64 wa ligi ya NBA utakaoanza rasmi Oktoba 27 2009 na kumalizika Aprili 14 2010.

Katika mechi hiyo ambayo Wizards walishinda 101-92, Hasheem alionekana kufanya vema kwa kuweza kufunga pointi 6 na kuzuia mitupo 4 ndani ya dakika 15. Huu si mwanzo m'baya kwa Hasheem ambaye alikuwa chaguo la pili kwa thamani katika draft ya NBA na sasa ameanza ngwe nyingine ya UCHEZAJI WA KULIPWA katika mpira wa kikapu.

Kila la kheri Hasheem
"
www.changamotoyetu.blogspot.com"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hasheem Thabeet(notes), the 7-foot-3 inch center out of Connecticut who was taken with the No. 2 overall pick, is raw.

    That was the knock against him leading up to the NBA Draft, and it was pretty clear to anyone who saw the new Grizzlies' center play in summer league action.

    He's long, lean, muscular and raw.

    But a 57-raw? Really, 2K Sports?

    It appears so.

    According to The Daily Thunder (via Tas Melas' Twitter account), Thabeet's "NBA 2K10" video game player rating is a miserable 57 overall.

    To put that rating in perspective, Derrick Brown(notes) got a 69 overall, Sam Young(notes) a 67, Chase Budinger(notes) a 65 and Danny Green(notes) a 64. All four of those rookie forwards were second round picks.

    Then again, as "The Real 2K Insider" points out, Thab got the same rating given to Charlotte Bobcats center DaSagana Diop, which might mean he's the only rookie that wasn't overrated in the game.

    That's what Grizzlies fans are hoping for, anyway.

    *****

    By the way, did anyone out there pick up copies of "NBA Live 10" or "NBA 2K10" yesterday? Should I ditch my classic NES' "Double Dribble" game for either of 'em? Let me know in the comments, gamers. Cheers

    ReplyDelete
  2. NBA sio lele mama...... Tulio USA ndio tunajua...
    ana chance ya kuimprove, lakini inabidi ajifue. Mwaka huu best rookie ni Dejuan Blair, na nilisema the kid have talent. Jana amepiga double double.....

    ReplyDelete
  3. CCM fanya kazi yako rinda uhuru waraia wako......

    ReplyDelete
  4. all the best

    ReplyDelete
  5. waswahili mmemtia nuksi mie naona arudi nyumbani afanyiwe "KAFARA LA NGUVU" halafu arudi kufanya vitu vyake. Na pia ulaya huku mambo ya kutudharau sie watu wa africa ni yako sana so ategemee kuangushwa kila mara ila kama wazungu wanavyosema "let your haters be your motivators"

    good luck bro hash

    ReplyDelete
  6. kwa kweli ni mtanzania mwenzetu,tunafurahi sana, kwani atapeperusha bendera ya nchi yetu, na tunamtakia kila la kheri....ila tuu ajifue....NBA sio lele mama....all the best bro.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...