Tunapenda kuwakumbusha wasomaji na wasikilizaji wetu kuwa habari kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC zinapatikana kupitia wavuti maalum kwa ajili ya simu za mkononi -
http://www.bbcswahili.com/mobile
Huduma hii mpya inawawezesha watumiaji wa simu za mkononi kusoma taarifa za kila siku moja kwa moja katika simu zao badala ya kutumia kompyuta. Hata hivyo ieleweke kuwa baadhi ya simu (handsets) haziwezi kupata huduma hiyo kwa kuwa hazikuundwa maalum kupokea mawasiliano ya tovuti.
BBC haitozi fedha kwa wanaotumia huduma ya wavuti kupitia simu za mkononi, ni bure kwa kila mtu. Lakini unatakiwa kuzingatia kuwa makampuni ya huduma ya simu za mikononi au PDA kwa kawaida hutoza gharama kutumia huduma ya internet. Lakini hutofautiana kutoka kampuni moja hadi nyingine. Kuna uwezekano ukatozwa na kampuni yako ya simu gharama ambazo hujulikana kama “data charges”.
Endapo huna uhakika wa uwezekano wa kutozwa fedha kwa kutumia tovuti kwenye simu yako, tafadhali wasiliana na kampuni inayokupa huduma ya simu. Lakini kwa kuwa taarifa ni za maandishi pekee bila picha, sauti au video, gharama yake inaweza kuwa ni ndogo.
Toleo la wavuti ya BBC Swahili mobile linapatikana kupitia simu za mkononi, PDA na vifaa vingine vya mawasiliano ya mkononi. Kutakuwa na taarifa za matukio na vile vile soka. Wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Angola, mwanzoni mwa mwaka ujao, utaweza kupata taarifa za moja kwa moja
Huduma kama hii pia inapatikana kutoka Idhaa nyingine za BBC zinazorusha matangazo Afrika katika lugha kama Kisomali, Kihausa, Kinyarwanda, Kireno na Kifaransa.
http://www.bbcswahili.com/mobile

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Michu, mpigie debe Elizabeth, wadau wampigie kura yuko kwenye kitimoto anaweza toka this week..mpambano ni mkali..mi huku niliko napiga kura kila baada ya one hr..tumsaidie mTZ mwenzetu...

    ReplyDelete
  2. ...tadhali mwenye kuelewa anieleweshe tofauti ya tovuti na wavuti...

    ReplyDelete
  3. hakuna tena kusikiliza redio mambo ni kwenye kiselula tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...