Athumani Juma Ubao a.k.a AJ Ubao a.k.a Father D

Na Sunday Simba Shomari
Kwa jina anaitwa Athuman Juma Ubao au AJ Ubao au Father D, alizaliwa katika hospitali ya Ocean Rd jijini Daressalaam Tanzania ni mtoto wa pili katika familia ya Mzee Juma Ubao a.k.a King Makusa.

Aj anasema “nimetokea kwenye ukoo wa muziki kuanzia kwa babu yangu hadi baba mzazi ambaye ni mkongwe wa muziki Tanzania na enzi zake alikuwa akienda kurekodi miziki Nairobi Kenya akiwa na bendi yake Six Manyara kwani wakati huo hakukuwa na studio pale nyumbani Tanzania”.

Lakini hivi sasa mzee Ubao ameanzisha kundi liitwalo Wanne Cultural Group akiendeleza libeneke katika utamaduni wa Mtanzania.

Kwahiyo alianza muziki miaka mitano iliyopita akiwa katika kikundi kiitwacho “The Swahili” akiwa na mwenzake Herry Omary a.k.a Dirty Herry hapa Washington Dc. Anaendelea kusem “tulitoa albam moja ambayo haikupata mafanikio makubwa”.

Hapo basi ndipo alipoamua kubadili mwelekeo wake wa muziki kama mwimbaji na Rapper kwasababu anasema nimejifunza kwamba sikuhizi muziki wa R&B unategemea hiphop na hiphop nayo inategemea R&B kwahiyo unaweza ukavuta watu wote wa makundi hayo mawili kupenda muziki wako bila wasiwasi.

Hivi sasa nimeamua kuimba mwenyewe yaani “Solo” na kazi yangu ya kwanza inaitwa Haya ni Maisha yangu (This is my Life) na sababu ya kuipa jina hili anasema ni kwamba anaongelea juu ya maisha yake na mambo magumu aliyopitia.


Albam hii itakuwa ni katika miondoko ya R&B na HipHop na imetengenezwa na prodyuza Akili Msola a.k.a Mtaalam anasema “tunategemea itakamilika mwanzoni mwa mwaka ujao. Na itakuwa na nyimbo maarufu kama Adabu Tupu, Macho, Feel The Music, Haya ni maisha yangu na nyingine nyingi itakuwa ni moto mtupu anaongeza AJ.


“Nataka muziki wangu uwe wa starehe na pia kuelimisha jamii na ndio maaana naimba kwa lugha mbili kiingereza na Kiswahili na pia ndoto yangu ni kuwa mmoja wa wasanii bora kutoka Daressalaam Tanzania anasema AJ kwa utulivu mkubwa.

Napenda nichukue nafasi hii kushukuru blog yako, T&J Entertainment, Dj Luke Joe, Si Matani, DMK Global, Dj Joe, Afrikan Track, marafiki na mashabiki zangu wote wanaoniunga mkono katika safari yangu kimuziki nawaahidi muziki mzuri na msikose kununua albam yangu ikitoka nawaahidi sitowaangusha.

AJ ameonyesha ukomavu kwenye masuala ya muziki na hivi sasa anasema anafanya kazi kwa bidii kuweza kuwapa mashabiki zake muziki ulio bora zaidi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. eeh bwana AJ nasikia jumamosi iliyopita umefanya shooting ya video ya single yako hapo The gallery, silver spring sasa tuwekee basi hiyo video tuone nasikia kuna watoto wazuri balaa kwenye hiyo video si kitoto

    ReplyDelete
  2. Michuzi i think tunatanguliza baba before mwana yaani ingesomeka hivi KWA kimatumbi"KAMA BABA, KAMA MWANA" kwa kimombo ni "LIKE FATHER, LIKE SON"
    mdau mwl Kaizilege

    ReplyDelete
  3. KWELI ACHU HONGERA NA MUNGU ATAKUSAIDIA .UMEONA MBALI UKIWA MDOGO.USIJE UKAWAIGE WATU KAMA KINA DJ LUKE HAWAJUWI WANACHOKIFNYA .KAZI KUANGAIKA NA WANAWAKE NAKUSFIRI OVYO NA KUTOLETA MAENDELEO .MUNGU ATAKUSAIDIA SANA ,/

    ReplyDelete
  4. Wabongo sasa hivi kila mtu mwanamuziki..hasa nani atasikiliza hiyo miziki?! si wengine tuwe wasikilizaji?~

    ReplyDelete
  5. Mimi nashindwa kuelewa hii article imeandikwa na nani kati ya Sunday Shomari na Athuman Juma? Kwa sababu grammar inachanganya mara alipoamu.... mara nimeamua.....

    Try to be very clear, when you communicate so that readers can know clearly who is sending message.

    ReplyDelete
  6. my man thats wuz up keep it up iam in london airport right now i just saw this post on my way to bongo. Keep DC bongo on the map mohammed peace one love. yo if u see this hit me up on the email moesua@live.com.

    ReplyDelete
  7. Watanzania tuache vijitabia vya kukosoa na kulalamika sana,badala yake tuwe na mtazamo mwema,kama kuna moja ya watoto wetu kafanikiwa kisanaa au kimichezo kwanini?tusimpe moyo badala yake tumekuwa tunaangalia wapi pamekosewa katika Lugha,hata shuleni sio wanafunzi wote sawa,

    ReplyDelete
  8. AJ fata ndoto yako ipo cku na wewe utakuwa juu kama wakina AY,Mwana FA, Chidi Benzi na wengineo. Keep DC rolling na U.S mzima. Endeleza kipaji chako utafika unapokwenda japokuwa ni mbali. Maisha hamna kukata tamaa do ur thing

    ReplyDelete
  9. Kama shuleni wanafunzi wote sio sawa kwanini usimshauri AJ atafute mtu aliyezingatia masomo ndio aandike historia yake? AJ, wewe ni mtu poa lakini washauri wako ndio wapuuzi. Tafuta mshauri aliyeenda shule... All the best.

    ReplyDelete
  10. achu,Aj Congratulation man, wishing you all the best and i know you will make it man no dough no dignity,Go GO GO achu.salaam mama mwambiye mdau wa new york kamsalimiye...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...