Mshiriki wa Big Brother E,izabeth Gupta akiongea na wanahabari leo hoteli ya Paradise jijini Dar. Kulia ni bosi wa operesheni wa MultiChoice Baraka Shelukindo na shoto ni afisa operesheni wa MultiChoice Grace Urassa. Pamoja na mambo mengine Elizabeth amewashukuru wadau kwa kumpigia kura na kumpa taffu katika kipindi chote alichokuwa mjengoni.
kasema ana mpango wa kurudi masomoni kwani ndio kwanza kamaliza kidato cha sita hivyo ana kiu ya kusoma sanaa na kuigiza pamoja. amesema anapenda kuigiza na kuimba na ameshawahi kuwa mtangazaji. amesema anatafuta sponsa kujiendeleza katika sanaa na akimkosa atajilipia mwenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Hongera Elizabeth. Ulikuwa huru kufanya chochote ulipokuwa BBA lakini ulijisitiri kwa heshima yako na Taifa lako.

    Wasichana wa umri wako wanaweza kujifunza kitu kizuri kutoka kwako, kutolipiza kisasi.

    Uzalendo wako. Walipoongelea kuhusu Coco Master wewe ukaongelea kina AY na Professa J wako.

    Upungufu upo kwa kila binadamu lakini umekuwa darasa la uzalendo ambalo wengi tunapata fursa ya kuliendeleza lakini tunaishia kutangaza mambo ya watu wengine.Binafsi Ninakupongeza.Jiendeleze zaidi.

    ReplyDelete
  2. We love u Elizabeth and we are proud of you. Umetuwakilisha kwa kiwango kizuri sana, hasa ukizingatia wewe ni kijana wa kike tumependa sana uwakilishi wako kwa kweli. Nakutakia kila la kheri kwenywe maisha yako mrembo

    ReplyDelete
  3. mtoto katulia sana, kaka michuzi hebu weka na namba ya mtoto huyo

    ReplyDelete
  4. safi sana dada,
    hata mimi nipo tayari kusaidia senti kidogo za masomo

    ReplyDelete
  5. Hi Gru good to hear abt yr service with MultiChoice.

    Elizabeth, welcome back home!

    Regards,

    Masoka - Alumnus;
    jmoseemoseej@yahoo.co.uk
    The Netherlands

    ReplyDelete
  6. Ya mjengoni yamebaki hapo zamani za kale, angalia makosa uliyofanya and 'think positively 'na ujifunze kuishi kama mtoto wa africa tena wa kitanzania. Wewe siyo mbaya wa tabia hivyoo ila unaonekana huna 'exposure' kwa umri wako unahitaji kujenga future kwa kujipanga sawa sawa. Fikiria mbele zaidi unakotakiwa kwenda na si ulikotoka.I waz your fun anyway, it waz a 'game' lakini game la maisha linaendelea, kila binadamu ana udhaifu fulani lakini songa mbele mdogo wangu. watasema sana lakini kama nilikuambia imebaki "hapo zamani za kale" najua umri wako nao unachangia but still you have a chance. ni hayo tu my sis'

    ReplyDelete
  7. mimi kwakweli nimefurahishwa na Eliza sio siri kaka michuzi yani dada uyu siyo kama yuleeee, utofauti mkubwa upo jamani.. alafuu heshima, yale maisha mengine ni weekness tu kila mtu anazake huwezi act mule ndani, unaishi jinsi ulivyo. all in all she is the best.

    Hongera Eliza, hongera pia kwakushukuru wapiga kura wako. ni vizuri.

    Mdau,
    Nam.

    ReplyDelete
  8. mimi kwakweli nimefurahishwa na Eliza sio siri kaka michuzi yani dada uyu siyo kama yuleeee, utofauti mkubwa upo jamani.. alafuu heshima, yale maisha mengine ni weekness tu kila mtu anazake huwezi act mule ndani, unaishi jinsi ulivyo. all in all she is the best.

    Hongera Eliza, hongera pia kwakushukuru wapiga kura wako. ni vizuri.

    Mdau,
    Nam.

    ReplyDelete
  9. hongera sana Elizabeth usijali kutoka kwenye mjengo sio mwisho wa maisha u have long way to go usiangalie nyuma ulikotoka angalia mbele and rekebisha yale utakayo yaona ulifanya vibaya ndani ya mjengo.hongera sana Elizabeth we ar proud of u gel

    ReplyDelete
  10. DSTV ovyo sana yan local channels katika list yao eti TBC tu ndo ipo

    cable ya wapenda tamaduni za nje,mmeniudhi sana

    eliza anyway sikukujua ivo ila karibu home na uishi kama wabongo tu kwa uzuri lakini

    ReplyDelete
  11. Michu, niko tayari kusaidia provided anaacha yale maneno mbofu mbofu niliyokuwa nikisikia akiongea mjengoni.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana mdogo wangu Eliza. Ulijitahidi kadri uwezavyo lakini umekubali kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani. Umerudi uraiani kaza buti utafanikiwa tu

    ReplyDelete
  13. Hey baraka mambo?

    ReplyDelete
  14. She is young and has got that strong spirit. But the sad side is, Is it true that her mother kills the husband?that is existing story in Moshi up to now?

    ReplyDelete
  15. Grace Urasa hongera

    ReplyDelete
  16. Grace urassa wa wapi wewe dada..machame au rombo_mrembo kweli kweli!!hiyo itakuwa machame tuuu

    ReplyDelete
  17. inasemekana ni mjamzito. ya kweli haya??

    ReplyDelete
  18. Eliza mie nilipenda ulivyokuwa ukijiheshimu mle ndani ya mjengo.Pls!!may i have ur email adress,just send it through mtulinagwe@yahoo.com. or u can drop it here...tulline.

    ReplyDelete
  19. Elizabeth,nimesikitika sana kwamba umetoka kipindi hiki, ukweli ni kwamba wewe ilikuwa bora kuliko Leonel,Geraldine,Nnkena na Emma,Africa ilikupenda sana na mwanzoni na ulipobadilika tu ikakugeuka maana ulionekana kama ulifake tabia yako hapo mwanzona Mzamo ambae alionekana fake mwanzoni akaonekana yuko real ,vinginevyo ulipaswa kuwa kwenye tatu bora.anyway chukua hiyo kama changamoto maana changamoto kubwailikuwa ni mahusiano na wenzio ndani ya nyumba.Otherwise all the best,tumikia kafiri upate mradi wako na sponsa utampata.

    ReplyDelete
  20. Hiyo hadithi hata yeye aliisema mle ndani kuwa mamake alituhumiwa kwa kumuua baba yake,but nadhani ni uzushi,ukizingatia babake alikuwa mhindi.

    ReplyDelete
  21. Nimekusikia kwenye TBC leoumesema mchezo ilikuwa mgumu kwako kwa ajili ya sheria mpya na kwamba ulikuwa peke yako, hata mzamo yuko peke yake, ni mahisiano tu na wenzio ndiyo yaliyokushinda, maana hata wangekuswap mara ngapi Africa bado ingekuweka tu kama Eddie au Kevin,na upigaji kurani knyume na miaka iliyopita lakini bado ni vilevile unampigia unayempenda, sobado ungepigiwa tu, usijitetee kwa hilo,ni kweli guys wetu walifanya vizuri kuliko nyie,labda kwa kuwa walikuwa wavumilivu sana.
    dada punguza tu hasira utafanikiwa,hazina maana sana sana zitakurudisha nyuma

    ReplyDelete
  22. Elizabeth ...mimi gauuzz@yahoo.com nilikuwa mstari wa mbele sana kukucampaignia ulipokuwa ndani ya nyumba ... nilianzisha "EMSC" yaani Elizabwth Must Stay Campaign kwenye BBR website ... na kwa kweli ilisaidia kwa kiasi fulani ...Ila kosa kubwa ulilolifanya ni pale uliposema kuwa hujawahi kufanya mapenzi na mtu asiye mzungu ...pale kidogo ukafanya mambo yawe magumu kwa upande wangu sababu watu walianza kudhani kuwa wewe ni racist ... kosa lingine ni pale uliporushiana maneno na Itai na kusema ataona cha mtema kuni akiendelea kukufuata fuata ..pale watu waliona kuwa umeanza kuvimba kichwa kwa kuwa umesurvive more than two eviction ... Kosa la mwisho ni pale ulipodhihaki kwa kuosema kuwa Mzamo naye amepona kutolewa? hapa kidogo ikawa ndio msumari kwako ...na Mzamo kwenye diary room akakushtaki kwa Big Brother kwamba anamchunia eti kwa vile amekunominate ... huo ndio ukwa mshale wa mwisho na mimi nguvu zikaniishia ...

    ANYWAY ...NAFURAHIA MSIMAMO WAKO NA INTERGRITY ... NINGEKUWA NA MTOTO WA KIKE NINGEMLETA KWAKO UWE KUNGWI WAKE

    SO FAR HONGERA SANA AND ALL THE BEST

    ReplyDelete
  23. mie naoana ulipata kichwa baada ya kupona eviction mbili na Kevin, ukweli ni kwamba alikubeba sana,na rafiki mwema,lakini yote heri umerudi nyumbani uanze maisha mengine pambana sana utafanikiwa.

    ReplyDelete
  24. Jamani wadau mnaosema mama wa Eliza alimuua baba wa Eliza. Hebu jiwekeni katika nafasi ya mama Eliza. Inawezekana kweli mna watoto 4 pamoja na mmeishi pamoja miaka mingi mtu afanye kitendo hicho?Kulea kulivyo kazi hivyo inawezekana kweli?
    1. Kama walimtuhumu hivyo. Postmortum haikufanywa? na kwanini isifanywe?
    Binafsi naifahamu vizuri mno familia ya Eliza. Na siamini hilo linalosemwa. Kifo ni kifo tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...