Nimekuwa msomaji mzuri wa makala za Mashaka na ninakiri kuwa ana uwezo mkubwa wa kuchambua masula mbali mbali kwa kina na kitaalamu.

Habari ya shirikisho la Afrika Mashariki limejaa hila zilizojificha na kama viongozi wetu hawatakuwa makini,wataliangamiza taifa letu na kizazi kijacho. Ikiwa watapenda kuvikwa kilemba cha ukoka kwa kusifiwa kwenye majukwaa ya kisiasa na pengine kutunikiwa nishani kuwa kufanikisha muungano wa Afrika Mashariki,basi laana ya kizazi kijacho itawafuata huko huko watakapokokuwa iwe ahera au kwingineko.

Haiitaji mtu kutumia akili nyingi kujua kuwa majirani zetu wana uchu na ardhi yetu. Mfano,Kenya sehemu kubwa ya ardhi inayofaa kwa kilimo wanayo makabwela. Huko Rwanda nadhani wataanza kuchoma maiti kwa kukosa sehemu za kuzikia! Sasa hawa viongozi wao unadhani wanataka shirikikisho hili ili na “sisi” tuendelee? Nani kasema?

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi, majirani zetu wanajua fika kuwa viongozi wetu akili zao ziko kwenye kutafuta ushindi kwa namna yeyote ile na wanaweza wakasainikirahisi mikataba bila ya kuwa na muda wa kutafakari. Ndiyo maana wanaongeza shinikizo kadiri muda unavyokwenda ili saini iwekwe na waje kuwahi nchi yetu tuliyopendelewa na Mungu. Wenzetu wanafikiria kesho kutwa wakati sisi tunafikiria chakula cha leo tena cha kwangu!

Rafiki yangu daktari alikuwa nafanya kazi Kenya kwenye taasisi fulani. Mwaka ulipoisha wakakataa kumpa mkataba mwingine wakisema waziwazi kuwa watampa tu ikiwa hamna mkenya atakayepatikana kuijaza hiyo nafasi. Sasa hawa watu ndo mnataka kuwapa uhuru wa kufanya kazi hapa tuache wazalendo wakimangamanga mtaani eti ni mambo ya soko huria? Huo utakuwa ni uvivu wa hali ya juu wa kushindwa kutumia akili zetu ipasavyo.

Tazama uchaguzi uliofanyika huko Kenya na kuleta maafa makubwa. Kwa mtu makini anajua kabisa kuwa kiini kilikuwa ni ardhi, kwamba watu wengi tena masikini hawana ardhi . Tunahitaji tena onyo kali kutoka kwa Mungu zaidi ya hili. Ok, Mungu akatuonyesha tena juu ya mgogoro aliousema kaka Masaka wa kisiwa kidogo cha saizi ndogo kuliko uwanja wa mpira wa miguu. Mpaka maraisi wao wakawa wanasutana. Mwingine akasema kisiwa si changu bali maji yaliyozungua na vilivyomo ndani yake ni vya kwetu! Sasa hawa wakiona mbuga ya Selous si watasema kabla Yesu hajazaliwa hiyo mbuga ilimeguka kijiolojia na kuhamia Tanzania?

Ona jinsi walivyouana juu ya sakata la mfalme huko Ugand! Au mauaji ya Kimbari ambayo bado chuki yake haijaweza kuondoka hadi leo. Hivi jamani,tunahitaji afufuke Kinjeketile atuambie kuwa ni hatari kukimbilia shirikisho bila kuchukua tahadhari?

Sikatai kabisa kuwa shirikisho lina faida nyingi bali inabidi kuchukua tahadhari za hali ya juu kwani majirani zetu wamejawa na hila sana.

Tujihadhari na yale yanayotokea Zimbabwe yasije yakatokea kwa watoto wetu. Wazaliwe katika nchi ambayo hawataweza kwenda mkoa mwingine na kununua ardhi sababu ardhi yote yenye rutuba inamilikiwa na mhamiaji! Huoni kwamba tutatengeneza Mungiki wetu? Pata picha kama hali hiyo ingekuwa ndiyo iko hivi sasa, yaani mimi na wewe hatuna uhuru na ardhi yetu. Akitokea Mugabe wetu akatuambia chukueni bunduki tukawatoe wahamiaji hawa waliopora ardhi ya baba zetu, ani angekataa?

Hadithi ya ngamia mchoyo iwe fundísho kwetu. Viongozi wa nchi jirani wengine wana malengo yao ya kisiasa. Tena mmoja ameshatamka waziwazi kuwa anataka kuwa raisi wa kwanza wa shirikisho. Mtu wa namna hii ni wa kuwa naye makini. Unaweza ukasafiri na nyoka mfukoni kutoka Tegeta mpaka Msata ili mradi tu,hauweki mkono mfukoni. Viongozi wetu wangechukua tahadhari kama hii wanapokutana na wenzao kuongelea masuala ya shirikisho la África Mashariki.

Kama nchini mwao wameshindwa kushirikiana sembuse watashirikiana na sisi? Hao watutsi na wahutu wanaongea lugha moja na hawaelewani,sasa sisi inakuwaje?

Ridhaa ya wananchi inahitajika katika hili. kinyume na hapo,mie SIMO ila nakukumbusha uangalie historia ya kiongozi wa Romania aliyekataa kuondoka katika kasri yake. Kama unaona huko ni mbali basi angalia kwa komredi Mugabe basi kisha tafakari, chukua uamuzi!
Mungu ibariki Tanzania yetu
MDAU BS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Asante sana mdau hayo ndiyo mambo yanayotakiwa ata sisi wasiojua kiingeleza vizuri sasa tunajua kilichoandikwa ni nini. Tupo pamoja sio Mmarekani Mashaka make yeye hajui kuandika kiswahili

    ReplyDelete
  2. Israel na Palestina walianza kama hivi hivi. "Karibuni majirani zetu tejenge nchi... kwa nia safi kabisa" na matokeo yake ndiyo hayo! Miaka na miaka vita haviishi, wanaoathirika ni watoto, wanauliwa kila siku. Lakini wa kumlaumu ni wale viongozi wa Palestine wa enzi zileeee, aliyeruhusu wa Israel kupewa ardhi eti kwa muda tu. Ardhi bwana, asikudanganye mtu, Ardhi ni Maisha.
    Sasa viongozi wetu hawataona athari yake leo, wao watakuwa washakufa wakati vijukuu vyetu vinapigana vita na kina Ojwang na Othorongongo kugombania Ardhi huko Ukonga.

    ReplyDelete
  3. Tumshukuru Mashaka kwa mchango wake, sio wote hawaelewi anachoandika, lakini kuna wasioelewa, kama tutashirikiana na wale wenye upeo mzuri wa lugha zote mbili wakitusaidia kutafsiri anayoandika Mashaka ninaamini tutafika mbali!

    ReplyDelete
  4. watanzania tusimame kidete.Michuzi hakikisha ujumbe unafika kwa wenyewe.kwanza huo muungano tulishaaema basi,jasho litawatoka.Mungu akubariki michuzi mchango wako haupimiki

    ReplyDelete
  5. NYIE WATANZANIA ATI MWAOGOPA TUCHUKUE AJIRA YAKO YOOTE ATI KWASABABU HAMNA ELIMU BOLA. NJOONI KWA SHULE HAPA KENYA THEN YOU CAN COMPETE WITH US.

    ReplyDelete
  6. Makala nzuri, yote ulioyaeleza na mifano uliotoa yanahitaji mazingatio. Siku zote muungano wa unequals si wakuuingia kichwa kichwa na kwa kukurupuka, ndio maana hivi sasa wazanzibari tunalalamika sana juu ya muungano wetu. Kwa kweli umefanya jambo la maana sana kuandika kwa kiswahili hii inaanshiria unalenga kuwafikia watanzania wengi na sikutafuta umaarufu.

    Pia nakubaliana na wewe makala za bwana Mashaka zina maudhui mengi na ni za kitaalamu, kwa kweli mchango wake unahitajika ila binafsi I'm not his greatest fan. Watu wengi wamekuwa wakimshauri atumie kiswahili ila bado anang'ang'ania english, sasa sijui excuse yake ni kwamba hana skills za uandishi wa kiswahili au ndio misifa ya kitanzania kuonesha academic excellence na kimombo kinapanda?

    Personally, I think Mashaka is after fame and publicity more than reaching out to Tanzanians, sasa watu wa aina hii kidogo nina mashaka nao. Kwanza nimepeleleza wengi tuna post hizi makala za uchambuzi kwa pseudonames kama mimi Ahmed sio jina halisi hali kadhalika pen names kama mdau BS hapo juu na wengine wengi, ila John Mashaka amekuwa shujaa mstari wa mbele kutangaza jina lake, istoshe anapewa praise sana hadi wengine wanamwita nabii na hakuna hata siku moja niliona akiandika makala to retract such claims instead anaendelea tu kutukosha na beautiful articles, I wonder what is in for him!

    Kwa kumalizia, napendekeza kuanzishwe utaratibu kwa makala nzuri kama hizi au hata hizo za Mashaka ziwafikie hao wakubwa wayafanyie kazi mapendezo au kuaddress hizo concerns, bila hivo tija itakayopatikana baada ya kusomeka hapa tu itakuwa ndogo sana.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  7. afadhali yan leo nimesoma kabisa hii makala,,tumekupata mdau

    ujume ufike kwa walengwa,yani tunasema ivi mtu awaye yeyote atayeuza ardhi ya Tanzania kwa hao majirani atalaanika milele na kizazi chake excpet wale wataotubutu na kurudisha gharama...
    hatupimi nn wala nn apa hatutaki arhdi iwe ktk list ya "MGAO" umeme unatosha kabisaa

    ReplyDelete
  8. Mada nzuri sana, hilo shirikisho labda tujaribu 2020 si sasa, angalia nchi wanachama wote tunamatatizo makubwa, kama bongo ya kwetu wenyewe yametushinda mfano ufisadi, muungano, katiba, system nk na yanazidi kutuelemea..sijui 2015 tutakuwa wapi.
    Tz tunahitaji miaka 10 ya kurekebisha ya ndani
    hao wakenya, uganda wenyewe kwa wenyewe hawapendani ni ukabila tuu..
    siogopi EAC lkn sioni mwenyesifa ya kuungana nae hapo wote wanafiki na wabinafsi

    ReplyDelete
  9. kwakweli mdau tume kusikiliza kwa makini kuhusu muungano wa Afrika mashariki. huumungano wa Afrka mashariki hao watu wengine wana malengo yao yaki siyasa na wa TaNZANIA msipo kuwa makini kuhusu hawo watu miaka yambeleni mtajuta. mfano wakaribu tazama jinsi wanyarwanda walivyo pata ardhi inhini Congo (RDC) walipewa hifadhi kila kitu cha muhimu ila tazama jinsi walivyo leta vita wakidai kwamba wao ni wa KONGO hadi leo wanaweka vurugu. hiliswala ninzito maana nimpango ambao utachukuwa mda mrefu. Ebu Rais Mobutu angekuwepo kwasasa inge kuwaje???? tazama jinsi wakongo wanavyo hangaika .kwasababu mobutu kaharibu kila kitu nakwasasa nivigumu kurekebisha hali ya CONGO.

    ReplyDelete
  10. mdauz bs leo umetukuna wengi manake viinglish vilikuwa vinatuletea kigugumizi cha utu uzima hii ndo mambo tunataka ingawa kila mtu ana uhuru wake lakini ili ujumbe uwafikie walengwa asilimia tisini ni kiswaz tu ndo kinanoga ebu mashaka anguka kiswazi uone idadi ya wadau siku hiyo hadi mia tano watafika! si mnakumbuka yale mapicha ya king mswati wadau walivyochangia kwa bidii nilichekaga hadi basi kweli kiswazz kina raha sana kidu kidumu kidumu asante bs

    ReplyDelete
  11. wewe mdau, nadhani itakuwa vyema sana ikiwa unaweza kujitolea kutafsiri makala ya John Mashaka ili wale ambao chiingilish not richebo nao waweze kunufaika kuliko yule Taleban leader US-Blogger.

    Makala ya mashaka yana maana sana, kwa hiyo yangekuwa yanatafsiriwa kwa kiswahili watu wengine sana wangenufaika kwa mawaidha yake. Wajama, naombeni msaada, hivi yule Joseph Ikalimba kazukia wapi? Ananiachaga hoi, yaani mkali kuliko Peter Nalitolela

    ReplyDelete
  12. nashukuru kwa michango mizuri na hoja zilizotolewa na mwandishi wa nakala hii. tunahitaji viongozi wanaofikiri zaidi ya matumbo yao.wawapende wengine kama wanavyojipenda wao.

    ni muhimu sana kujua kuwa sisi ni mtandao, ni kama utandu wa buibui. kila mmoja ni sehemu ya huo utandu(web) chochote utakachokifanya kuathiri huo utandu, unajifanyia wewe mwenyewe na athari yeyote itakayotokea katika huo utandu, ni athari kwako kwa asilimia mia moja. ni lazima tuwe na watu wenye fikra kama hii.

    sisi ni watanzania, ni utandu wa watanzania, na kila mmoja ameshikilia maisha ya huu utandu.

    utajiri wa hapa norway ni wa miaka 60 tu iliyopita. wametawaliwa kwa zaidi ya miaka 400 wakiwa maskiini sana. baada ya ugunduzi wa mafuta miaka 60 iliyopita, na kuweka utaratibu na kwamba faida ni kwa wanorway na lengo kubwa likiwa ni wazawa wenyewe, ndio norway unayoiona leo. viongozi wanafikiria zaidi maisha bora kwa wanaowaongoza na hivyo ni wazi kuwa kwa kuwa nao ni sehemu ya hiyo web, utandu, mtandao, basi na wao maisha yao kuwa bora.

    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  13. TANZANIA KAMA TUKIFANIKIWA KUPIGANA DHIDI YA UDINI NA UMBUMBUMBU WA KISIASA HII NI NCHI BORA KABISA HAPA DUNIANI TUNA KILA KITU ILA TATIZO SIJUI NI NANI KATULOGA?

    ReplyDelete
  14. MDAU AHMAD,

    UNAPONDA MAKALA ZA KIINGEREZA ILI HALI WEWE UNAKITUMIA TENA UNAKITUMIA KWENYE KUPONDA...HAHAHA...!!!! NINAVYOJUA MIMI MAMBO YA MUUNGANO YANA HATUA MBALIMBALI AMBALO HILI LINALOJADILIWA HAPA NI MUUNGANIKO WA KIUCHUMI NA MWISHO WAKE UPO MUUNGANIKO WA KISIASA AMBAPO MIUNGANIKO HII MIWILI ISIPOANGALIWA KWA MAKINI WANAANCHI WA CHINI NDIO WATAKAOUMIA. PIA SERA ZA UMILIKAJI WA ARDHI KWA WANANCHI HAZIJAKAA VIZURI SANA HAPA NCHINI SASA LIKICHANGANYWA KWENYE MUUNGANO NDIO MAMBO YATAZIDI KUAHARIBIKA ZAIDI.

    ReplyDelete
  15. HAWA VIONGOZI WETU WANA TAMAA SANA.MARA NYINGI WANAPOTUNGA SHERIA HAWAFIKIRI VIZAZI VIJAZO. mara nyingi wanapotunga sheria zao hawazipitili kwa mapana. kama mdau ailivyo sema hapo awali...yaani amenukuu points muhimu sana ambazo inabidi watu wailimishwa juu ya sakata hili.viongozi wetu wanafeli kujua ya kuwa hata yule ombaomba ana haki yake..haimaanishi haendeshi gari au hana bajaji anyimwe haki yake. kuna article moja NILIWAHI KUISOMA...KATIKATI YA MWAKA YA KUWA WAKULIMA WA VITUNGUU TANZANIA WANAKANDAMIZWA KWENYE SOKO LAO, NA HAO WAKENYA...HAKUNA ARDHI NZURI KWENYE EAST AFRICA KAMA ya TANZANIA.

    sitaki kutoa hutuba hapa ila mdau nakushuru kwa kuweka wazi swala hili na sio wengine hao vibaraka kutaka kutumia ulimi wa mazingaombwe wa lugha kuwabababisha watu...NA VIONGOZI ACHENI TAMAA...MSITUTIE KWENYE VITA KISA NI "NG'OME MMOJA KUULIWA".

    ReplyDelete
  16. This is like telling a 2 yaer old child not to eat too many chocolate biscuits and then leaving a cookie jar open, our current generation of leaders are just as irresponsible as 2 years old child, if they do something they will, with no thought for the future, we all know that our leaders think they are God's gift for some strange reasons and they will never change their ways until their hand is forced!

    ReplyDelete
  17. safi sana big up na wachangijia wa maona shukran sana kwa mara ya kwanza kabisa nasema bi up kwa mwenye kuandika nakala hii na wachangiaji hoja na kwako bro michu kwa kutuwekea mtandaoni hoja hii..ila kuna kitu kimoja nacho ni bwana Ahmed ulimsema mwenzio kwamba sijui kwa nini hatumi lugha ya kiswahili katika makala zake labda ndo hivyo ulivyosema academic excellence na kimombo kinapanda lakini na wewe je mbona umetupia tupia vijineno vya hapa na pale vya kizungu au tujue na wewe kwamba kinapanda lakini umeamua kubanisha,si fresh ukitumia lugha mmoja basi nenda nayo hiyo hiyo kwa sababu si wote wanaofahamu hivyo vijineno neno vya kimombo ulivyovitumia..

    alamsik

    ReplyDelete
  18. TUMEONA NA KUSOMA MAKALA NYINGI KUHUSU MUUNGANO WA EAST AFRICA.SASA NI NINI KIFANYIKE?MUUNGANO NI MUHIMU SANA.KUNA SHRIA TUNAWEZA KUTUNGA SHERIA ZA MAJIMBO KUHUSU MUUNGANO KATIKA HII ISSUE YA ARDHI.TUWE NA AKILI SIO TU TUSEME BASI HAPANA.ALAFU LAZIMA UJUE WABURUNDI NA WARWANDA WALIKUWA WATANGANYIKA ENZI ZILE.JE WAO WAKISEMA TUNATAKA TANGANYIKA YETU WEWE UTASEMAJE.JIBU HAPA NDUGU ZANGU NI KWAMBA TUNATAKIWA TUIFADHI ARDHI KUANZIA SASA.INASIKITIKA SANA KUONA WATANZANIA ETI WANASEMA TUNA ARDHI NYINGI HAPA.WAMESHINDAWA KUJUA KUWA WANAISHI NA VIUMBE WENGINE [SPECIES],KAMA WANAYAMA WA PORINI,AMBAO VILE VILE UTULETEA FAIDA KUBWA SISI BINADAMU[WATALII KUJA HAPA].TUKIONA WEZETU WANANYOLEWA SISI TUWEKE MAJI.HATA KILIMO.TUNATAKIWA SASA HIVI KUWA NA SHERIA NZURI ILI WATU WASICHUKUE SEHEMU KUBWA YA ARDHI,na ardhi ibaki kuwa mali ya serikali.Na ujenzi wa nyumba kuanzia sasa uwe wa mpangilio unaofaa wa kuifadhi ardhi.wataalam wa ardhi na mipango miji sasa ndio wakati wa kuweza kusaidia kuifadhi ardhi yetu.Na inabidi tufanye utafiti hata kuingia kidogo kwenye bahali kwa ajili ya majengo tu ili kuwezesha kuwa na ardhi kwa ajili ya kilimo huko bara.Na vijiji vinavyozunguka kwenye mbuga za wanyama ziwezeshwe kujengwa nyumba za ghorofa[flat].mtu anatakiwa kununu kiwanda juu ya nyumba ya mtu.au serikali ijenge flat ,wakishirikiana na wanakijiji ili.PESA IPO,TANAPA LAZIMA WASAIDIE HILI ZOEZI.SIO KUKAA TU KIMYA HUKU MBUGA ZA WANAYAMA ZIKIVAMIWA NA KUWAFANYA WANYAMA WAKIMBIE NA HATIMAYE KUPOTEA KABISA KWANI HAKUTOKUEPO NA ARDHI TENA.MUNGU IBARIKI EAST AFRICA.

    ReplyDelete
  19. KELELE ZENU HUMU KWA MICHUZI AZIBADILISHI KITU....KAPIGANIENI UBUNGE LABDA MTASIKIKA.
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  20. NIMEFURAHISHWA NA MCHANGO KWA KISWAHILI SAFI SANA, NA HONGERA SANA ENDELEA HIVYO HIVYO NA WENGINE TUWAIGA, NA KIINGILISHI PIA SI VIBAYA TUWEZA KUTUMIA LUGHA ZOTE MBILI

    ReplyDelete
  21. ALLANI MAKWAIYANovember 12, 2009

    This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  22. HONGERA SANA KWA UAMUZI WAKO WA KUTUMIA LUGHA YETU YA TAIFA KWENYE MADA YAKO. KINACHINISIKITISHA KWENYE HII ARTICLE YAKO NI KWAMBA UNARUDIA YALEYALE YALIYOANDIKWA NA WENGINE BILA KUTOA UFUMBUZI WOWOTE.

    NI KWELI KWAMBA MAJIRANI ZETU WANA MATATIZO YA ARDHI, UBINAFSI, NA UKABILAL LAKINI SWALI NI KWAMBA JE TANZANIA IENDELEE KUJITENGA KATIKA DUNIA AMBAYO NCHI NYINGI ZILIZOENDELEA ZINAJITAHIDI KUFORM REGIONAL INTERGRATIONS? AFRICA TUTAWEZAJE KUPAMBANA NA NCHI ZA JUMIIYA YA ULAYA, ASIA, AU AMARICA KASKAZINI (NAFTA) BILA YA SISI KUWA NA JUMUIYA MADHUBUTI ZA KIUCHUMI?

    KWA MTAZAMO WANGU MIMI, SUALA LILOPO NI JINSI GANI TUNAWEZA KUBORESHA MASHARTI YA KUJIUNGA NA HIZI JUMUIYA, NA PIA KUWEKA MUDA MAALUM AMBAO MHAMIAJI KWENYE NCHI NYINGINE AMBAYO NI MWANACHAMA WA HII JUMUIYA ATATAKIWA KUKAA KABLA YA KUWA NA HAKI YA KUMILIKI ARDHI AU RASILIMALI ZINGINE. LAKINI KUENDELE KULAUMU NA KUIPINGA JUMUIYA BILA KUTOA SULUHISHO HATUTAFIKA KOKOTE.

    NAFASI YA TANZANIA PEKE YAKE KUPAMBANA NA VIKWAZO VYA BIASHARA VYA WTO NA GATT NI NDOGO SANA KULIKO KUTIA JUMIA ZA KIUCHUMI.

    BRO' K.

    ReplyDelete
  23. Duh katika comments zote ya ALLANI MAKWAIYA komesha, haina mwanzo wala mwisho. Teheehehehehe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...