mjasiriamali maarufu jijini iddi janguo ameingiza mjini dar limo aina ya Chevy Krystal ambayo kama kawaida itatumika kwa kubeba watu kwenye sherehe na matukio
iddi akiwasili viwanja vya leaders club na limo lake
kijana wa iddi akijidai na mchuma wa baba
iddi akiwa ndani ya limo lake
anko naye alionja kidogo uroda wa limo...





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. VERY CLASS! HIVI HUYU IDD JANGUO NILIMFAHAMU ZAMANI SANA NDIE ALIYEMUOA AZIZA MADATI AU?

    ReplyDelete
  2. yeah ndo mwenyewe mzee wa totoz! Babake alikua Bandari walitesa sana kipindi kile cha Mzee Rukhsa! Naona bado yuko juu jamaa! holla!

    ReplyDelete
  3. Michuzi umependeza ndani ya limo we acha tu bongo !

    ReplyDelete
  4. duh michuzi unameremeta humo ndani unaonekana msafiiiiiii uko juu kama hilo limo

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza,Iddi hajamuoa Aziza Madati bwana,walibwagana kitamboooooooooo.

    ReplyDelete
  6. Hapo ukipiga lesi mara moja tu ujuwe lita moja ya wese imeondoka kwa kifupi kanunua jini hilo.

    ReplyDelete
  7. Huyu Idd mkewe si anaitwa Nadhifa chamali? au sio huyu?

    ReplyDelete
  8. huyu idd mkewe si Nadhifa chamali?au sio huyu?

    ReplyDelete
  9. mdogo wake na Iddy ndiyo alikuwa anatoka na miss Madati

    ReplyDelete
  10. Hivi left hand bado zinaruhusiwa Bongo au kwa vile mtoto wa who is who? usibane hii Michuzi

    ReplyDelete
  11. kwa wenzetu kule majuu gari hii is used to service those who have crossed to the second world. Can you dare Michuzi to avail this comment? I cannot hire it i\even for free I swear

    ReplyDelete
  12. mie nakumbuka hirizi tu.

    ReplyDelete
  13. Mzaramo huyu anamatusi ya Kwao Mwanarumango.

    ReplyDelete
  14. Anko sio URODA ni UDORA

    ReplyDelete
  15. Du kuna watu wana jelasi Noma umelazimishwa ukakodishe ???? ukiwa na uwezo wakuvuta mchuma kama huo wese kwako sio bajeti unamwaga tu Mpigieni salute tu kapiga Bao si mchezo

    ReplyDelete
  16. wabobongo wana roho mbaya jamani kaaaa, hapo wanataongea manegativu weee na wengine wanataka kuharibu ndoa ya jamaa

    ReplyDelete
  17. Watoto hawa wamezaliwa wameikuta pesa, maana baba mjasiriamali, mama mjasiriamali, na watoto hawakujibweteka. Watoto wengine waliojibweteka wazazi wao walikuwa matawi ya juu sasa hivi wanajuta an wamekwisharost.

    Kama biashara ipo na wateja wapo kwanini asilete limo akajiingizia pesa zake? Si watu wenyewe wanataka kwenye maharusi na magraduation yao! Sasa tabu iwapi, kama suala la mafuta hilo si tatizo linaingizwa kwenye bei ya kukodi.

    ReplyDelete
  18. Hii kweli ni BUY ONE GET ONE FREE. mtu kauliza kama ni yule iddi aliemuo AZIZA mwingine anajibu eti ooh mtu wa totoz hata kama ni mtu wa totoz si yeye.

    ReplyDelete
  19. hivi hao wanaomkanda wote wako nje hao, wanatumind tuliokuwa bongo tuliowini njooni bongo acheni kuosha vyombo huko, iddi umepiga bao, wazee wa upanga magnet - house balm beach twakupa saluti, kamua mwanetu

    ReplyDelete
  20. Hili ndo kanunua baada ya kula mshiko wa bima ya lililoungua hapo juu???ufisadi bongo hautaisha....tambarareeee.

    ReplyDelete
  21. MICHUZI UTANISAMEHE... wadau wabeba maboxi bado wana mambo ya kitotoo sana kuuliza alikuwa anamchukua na nani, kamuoa nani, babake alikuja, mara hirizi hayoyote yametoka wapi??? Mpeni hongera kijana wa Janguo kwa ujasiriamali wake

    ReplyDelete
  22. Jamani yule saidi janguo yuko wapi? mbona yeye hasikiki? kafulia nini?! hebu michu siku moja tuwekee tumuone mpaka tushamsahau!

    ReplyDelete
  23. Watu bwana Mnawekewa Picha za Limo Ili mpeleke Harusi zenu mnaanza Majungu Mengine Mazaramo Juu. Watoto wa Kisarawe Na Dar hapa hapa sio Kuja leo.

    ReplyDelete
  24. BIMA ya lile liloungua imefanya kazi.

    WaBongo wana akili jamani! Khaah!

    ReplyDelete
  25. mmh, afadhali ngazi-ngazi leo imefuliwa!

    ReplyDelete
  26. Wabongo wana geere, mwaongelea wese, mwataka gari ile nini? tafuteni magari yanayokula chips basi. Bali angeingiza trekta 100 angekuwa amefanya jambo bora kwa mlala hoi. Hapo kawatengenezea wenye nazo, wanaopenda kutembea wamekaa.

    ReplyDelete
  27. Jamani hawa watu wanapata wapi pesa za kununulia magari kama haya?

    ReplyDelete
  28. Michu sidhani kama Chevy kristal ndio model yake, hiyo kristal ni dealership.

    ReplyDelete
  29. we anon hapo juu kwenda zako kule hiyo ni jelaz tu inakusumbua sijui gari used point ushuzz tu hiyo gari hata ukiirudisha ulaya bado na hakika watapanda macelebrity acha kujidai unajua mambo ya ulaya kuliko wenye nchi zao utabaki kuwa na donge hadi ufe na roho ya kwa nini nilijua mtasema huwa hamkosagi neno na roho zenu nzito wakija kina jay z watayapanda tu sembuse wewe kajamba nani kweli gunia la misumari halibebeki

    ReplyDelete
  30. Anaonekana alianza kuchoka kidogo. Au naye alikuwa juu ya mawe baada ya limo lake kuungua?

    Hongera bwana Idd. Penye nie pana njia.

    ReplyDelete
  31. Not bad for mtoto wa Kizaramo from MSANGA...

    mkwe MWARABU tick

    Fluss za kubadili mboga tick

    Kidi...tick

    kibanda cha kuishi..tick

    gari refu tick

    Haya ndio mambo tunayotaka kwa WAZARAMO

    ReplyDelete
  32. KWA WALE AMBAO TUNGEPENDA KUKODI'S KWA SHEREHE NI VIZURI PIA TUNGEJUA TRA TIN NAMBA ILI TUWE NA UHAKIKA HATUINGII KWENYE BIASHARA ISIYOLIPIWA USHURU.

    ReplyDelete
  33. WIVU! WIVU! WIVU! WIVU! JAMANI TUACHE WIVU!!!!!!

    ReplyDelete
  34. Wewe michuzi hamna chevy crystal hiyo crystal ni jina la dealership lakini hicho kitu kinaitwa chevy Tahoe baba ake kwa mwaka is more likely 99 lakini haijalishi maana africa kila kitu kutoka mtoni ni mupya.

    ReplyDelete
  35. Watu mijalusi na ntimanyongo imewajaa mtakufa na vijiba vya roho si na nyie mtafute biashara zenu. Yaani ni mazengwe tuu kila kitu mnaponda. Unaeuliza TIN namba si uende mwenyewe TRA ukaangalie unataka nani akufanyie hiyo kazi. Kama hutaki kukodi yako mabaloon kibao kakodishe.

    ReplyDelete
  36. HIVI JAMANI, WAHINDI NAO WANAPIGANA MADONGO HIVI?

    NAFIKIRI KITU CHA MSINGI, NI KUWA NA WIVU WA KIMAENDELEO, KAMA IDDI AMEFIKA HAPA, JE MIMI NIFANYE NINI KUMKARIBIA, AU HATA KUWA ZAIDI YAKE?

    WE SHOULD REGARD HIM AS A ROLE MODEL, FOR OUR OWN BENEFIT.

    KUWA MTOTO WA KIGOGO, AU KUKULIA KWENYE FWEZA, SIO LAZIMA NAYE AWENAZO, NI JITIHADA ZA MTU BINAFSI.

    90% YA MILLIONAIRES/BILLIONAIRES IN THE WORL, ARE SELF MADE, HAWAKURITHI.

    ANYWAY: I LIKE THE CARE, IT'S WOW!!!! NAFIKIRI TRA WAMEISHA KAMATA KODI ZAO VIZURI, WELL DONE DOGO KWA KUCHANGIA UCHUMI WA JK

    Mzee wa BUGATI

    ReplyDelete
  37. Uliye Uliza Saidi Janguo yuko wapi Mie huyu Jamaa simjui sana ila Iddi Sindio Said? Said kwa kifupi Wabongo tunatumia Iddi Jamaa Kaamuwa mashallah Sasa kama mtu haonekani ndio kafulia mtu asioonekana Bora kuliko anayejionesha Kwenye masehemu Bora kukimbia Husada na Macho kuliko kuyatafuta. Inshallah Jamaa yatamfungulia mazuri zaidi na kila mtu wa humu Blog. Kondo.

    ReplyDelete
  38. Misupu, mtindo wa kuweka Miguu juu ya meza unaniudhi wewe! Gari yangu mi ikija hupandi kha!

    ReplyDelete
  39. Acha ushamba, achana na Michuzi, hilo ni bomba la kunin'ginizia miguu.

    ReplyDelete
  40. Mimi napenda kuuliza swala moja tu. Watanzania wanafanya kazi saa ngapi? Tunaelewa kuwa wadau wengi wa Bongo hawana uwezo wa kununua PC kwa hivyo wanategemea internet cafe. Tumieni muda wenu kujenga taifa lenu, sio kukaa tu na umbea na roho ya korosho. Angekuwa mzungu kaleta gari hapo, mngemkimbilia. Kama huna uwezo, kaa kimwa, waache wenye uwezo watanue. Hata Mungu hapendi Umbea.

    Tuache kujali jirani amepata wapi pesa za kutanua. Anza kujali kwa nini wewe uko arosto kuliko mwenzako na utafanya nini ili ujiendeleze. Nenda nchi yoyote nje ya Tanzania, hutakuta watu wengi wamekaa mitaani saa za kazi, ni nchi yetu tu wananchi ni wavivu. Kwa nini lakini?

    ReplyDelete
  41. misupu ilo dole mkono wa kulia apo ndo nini?pozi,una kilema,holla au

    hahhahaaaa unapenda raha we mwanaume?

    ReplyDelete
  42. HIVI KWANINI WATANZANIA TUKIAMBIWA TUPUNGUZIWE BEI NA RISITI USIPEWE TUNAFURAHI? KWANINI HATUPENDI KUNUNUA VITU KWA BEI HALISI ILI TUPATE RISITI AMBAYO ITATHIBITISHA ULIPAJI WA KODI? KUNUNUA KITU UKADAI RISITI NAO NI WIVU? NI SISI WENYEWE TUNAOPENDA KULALAMA TUNAPOKOSA HUDUMA ZA KIJAMII KUTOKANA NA SISI WENYEWE KUPENDA SANA KUKWEPA KODI NA HASA WAFANYABIASHARA TOFAUTI NA WAAJIRIWA. WANAODAI KUWA NI WIVU NI HAOHAO WANAOWASIFU WAUZA UNGA KUWA NI WAFANYABIASHARA MAARUFU. bila kulipa kodi wewe si raia mwema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...