Na Mwandishi Wetu, Rome, Italia

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini hapa, Rome, Italia, usiku wa kuamkia leo, Jumapili, Novemba 15, 2009, kuhudhuria Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Hali ya Chakula Duniani.

Kwenye uwanja wa ndege, Rais Kikwete amepokewa na viongozi wa Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), maofisa wa Ubalozi wa Tanzania kwenye makao makuu ya FAO, na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

Maofisa hao waliongozwa na Balozi Wilfred Ngirwa, Mwakilishi wa Tanzania makao makuu wa FAO, na Balozi Ali Abeid Karume, Balozi wa Tanzania nchini Italia.

Akimwelezea Rais Kikwete juu ya Mkutano huo, Balozi Ngirwa amesema kuwa umeitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa FAO, Dkt. Jacques Diouf, kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu uliopita wa shirika hilo.

Balozi Ngirwa amesema kuwa Mkutano huo unafanyika kutokana na athari kwenye sekta ya kilimo zilizotokana na zahama ya sasa ya kiuchumi pamoja na uhaba wa chakula na bei kubwa za chakula duniani.

Mkutano huo ni wa tatu wa wakuu wa nchi kuzungumzia kilimo na chakula duniani baada ya mikutano miwili iliyofanyika 1996 na 2002.

Mkutano huo pia unaungwa mkono na viongozi wa mataifa makubwa duniani, akiwamo Barack Obama wa Marekani na kuwa unagharimiwa na Saudi Arabia ambayo imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 2.5 kufanikisha Mkutano huo.

Mara baada ya Rais Barack Obama kuingia madarakani mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Kikwete alimwandikia barua kiongozi huyo wa Marekani akimshauri aongoze kiwango cha uongozi katika nyanja ya chakula.

Rais Kikwete alimwambia Rais Obama kuwa kama kiongozi huyo wa Marekani alitaka kukumbukwa kwa uongozi bora duniani, basi njia bora zaidi ilikuwa ni kuelekeza nguvu zake katika kuendeleza kilimo na kupambana na ukosefu wa chakula duniani.

Mara baada ya kuwasili mjini Rome, Rais Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon katika Hoteli ya Ambasciatori Palace alikofikia Rais Kikwete na ujumbe wake.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano huo, Rais Kikwete amepangiwa kuhutubia Mkutano huo leo, Jumatatu, Novemba 16, kuanzia saa 10 mchana kwa saa za Italia (sawa na saa 12 jioni kwa saa za nyumbani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tanti auguri a voi tutti che inctranno a Roma per questo grande meeting. Volgiamo cibbo per tutti.

    ReplyDelete
  2. POLE KWA SAFARI KIJANA, HAYA MATATIZO YA NYUMBANI YATAJITATUA TU YENYEWE SIKU ZINAVYOKWENDA; AFTERALL ITV NA REDIO ONE WATAKUREKEBISHIA KWA KUYAFUNIKA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...