Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Abdirahim Haithar Haji akikagua timu kabambe ya Wazee Club a.k.a Arusha Veterani wakati wa ufunguzi wa michezo kuadhimisha miaka 10 ya Jumuiya iliyoanza leo uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini A-Taun. Shoto ni afande Amiri ambaye ni mmoja wa nyota wa timu hii inayoundwa na wakongwe toka sekta mbalimbali
Klabu ya Wazee a.k.a Arusha veterani wakikagulia na Mh.Abdirahim Haithar Haji
Timu ya Bunge la Tanzania ikikaguliwa na Mh.Abdirahim Haithar Haji
Mh.Abdirahim Haithar Haji akikagua timu ya Bunge la Tanzania
Timu ya Waheshimiwa wabunge wa Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu (suti nyeusi) akiwa na Spika wa Bunghe la Afrika Mashariki Mh.Abdirahim Haithar Haji wakati wa ugunguzi wa michezo hiyo
Meza kuu katika ufunguzi wa michezo ya kusherehekea miaka 10 ya Jumuiya
Hatari katika goli la Bunge la Tanzania (uzi mweupe) walipocheza na Arusha veterani
Bendi ya JWTZ ikitumbuiza

Waheshimwia wabunge wa Uganda wakishangilia bao
Picha na Habari na Woinde Shizza,
Arusha

Wabunge wa bunge la Kenya juzi walianza vyema michuano ya soka ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa jumuia ya Afrika ya mashariki baada ya kuwakung’uta wabunge wenzao wa Rwanda kwa mabao 5-1 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid wa mjini hapa leo.

Timu zinazoshiriki michuano hiyo inayofikia tamati siku ya kilele cha maadhimisho hayo novemba 20 mwaka huu ni pamoja za wabunge wa mabunge ya nchi za Tanzania,Rwanda,Kenya na Uganda pamoja na maveterani wa Wazee Club ya mjini hapa na wafanyakazi wa makao makuu ya Jumuia ya Afrika ya Mashariki

Katika mchezo huo wa fungua dimba, Kenya iliweza kutawala sehemu kubwa ya mchezo na mpaka mpaka wabunge hao wanakwenda mapumziko ilikuwa ikiongoza kwa mabao 5-0

Katika mchezo wa pili Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walishindwa kufurukuta baada ya kuchapwa mabo 2-0 na maveterani wa Wazee Club ya mjini hapoa

Wabunge hao wakiongozwa na Idd Azan aliyekuwa langoni huku safu ya washambuliaji ikiongozwa na Lucas Seleli na Ramadhani Maneno walishindwa kabisa kuupenya ukuta wa mabeki wa Wazee hao wa Arusha.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa wabunge wa Tanzania Hafidhi Alli alisema wamewafungwa kwa bahati mbaya kutokana na kuwa na muda mfupi wa mazoezi.

Alisema kuwa katika mchezo huo walikuwa wanaipima timu yao ambayo hivi sasa imeongeza wachezaji kadhaa wapya na amahidi kushinda michzo yote iliyobaki

Awali akifungua mashindano haya katibu mkuu wa Jumuiya Afrika ya mashariki balozi Juma Mwapachu alisema katika maadhimisho hayo wameamua kuwashindanisha wabunge ili waweze kutoa changamoto ya kizazi kipya kipende michezo.

“Tusisahau kwamba michezo ni furaha lakini pia michzo inatoa fursa kwa waheshimiwa wetu kupata mazoezi ya uhakika lakini pia kuwaleta karibu na wananchi,”alisema Mwapachu

Alitoa wito kwa watanzania kwa ujumla wapende michezo kwa kuwa ni ajira ambayo ulipa kuliko zaidi ya mtu anayeajiriwa ofisini

“Iwapo utashirikii michezo hutasikia hata siku moja ukinyemelewa ovyo homa na hasa wazee wenzangu,jamani tushiriki michezo, siyo kisa unaona umeitwa baba basi nawe unabweteka na kuacha michezo,tunatakiwa tupende michezo na tuwaase watoto wenu pia waipende ”alisema Balozi Mwapachu










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Majina ya Kizaramo sawa tu na ya Kiengereza Tiger kuna Chui Tabu Bahati chausiku Kipanya Mashavu Uengereza unakutana na Livingstone kina Armstrong kina Wood basi kazikwelikweli sasa Ukienda Mikoa ya Kati ukianza kina Mwaipopo Majina yetu lazima tuyapende jamani tujivunie ila tuwache kuita Watoto Tabu tu na Shida. tuwabadilishe kwa majina Raha au Bahati au Zawadi si Gift. Chuma

    ReplyDelete
  2. wapunguze vitambi!!

    ReplyDelete
  3. Hiyo picha ya wabunge wa Tanzania inaonyesha sehemu ya matatizo tuliyo nayo nchini. Watu wamejisahau kabisa wao ni nani.

    Wimbo wetu wa taifa unapopigwa utaratibu wetu ni kusimama kwa ukakamavu mguu sawa, huku tukiwa tumebana mikono yetu yote kwenye mwili. Hao wabunge wetu WOTE wameweka mikono yao ya kulia juu ya kifua utafikiri wanaimba wimbo wa taifa wa Marekani. Sisemi kwamba wakiwa bungeni wanaimba nyimbo za mataifa ya ng'ambo lakini hii ni aibu!

    ReplyDelete
  4. hivyo vitambi vitacheza mpira kweli. at least some eksesaisi.

    ReplyDelete
  5. uwanja wa shekhe Abri unabidi ufanyiwe kazi kidogo, nyasi ni nzuri lakini back ground imepitwa na wakati!
    hongera kwa ushidi lakini tuwapige mabaoo kwe sekta zote!

    ReplyDelete
  6. Watanzania huwa tuna tabia ya kuiga mengi, hatuanzishi ya kwetu, hivi ni lini watanzania nasi tumekuwa tukiweka mkono kifuani panapoimbwa wimbo wa taifa? pigeni kelele wote lakini ukweli unabaki pale pale hii sio mtindo wetu.

    ReplyDelete
  7. Hivyo vitambi vya hao wabunge hapo juu mh, wanajitafutia matatizo tu uwanjani!

    ReplyDelete
  8. Ni jambo la kusikitisha kuona wabunge ambao ndio watungaji wa sheria zetu hawajui jinsi ya kusimama wimbo wa taifa unapopigwa . Nani kasema watanzania tunaweka mkono kifuani Wimbo wa taifa unapopigwa ? Hii ni kuiga nchi zingine , watanzania tunatakiwa kusima kikakamavu !

    ReplyDelete
  9. jamani vitambi vinatokana nanini?je wakiwa nafasi ya kikwete si watakua wanatembea na wheelchair? huu ni wizi,ulafi tamaa au kundi gani jamani,tunaomba dakika za michezo yao zipunguzwe maana nahisi kama afya si nzuri hivi

    ReplyDelete
  10. Mheshimiwa Spika kama Mtanzania naomba uwafundishe hawa wabunge namna ya kisimama wakati wimbo wa taifa ukiibwa hii ni aibu kwa kwa watunga sheria hawa wa tanzania!!

    ReplyDelete
  11. Jamani waheshimisha ongezeni diet, watch what u eat and exercise

    ReplyDelete
  12. akhaa mie sitaki nichafue hewa umu ndani.yote wadau washasema uo usimamaji wa kif***la cjui wa wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...