Anita Theorill, Rais wa Hans Manneby Memorial Fund akisoma maelezo ya tuzo kabla ya kumkabidhi Dk. Paul Msemwa anayesubiri pembeni huko Sweden mwanzoni mwa wiki hii
Dr. Paul Msemwa akionesha sehemu inapojengwa ukumbi na studio ya kurekodia muziki wakati ujenzi wa jengo la makumbusho na jumba la utamaduni ulipokuwa unaanza mwishoni mwa mwaka 2007

ujenzi wa majengo mapya ya makumbusho na jumba la utamaduni unaendelea vyema na karibu utakamilika, ambapo badala ya kuangalia mambo ya makumbusho ikiwa ni pamoja na vitu vya kihistoria jengo hili litakuwa na ukumbi mkubwa wa kisasa wa maonesho ya sanaa za jukwaani, studio ya kurekodia muziki, internet cafe, mgahawa mkubwa wa kisasa, sehemu za kuchezea watoto na kadhalika. hii yote ni kupachangamsha mahali hapo na kupafanya pawe panatembelewa na wadau wa kila aina sio tu kwa kuanmgalia makumbusho.

Ujenzi wa makumbusho na jumba la utamaduni unafadhiliwa na serikali na nchi ya uswidi na unasimamiwa na mkurugenzi wake Dr. Paul Msemwa ambaye kutokana na ufanisi wake ametunukiwa tuzo ya The foundation of the Hans Manneby’s Memorial Fund for Museum Development, Jumanne iliyopita katika Art Gallery ya Regional museum of Bohus, Uddevalla, Sweden.

Habari za uhakika zinasema wafanyakazi wa makumbusho na jumba la utamaduni wanaandaa mnuso wa kumpongeza Dr. Msemwa siku ya Jumanne hapo hapo mjengoni.
-----------------------------------------------

SWEDEN CONGRATULATES DR. PAUL MSEMWA FOR HANS MANNEBY AWARD

I’m delighted to learn that the first Prize of the Hans Manneby Memorial Fund for Museum Development is being presented to Dr. Paul Msemwa, for his innovative work at Museums in Tanzania.

On Behalf of His Excellency The President of the United Republic of Tanzania I would like to take the opportunity to congratulate Dr. Msemwa for the wonderful work he has exhibited in past years. His contribution at the National Museum and particularly to the House of Culture in Dar es Salaam, Tanzania, is a clear demonstration that he deserves the Prize. He has made us, Tanzanians, proud and we sincerely appreciate his outstanding performance.

Sweden is a country that has the largest presence in Tanzania and in many areas. One important area is the cooperation in Museum Development. The Swedish support on this sector is highly appreciated by the government of Tanzania. It is because of that, I want to compliment you on your decision to present the first Prize to the most devoted person in the field and my fellow Tanzanian, Dr. Paul Msemwa. Indeed, I’m pleased to note that the gesture demonstrates that the future cooperation between our two countries in this and other areas, is both bright and firm.

For you all, who in one way or another, have been instrumental in initiating this Prize in honour of the Late Mr. Hans Manneby, who dedicated his work to take the relations of our two countries to its highest level, I want to say, keep up the good work. We are proud of your entire team and we thank you for taking this nobel decision in stride. Let us all pay tribute to Mr. Hans Manneby and honour his work.
Victoria Mwakasege
CHARGE D’AFFAIRES

EMBASSY OF TANZANIA, SWEDEN

NOTE:The Board of the Foundation Hans Manneby’s Fund for Museum Development is composed by five members. President is Ms Anita Theorell, Stockholm, the Secretary is Ms Elisabet Olofsson, Stockholm.

Other members are Mr Henry Bredekamp, Iziko Museums of Cape Town, South-Africa, Ms Anita Larsson Modin, Västarvet, and Ms Lena Millinger, Malmö.

The Foundation was initiated in 2008 by Samp intercontinental museum network and Swedish ICOM (International Council of Museums). An international museum prize is distributed once a year composed by an amount of money, the amount is set yearly, and a diploma.

The Prize is awarded to a person working in or with the museum sector and can come from or live in any country in the world, working in an innovative way and has inspired or been inspired by international and national collaboration.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ABEL I.NDUNDULUNovember 13, 2009

    HONGERA SANA DR.MSEMWA KWA TUZO NA HESHIMA HIYO.HII INAONESHA NI KWA KIASI GANI ULIVYO MAKINI KATIKA KAZI ZAKO ZA KILA SIKU.HII NI HESHIMA SIO TU KWA MAKUMBUSHO YA TANZANIA BALI KWA TAIFA KWA UJUMLA.NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SHUGHULI ZAKO ZA KILA SIKU.ABEL ISKAL NDUNDULU(AFISA TAWALA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO)

    ReplyDelete
  2. mimi nimefurahi sana kuona kusikia kitu kama hiki na tunafurahi hela imetumika ipaswavyo maana waswidi wange ingizwa mjini lakini busara yako imetumika kutustiri nakufanya kinachostahili,tunataka kusikia mambo kama haya sio kufisadiana.najiuliza hawa watu wanaofanya kazi huko serekalini hawafikirii watoto wajukuu hata kama watakua wanaishi ulaya lakini watakuja kuona hata makaburi ya ndugu au wazazi wao.kwahiyo wafanye kazi zao kwa kuangalia mbele kwa manufaa ya watoto au ndugu zao pamoja na taifa la kesho.maendeleo yanaanzia kwake yeye.sio kuweka hela benki za nje ufisadi mwingine hadi aibu eti mara magari mabovu ya zima moto eti mabati,mara richimond mitambo mibovu hivi hawa watu wanaakili kwanini wasi wafunge maisha watu kama hawa ili ikitokea mtu katapeli serikali adhabu yake iwe hiyo.nawakilisha mdau tzzzz

    ReplyDelete
  3. Mbona ile nyumba iliyoweka mwili wa Marehemu Mwalimu haionekani mpaka hii leo? Tunakuomba Dr. Msemwa uiweke ile nyumba katika kumbukumbu za kitaifa tafadhali.

    ReplyDelete
  4. Mzee Msemwa Upo JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU.Hongera sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...