Joseph Lawrence Ojjiki

Mchezaji wa zamani wa Timu ya Sunderland hivi sasa Simba, Joseph Laurence Ojjiki (77) a.k.a Msalaba, (pichani) amefariki dunia juzi jijini Dar es salaam na kuzikwa Novemba 11, 2009 katika makaburi ya Kinondoni jijini.

Ojjiki aliyezaliwa Juni 02, 1932 alifariki Novemba 08, 2009 baada ya kuugua ghafla.

Mbali na kuichezea timu ya Sunderland pia alikuwa akiichezea timu ya Taifa ya Tanganyika katika michuano ya Gossage siku hizi Challenge Cup katika mika ya 1950's.

Mbali na kulisakata gozi la Ng'ombe pia Ojjiki ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la muziki la Mary Black Birds akiwa na Mzee Ally Sykes.

Marehemu Ojjiki ameacha watoto 3 wajukuu 12 na vitukuu 8.
Blogu hii ya jamii inawapa pole wanafamilia wote, ndugu jamaa na marafiki waliokubwa na Msiba huo mzito.

Kipekee tunaipa pole familia ya Jaji Joseph Sinde Warioba, Familia ya Michael Maluwe na Familia ya Mwombela-Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Oh God..is this Mr Ojikki who worked for the World Bank back in the days? May The Almighty God Rest Your Soul In Eternal Peace. Good hearted man. You will always be remembered. To his family and friends- May God give you strength.
    RIP - Mr Ojikki. AMEN.

    ReplyDelete
  2. RIP mzee Ojjiki.

    ReplyDelete
  3. RIP Big Man we will miss you at St Immaculate Church Upanga... dedicated Man, Down to Earth....You have been received by the Lord for sure..... Bite Makani

    ReplyDelete
  4. May you Rest in Peace Mzee Ojiki. Poleni familia ya Mzee Ojiki.

    ReplyDelete
  5. Nasikitika babu yangu,jirani yangu kuondoka....pole nyingi kwa familia yake na hasa rafiki yangu,mjukuu wake Sarah na Neema.
    mtoto wa (Dokta)
    N.

    ReplyDelete
  6. POLENI SANA FAMILIA YA MZEE OJIKI MUNGU AKULAZE MAHALA PEMA PEPONI UKUTANE NA MKE WAKO MPENDWA NAKUMBUKA ENZI YAK YA MORRIS GREEN COLOR
    MS 6000 OLD IS GOLD rn uk

    ReplyDelete
  7. ooh masikini, mungu amlaze mahali pema peponi mr ojjiki,napenda kutoa pole sana kwa familia ya mr ojjiki wote, waliopo hapo dar na hata nje ya nchi,na pia tumuombee kwa mungu marehemu mzee wetu,apokelewe na bwana mungu wetu, BWANA MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMEN!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...