kaimu katibu wa bunge mh. John Joel a.k.a JJ akiongea wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya manunuzi ya umma yaliyofanyika kwa wah. wabunge wote katika ukumbi wa ubungo plaza jijini dar. wengine toka shoto ni Mh. dk. Didas John masaburi, mwenyekiti wa chuo cha manunuzi na ugavi, waziri mdogo wa fedha mh. Yusuf Omar Mzee, mbunge wa ukonga Mh. Dk. Makongoro Mahanga na afisa wa chuo hicho
Mbunge wa Ukonga Mh. Dk. Makongoro Mahanga akimpatia Da'Asha Baraka laki 4 kama mchango wake alioahidi wakati wa uzinduzi wa albamu ya Twanga Pepeta ya Mwana Dar es salaam. Kulia ni waziri Mdogo wa fedha Mh. Yusuf Omar Mzee
Mbunge wa viti maalumu (CCM, Singida) Mh. Martha Mlata akiimba pamoja na Twanga Pepeta wakati wa hafla ya kumaliza mafunzo ya manunuzi kwa wabunge yaliyoandaliwa na chuo cha manunuzi na ugavi kwenye ukumbi wa ubongo plaza usiku wa kuamkia leo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Laiti mbunge wetu angetusaidia 'initiatives' za kukarabati barabara ya ukonga mombasa - moshi bar, kuliko hii michango ya pepetas!

    ReplyDelete
  2. ugavi ndio nini?

    na mbunge anatoa hela zote hizoo kwa twanga pepeta? Ah? Si wafanye maonyesho watengeneze hela..hizo hela zingeenda kufanya la muhimu zaidi ya hayo sijui maugavi

    ReplyDelete
  3. We ! anony 08:41:00AM
    Tafakari kwanza kabla ya kutoa maoni yako,Sasa kuna kosa gani?mbunge Makongoro Mahanga akitoa mchango wake kama motisha kwa Twanga Pepeta,Jaribu kuzingatia kuwa Mziki na sanaa nyingine ni kitu cha msingi kwa jamii,labda kwa kuwa wewe unachuki zako binafsi.
    Twanga Oyee!! na Mbunge Mahanga hongera sana kwa kuonyesha mfano wa
    kuwaunga mkono Twanga.

    ReplyDelete
  4. Huyu Martha Mlata, anajinadi kwa nyimbo za Injili, sasa wapi na wapi tena na nyimbo za Mziki wa Dansi?

    ReplyDelete
  5. mimi kuna hili jamba ambalo limeibuka hivikaribuni ktk bunge na wabunge kwa ujumla hapo tanzania linanitatiza. binafsi mimi sina tatizo na mbunge au kiongozi wa serikali kujipumzisha/kusherehekea pale anapo jisikia kufanya hivyo kama binadamu tena kwa gharama zake.
    lakini sikuhizi kuna style mpya hapo tanzania ambayo nahisi ni muendelezo wa tabia zoelefu ya watanzania yaani kufanya mambo kwa misimu,sasa ya safari hii ni wabunge kusakata dansi/muziki kila wanapo jumuika kufanya mambo yanayohusisha shughuli zao za kiofisi. sasa swali ni hili HII INA FAIDA GANI KWA TAIFA?
    mimi sijawahi kuona hili ktk nchi yoyote duniani tofauti na tanzania!! nafahamu kuwa mataifa karibia yote yana maadhimisho ya sherehe zao zinazo kumbusha mambo kadhaa ya kitaifa/yenye kumbukumbu ya kijamii na huwa kunaujumbe unao ambatana na kumbukumbu hiyo kwa jamii.
    anyway mimi sifahamu tija ya hizi sherehe na zinagharimiwa na nani hata kama sio fedha nyingi inayotumika lakini sioni mantiki yake zaidi ya kunikera tu binafsi. kama ni swala la dansi nenda night club,au wabunge jialikeni kama marafiki na sio kama wabunge mfanye sherehe ya kirafiki na mtumbuizwe na dansi mcheze mkate kiu na kuondoa stress kama lengo ni kuburududika.
    lakini inakera sana pale inapokuwa pin pointed kuwa WABUNGE wanasakata dansi,wabunge wanashiki ktk show ya mavazi,hii nikuonyesha tu kuwa wabunge sasa mnapoteza dira na mwelekeo wa title ya MBUNGE. kama ni kundi fulani limekualika kama kiongozi wa siasa ktk jamii na wakakuomba ufungue mziki hilo ni jambo jingine na sina shida nalo.lakini hili la kualika bendi kuja kuungurumisha ktk mijumuiko yenu linanifanya kuwa na walakini na haya mambo ya misimu hadi bungeni. JUST TAKE TIME TO THINK ABOUT THAT! najua ukiwa ndani ya uwanja huoni tofauti kati ya mchezaji huyu na yule lakini ukiwa nje unaona,na mimi niko nje na naona hili IS NOT OK!!!!hata kama mtabisha waheshimiwa wabungu!!!

    ReplyDelete
  6. NINI MAANA YA MANUNUZI NA UGAMVI?????MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  7. watu wengine mnalalamika tu, hamchoki? we hujuwi kwamba hiyo ni ada ya kuimbwa na twanga pepeta? unafikiri kampeni mchezo.

    ReplyDelete
  8. purchasing &supplies

    nyie wa-bongo sijui niwaiteje "eti"mliosahau kiswahili na utamaduni wa kiswahili baada tu kufika nje-kubeba box....

    jaman uwa sielewi ni ulimbukeni uliotukuka kiasi ichi mtu umezaliwa Tz ukakulia uku nk then ulipoenda ukijilipua nje "ghafla"umesahau bongo

    hahaaa

    ReplyDelete
  9. bwana sio kuwa tumesahau kiswahili ila misamiati migumu. Si unaona kaandika kwa kiswahili kabisa wewe kumlaumu ya nini? hata mimi nataka kujua maana ya UGAVI.

    purchasing & supply? What do you mean? Ndio umeniacha mbali zaidi. Tuelimishane polepole tu. Najua hata wewe kuna ingawaje upo hapo Tanzania lakini kuna misamiati mingine ya kiswahili hujui. Unafahamu maana ya nukunishi na kichakato wewe? teh teh teh teh

    ReplyDelete
  10. sio kwamba watu wanajidai hawajui kiswahili la hasha kuna maneno ya kiswahili hata huko bongo kuna watu hawayajui manake yanaibuka kila siku kwa mfano mchakato na hakika kuna watu wengi hawajui kulitumia ugavi ndo umeniacha heathrow!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...