ajali ya gari la mashindano lililoua watazamaji morogoro majuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. SASA WATAKUJA KULILIA LAMBI LAMBI KWA RAISI WAKATI ULIKUA NI UJINGA WAO:
    MASWALA MENGINE SIYO LAZIMA MTU AENDE SHULE:
    BONGO BAAAAAADO; NASIRUDI NG´O.

    ReplyDelete
  2. Kwanza namshukuru sana aliyeweka clip hii maana inaonyesha uhalisia wa atukio na inaonyesha ni nani wa kulaumiwa katika ajali hii;
    1.Waandaaji wa mashindano
    2.Wananchi (ukaaji wao bila kujali kwamba kuna lolote baya linaweza kutokea na hii ndo sehemu mabay zaidi iliyoleta tatizo.Hebu angalia ukaribu wa barabarani ,kona na mkao wa wananchi katika barabara hiyo.

    hatuna tahadhari kwa nini ? elimisha wananchi kwa yaliyotokea.Clip ni nzuri kwa kujifunza yaliyotokea

    ReplyDelete
  3. hii ajali ni uzembe lakini kwa kuwa bongo ni tambarare hakuna kiongozi atakaefunguliwa mashtaka,raisi alitakiwa awawajibishe watu wake ni common sense tu kwamba mashindano kama hayo watu walitakiwa wakae mbali kidogo na barabara hasa kwenye kona..

    ReplyDelete
  4. Hili ni zaidi ya fundisho.
    Mungu awalaze pema marehemu wote na awape afya na wapone haraka majeruhi wote.

    ReplyDelete
  5. huzuni iliyoje watu wale wasio na hatia wametangulia mbele ya haki.mungu awalaze pema peponi.napia ningependa kuwashauri watanzania wenzangu popote pale kuwa wasizisogelee gari kwa karibu namna ile maana inaonekana kana kwamba wanapisha gari kwa karibu kama vile wanaruka kamba..hatari sana

    ReplyDelete
  6. good thing to post this man but put a sign kwamba its real and shows some dead bodies, anyway its so sad even after accidents still people wanabaki katika eneo hatari na kusubiri magari mengine!

    ReplyDelete
  7. I am stuck with Words, I don't know how to react, BE ANGRY, JUST CONTEMPLATING.

    IT JUST MAKE ME ANGRLILY SAD, hakuna usalama, hakuna medics, hakuna warnings, hakuna chochote mpaka kutokea kwa ajali,

    You can hear people contemplating the imminent of accident at any time t, but why wasn't this picked up by race officials, DO THEY HAVE THEM?? I really dont know ?

    Safety wasn't the issue at the first place,

    I hate to throw blames now, someone must take a full blame, and PUNISHMENT, IT IS PURE NEGLIGENCE

    A GREATNESS OF A NATION, IS JUDGED BY HOW IT TREATS ITS VULNERABLES, IN THIS CASE, IT AFFIRM MY THOUGHTS. I GUESS THIS IS WHAT, THEY ARE SAYING QUIETLY AND OPENLY WACHE WAFE NI UZEMBE WAO? NOTHING WILL BE DONE!!

    I am not a race driver and I have never been one, they should have the race officials, they should for certain thats a dangerous corner, near a village, and should know really well, the spectators will be gathering on that corner to catch a glimpse, to them was a perfect spot, and never accustomed to racing, and never subjected to safety before, YOU CANNOT BLAME THEM, BUT SOMEONE ELSE WHO KNOWS THE IN AND OUT ABOUT THE CAR RACING.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  8. Inatisha...tahadhari kubwa zinatakiwa zichukuliwe ku-host michezo kama hii.

    ReplyDelete
  9. lawama ni kwa serikali na waandaaji. hapo naona wengi waliyojeruhiwa ni watoto. kwa nini serikali na waandaji wasiweke ulizi kwenye maeneo haya? kwa nini hakuna uzio wa kuashiria mwisho wa watazamaji? je kwa nini waandaji wa mashindano/serikali wasiweke vituo vya huduma ya kwanza na ambulance kwa umbali furani ambapo ingekuwa rahisi kuwafikia na kuwasifirisha majeruhi na waliokufa. ajali ktk mbio kama hizi always zinachance ya kutokea, hata kama hakuna watazamaji lakini madereva wa mbio za magari wanaweza kupata ajali. je walijiandaa vipi kama hilo lingetokea. mwisho kwa nini serikali mpaka sasa imekaa kimya bila kutoa statements yoyote kama vile hakuna kilichotokea? Nafikiri ni wakati watanzania tuamke na tuanze kuwa outrage na vitu kama hizi, hata kama kuanza kusue makapuni pamoja na serikali. mengi yanatokea nasi hukaa kimya bila mabadiliko yoyote kufanywa. Mnakumbuka watoto walivyokufa kwenye disco toto kwa sababu ya msongamano na ukosefu wa hewa, mabweni ya shule kuungua, ajali zinazoendelea barabarani.Hatusikia serikali kuchukua hatua yoyote kuhakikisha vitu kama hivi havitokee tena

    ReplyDelete
  10. WATUNGA SHERIA MKO WAPI KAZI KUKAA BUNGENI MNALALA NA KUJAMBA TU! VITU KAMA HIVI NI AIBU KUBWA WANACHI WANAUWAWA BILA SABABU!!INASIKITISHA SANA !

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli tunatakiwa kuwafundisha wanavijiji jinsi ya kuokoa maisha ya watu.CPR course tu.Na ni rais kummfundisha watu.kwani nimeona hapo baada ya kumpulizia hewa mdomoni na kupump kwenye kifua kama ili kurudisha mapigo ya moyo.Tufundishe vijana wa shule za msini na wazee ktika vijiji vyetu.Ukiangalia hii video,utashangaa hakuna first aid hapo.sio tu kuwa na vifaa ni kuweza kuzuia damu hisitoke kujua kama wanapumua ,na kama hawapumuhi,KUANZA KUTOA CPR ILI AWEZE KUPUMUA HATA KAMA KUMIVIPI?MUNGU MKUBWA ANAFANYA MAAJABU YAKE.

    ReplyDelete
  12. Tukio hili linasikitisha sana. Mashindano kama haya hayakutakiwa kupewa kibali kwa sababu hakukuwa na maandalizi yeyote ya kuhakiki usalama. Mtoa kibali na waandaaji inabidi wawajibishwe. Je ni UZEMBE au KUTOJALI kwa waandaaji na watoa kibali? Kuhakikisha usalama wa watu ni gharama ndogo sana ya muda na fedha ukilinganisha na UPOTEVU uliotokea. Watoto hawa wamenyimwa HAKI YA KUISHI kwa sababu ya uzembe. Kwako kiongozi wetu unayesoma hii blogu: Je, utalifumbia macho suala hili kwa sababu sio mtoto wako, jirani yako au mtu unayemfahamu? Hatua utakayoichukua itadhibitisha wito wako wa kuwatumikia wananchi - FANYA JAMBO MOJA ZURI NA WENGINE WATAFUATA NYAYO ZAKO. Pole kwa wote waliofiwa.

    ReplyDelete
  13. Jamani poleni sana watanzania wenzangu.ila moja tu naomba waandaaji wa hayo mashindano feki wawe wanakuwa responsible make hakuna hata watu waliokuwa trained kuokoa majeruhi. kuna watu kibao wanapoteza uhai kutokana na uokoaji.hata ambulance hakuna je hayo mashindano yanataka nini kwa watu ambao hawajaelimishwa.pili nilikuwepo tanga wakati wa mashindano nadhani kati ya 2005 au 06. inasikitisha wabongo wanavyoizunguka barabara kwenye kona kama hiyo hiyo jamani mtu anasimama kwenye kingo ya kona mbele ya gari la mashindano.its a shame kwani haihitaji hada elimu ya vidudu kujua kama gari iko na asilimia kubwa ya kuserereka.sina jinsi ninavyoweza toa picha nilivyoiona kwani siku nzima nilibaki kusimulia na nilijua iko siku yatatokea.MUNGU WALAZE MAHALI PEMA WALIOPOTYEZA MAISHA

    ReplyDelete
  14. sidhani kama madereva wana makosa, mwenye kamera kawaambia watu watoke kwenye kona mara 3 bado hawasikii
    poleni wafiwa.

    ReplyDelete
  15. OMG! very graphic, left me in tears. No CPR, first AID kit could have save a life or two.
    May our lord rest their souls.

    ReplyDelete
  16. EVEN ME I COULD STAND THERE WHEN I WAS YOUNG. I REMEMBER WHEN LIVING IN MY VILLAGE CALLED CHITANDI, NEWALA THOSE ALL GOLDEN DAYS THERE WERE THESE BIG TRUCKS(COMMER AND MERCEDES BENZ) COMING TO OUR VILLAGE TO COLLECT KOROSHO/CASHNUTS, THEN WHEN THEIR WAY BACK TO NEWALA TOWN THEY USED TO GET SOME PROBLEMS WHEN CROSSING THE HILLS TO NEWALA SOME OF THEM OVERTURNED SO WE USED TO RUN FROM THE VILLAGE TO THE HILLS ALMOST 5 MILES TO WATCH THEM AND HELPING TO PULL THEM OUT IN A VERY DANGEROUS WAY. TODAY I THINK AND REALISE THAT WE WERE DOING HATARI JOB THEN WITH IGNORANCE, PEOPLE THEY SHOULD STAY FAR AWAY FROM THE ROAD AS ANYTHING COULD HAPPEN AS IT DID

    ReplyDelete
  17. HIVI JAMANI NYUMBANI KUNA MATATIZO GANI?ROHO INANIUMA SANA KUONA THAMANI YA MAISHA YA BINADAMU IKICHUKULIWA KAMA MNYAMA,HAYA MAGARI YA MASHINDANO YANA FAIDA GANI ZAIDI YA MAISHA YA BINADAMU ,INA MAANA HAKUNA HATA WATU WA USALAMA AMBAO WANAHITAJIKA KUANGALIA BARABARA JAMANI ,ANGALIA AJALI IMETOKEA MAGARI MENGINE HAYANA TAARIFA YANAPITA TU WAKATI ILITAKIWA MASHINDANO YASIMAME VINGEWEZA KUTOKEA VIFO VINGINE PALE NAUMIA ROHO ,SERIKARI UMEKALIA KULA PESA MAISHA YA WATU WANATEKETEA TU INASIKITISHA

    ReplyDelete
  18. ni huzuni kwa kweli,lakini kwa maoni au muono wangu ilikuwa haina haja ya kuweka mashindano ya magari hapa bongo sababu nchi bado ipo nyuma kimaendeleo isitoshe hakuna tahadhari inayochukuliwa,wadau angalieni hiyo video jinsi gani hizo gari zinavyokimbia kwa kasi halafu watu walivyojipanga hiyo inaonesha dhahiri kwamba ipo siku hizo gari zitavamia watu it is sad to watch,watanzania kuna mambo nahisi tunaweza kuyaepuka.

    ReplyDelete
  19. michuzi hapo nimesikia kuna mtu alikuwa anatoa onyo watu waondoke kwenye kona lakin wakakaidi hiyo amri halali ndio mauti yakawakuta,na huyu mtu aliyekua anatoa onyo alishaanza kuona.Natoa pole kwa wafiwa wote,mungu awaweke roho zao mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  20. Hilo ni kosa la makusudi na la kudharau USALAMA WA RAIA kwenye mashindano ya magari.YAANI HIYO NUMBER YA WATU WALIOKUFA NA WALIOJERUHIWA NA MOJA YA HAYO MAGARI YA MASHINDANO STILL MAGARI MENGINE YANAENDELEA KUPITA KANA KWAMBA HAKUNA KILICHOTOKEA!!!!!????? HIVI HAWA JAMAA WANADHANI WAMEGONGA MBUZI WA MAMA RODA???
    HIVI NDIVYO MAISHA YA MTANZANIA YASIVYO THAMINIWA!!!!! USALAMA WA MTANZANIA HAUTHAMINIWI!!!??. KWANINI BARABARA ZA MASHINDANO YA MAGARI ZIPITE SEHEMU ZA RAIA?? KWANINI RAIA WARUHUSIWE KUSIMAMA AROUND HIZO BARABARA????
    HIVI HICHO CHAMA CHA MASHINDANO YA MAGARI KINAJUA NINI KUHUSU USALAMA BARABARANI??
    HIVI SERIKALI YETU INAUGONJWA GANI?? KWANINI INARUHUSU MICHEZO HIYO AMBAYO SI SALAMA KWA RAIA KUFANYIKA???? HIVI HII NDO ADHABU YA UMASIKINI?? HIVI NI LINI TUTAPATA VIONGOZI WANAOPENDA NA WANAOWAJALI WANANCHI WAO????
    Mungu Ibariki Tanzania(MITA)

    ReplyDelete
  21. HAYA MASHINDANO LAZIMA YAFUNGWE MPAKA ITAKAPOKUWA SALAMA KWA RAIAM
    Mdau

    ReplyDelete
  22. WAZIRI WA MICHEZO INABIDI AWAJIBIKE TENA NAMAANISHA AWAJIBIKE
    RAIA

    ReplyDelete
  23. jamani kaka michuzi, watoto wadogo jamani.. maskini.. poleni wafiwa, lakini kwanini na sisi wazazi tunaacha watoto wadogo namna hiyo kwenda kuangalia mashindano ya magar na kuwaacha wasimame barabarani kiasi hicho jamani.. poor kids.. R.I.P all ..

    ReplyDelete
  24. It was horrible accident, inasikitisha sana, tuweni makini jamani.
    Poleni kwa wafiwa wote, na walio hai katika waliopata ajali hii. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema. Amiyn.

    ReplyDelete
  25. POOR SPECTATORS!! VERY SAD ...SHOULD THEY DIE THAT WAY, REALLY??

    ReplyDelete
  26. Duh!! nimeshindwa kuimaliza kuingalia video hii yaani imenisikitisha hadi machozi yamenitoka,nawaombea Mungu marehemu wote makaazi mema peponi na Mungu awape subira wafiwa wote katika mtihani mzito kama huu.

    ReplyDelete
  27. Hii ni ajali ya kuhuzunisha sana,ila kuna udhaifu na uzembe mkumbwa umejionyesha,waandaaji kwa kushirikiana na wanausalama walitakiwa wahakikishe kuwa
    1.katika kila kijiji au mji magari yanapopita kuwe na usimamizi wa kuwaoongoza watu wakae sehemu za usalama
    2.wahakikishe kuwepo na upatikanaji wa huduma ya kwanza,ingesaidia si tu kwa raia hata kwa hao madereva pindi watakapopata ajali

    ReplyDelete
  28. Ргг ni uzembe mkubwa sana ambao unasababisha maafa kama haya lawama za kwanza zinatakiwa kwenda kwa Organizer ambaye anafanya mashindano bila kutoa elimu ya kutosha kwa wanakijiji hebu angalia jinsi watu walivyopanga magari pembeni ya barabara na kuocha nafasi ndogo hasa kwenye kona!!, magari pikipiki, baiskeli na watu hivi unawezaje kukimbia Ajali ukiwa umezungukwa na vitu vyote hivyo? Shame!!! ni vifo ambavyo vinaweza epukika

    ReplyDelete
  29. jamani jamani jamani tanzania na afrika kwa ujumla nini hii mnafanya kwanini mnaruhusu mashindano pasipo utafiti wa ubora unaohitajika?barabara haziwekwi hata vizuia ajali kwa watazamaji/?ona hapo kamasikosei masikini watoto ndio wengi ktk walifariki maskini mtoto huyo mguu umekatika vibaya sana warataibu wahusike juu yahilo.imeniuma sana maskini watoto dah poleni wazazi wenzangu mungu awe nanyi ktk kipindi hichi kigumu.poleni sanamdau greece

    ReplyDelete
  30. kwa maoini juu ya ajai iliyotokea morogoro safari rally, kwa mujibu wa hii ajali ilivotokea, inaonekanika kwanza hawa maorganiser wame neglect health and safety, pili inekuwa uzuri kama serekali ingewaweka maorganiser accountable na matukio kama haya, na zaidi michezo kama hii ingezuiwa mpaka masuala ya health and safety yawe appreciaed na kupewa kipao mbele hapo ndo tuweze kuwa namichezo kama hii, la siivyo hizi sfari reli zitandelea kutoa roho watu....

    ReplyDelete
  31. Inasikitisha! yaani hata sijui nianzie wapi! Kwani hao watoa vibali vya mashindano,huwa hawaangalii usalama wa watazamaji,umbali kati ya watizamaji na magari yanapopita,hata kama ni vijijini.Jamani inabidi hili swala inabidi liangaliwe upya.Poleni sana na msiba huu.

    ReplyDelete
  32. Bro. Mithupu inasikitisha sana kwa sisi watanzania tusivyojali maisha yetu. Sehemu zenye hatari huwa ndo tunakimbilia! Kumbuka mabomu ya mbagala yalivyolipuka badala watu kukimbia kunusuru maisha yao badala yake walikimbilia milipuko ilipotokea!
    Sasa hapo katika mashindano ya magari hizi sio sehemu za watu kusimama na kusubiria kuona magari ya mashindano. Ni hatari tupu na cha kuchangaza baada ya ajali kutokea watu waliendelea kukaa endo lile lile la hatari! Ni hali ya kutisha hii na wala simlaumu dereva wa gali la mashindano ninalaumu viongozi waandaaji na watazamaji nafikiri kungekuwa na maeneo maalum yaliyotengwa kwa watazamaji sio kusimama sehemu yoyote!
    Inasikitisha sana watu kupoteza maisha kiholela namna hii. Natoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao na majeruhi wote Mwenyezi Mungu awarehemu.
    MDAU USA

    ReplyDelete
  33. watayarishaji wanachukua tahadhari gani kwa watazamaji, je wadhamini watawalipa hao waathirika?

    ReplyDelete
  34. It's very sad.

    ReplyDelete
  35. My two centsDecember 21, 2009

    Michuzi please be sure to provide this evidence to the appropriate authorities! Thank goodness we have technology these days. May god rest these peoples' souls.

    ReplyDelete
  36. yaani inasikitisha sana kwa jinsi ajari ilivyotokea,ni uzembe tuu wa waandaaji ambao hawachukui tahadhari yeyote kwa usalama wa wananchi,lazima hapa insurance na kampuni za hawa waaandaaji zilipe mamilioni kufidia waliokufa na walioumia..wananchi wasidanganywe kwa visenti vidogo lazima walipwe mamilioni na hawa waandaaji na makampuni yao ya insurance ,naomba kuwa lawyer wao tuu ili kukomesha uzembe kama huu,yaani wanaandaa na hakuna hata anayejua kama kuna ajari imetokea wanaohangaika ni wengine kabisa,nina uhakika kungekuwa na tahadhari za usalama kuna wengine wangepona kabisa,lazima hawa wakomeshwe maana bongo watu wanafanya makosa bila consequences zozote

    ReplyDelete
  37. This is so sad. So sad jamani watoto wamekufa wengi.
    Kuna mtu alisema tokeni kwenye Kona I guess no one kasikiliza.

    Mashindano kama haya yanatakiwa kuwe na vyombo vya usalama (police, fire, paramedics, first aid kits).
    Poleni sana jamani.

    ReplyDelete
  38. Kaka michuzi ajali mbaya sana machozi yamenitoka, poleni sana wafiwa

    ReplyDelete
  39. TOOOOO BAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAD

    ReplyDelete
  40. Kaka Michuzi hii ajali ilikuwa mbaya na wale waliowapoteza wapendwa wao nawapa pole, kwa waandaaji na sisi watazamaji nafikiri ni wakati umefika kulifikiria suala la usalama zaidi kwenye michezo maana hata hao madereva waliokufa Zanzibar walikuwa wakijaribu kuokoa maisha ya watazamaji walio kuwa wamesima ndani ya barabara, kwanini watu wasimame umbali kidogo kutoka kwenye barabara na pia labda kuwe na uzio wa kuonyesha mwisho wa sehemu salama kusimama kuangalia magari. Nampongeza sana aliyekuwa anapiga hiyo video maana toka mwanzo nilimsikia akiwaonya hao walio kwenye corner, na pia hakuachia camera mpaka tukio lilipokamilika.

    Mdau
    Mdee

    ReplyDelete
  41. Ni uzembe, toka kwa waandaaji mashindano,watazamaji,ile sehemu ya kona inaonekana jinsi ilivyo hatari na magari yanakuja kwa kasi,ni wazi kwenye kona ni rahisi sana dreva kukosea stepu kwa spidi aliyonayo na gari kuserereka; kwani trafiki siku hiyo hawakuhisishwa?angalau wangewekwa sehemu hatari za kona k.m hizo na kuhimiza watu wakae mbali kabisa na barabara;lakini ndo hivyo mpaka yatokee ndo linakuwa fundisho.

    ReplyDelete
  42. USALAMA BARABARANI

    NI VEMA SERIKALI ISHINIKIZWE ILI IJUE KUWA INA WAJIBU WA KUHAKIKISHA TARATIBU ZA USALAMA ZINAANDALIWA NA WAHUSIKA, KWA KUWATUMIA TRAFIC WA USALAMA BARABARANI, ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOONEKANA WAZI ZINAWEZA KUTOKEA.

    ReplyDelete
  43. Poleni sana wafiwa makosa ni ya waandaaji hao watoto na vijana wasingeweza kufanya risk Assesment ya kutosha kujua ni sehemu gani ni hatari,na ukiangalia kwa makini upande walio wao ni salma zaidi kuliko upande mwingine wa barabara.

    waandaaji walitakiwa waweke utepe wa njano kuonyesha ni umbali gani wananchi wanatakiwa kukaa hasa kwenye kona kama hiyo iliyotokea ajali.

    Waziri wa michezo na hakika anafahamu hilo na anawajibika kuhakikisha kabla mashindano hayajaanza usalama wa kutosha wa wananchi unachukulia.

    Ni uzembe wa kutokutoa elimu ya kutosha kuhusu hatari ya kusimama kwenye kona kama hiyo na kutokuweka alama yoyote kuhakikisha wananchi wanakaa mbali na eneo hilo.

    Mjusi

    ReplyDelete
  44. kaka hapo watu wabishi ukiwambia unaonekana mjinga lakin hii ingewekwa kwenye matangazo ya kila kona ili watu waone na wajifunze jambo moja muhimu katika maisha yao,kusema kweli inauma sana poleni sana waathirika.hapo hamna kesi yoyote.

    ReplyDelete
  45. Sidhani kama ni suala la kuwalaumu wahanga kwa ujinga wao - bali waandaaji wa mashindano walitakiwa kuweka mazingara ya afya na usalama wa watu na wanyama wakati wote. Under no circumstances should the victims be held responsible and further, I think the images are too distressing to be put in the public domain in thi sway. WMwenyezi Mungu awarehemu waliofariki na awaafu waliojeruhiwa. Kilo changu ni kwa waandaaji wa mashindano na wahakiki wao.

    ReplyDelete
  46. Dj Spark MassiveDecember 21, 2009

    I'm real shocked, lost words and i don't know where to start, this clip left me in tears i can't imagine how poorly the whole thing was been arranged, no warning signs, no race wardens no traffic police no barriers. It was as if planned to happen that way. I'm very deeply saddened by they are loss. My thought and prayers goes to their families and beloved ones, may Almighty God give you courage to overcome this grief

    ReplyDelete
  47. Aaaaaaaaastaghafirulai maulana wa bakwata!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  48. Kwa Tanzania ninayoijua mimi, ajali hii sio fundisho hata kidogo, Zimeshawahi tokea ajali nyingi kwa uzembe wa watu na hakuna hatua inayochukuliwa kwa watu wanasababisha uzembe unagharimu maisha ya watu. Tujiulize ajali ya MV Bukoba, Ajali ya treni Dodoma, nani kawajibishwa kwa uzembe alioufanya?. Ajali ni nyingi sana mfano mwaka 2004 peke yake, zilitokea ajali 17,039 na ziligharimu maisha ya watanzania 2,366 na kuacha majeruhi 17,231. Kuna uzembe mwingi sana katika vyombo vya usafiri hasa mabasi. Hivi nyie watu wa Serikali hamuoni uchungu kuona Uhai wa Watanzania zaidi ya 2000 unapotea kwa uzembe kila mwaka? naona kichefuchefu kulitaja Jeshi la Polisi kwani limeoza kabisa na linanuka. Viongozi wetu mmekosa moyo wa uzalendo wa kuipenda Tanzania na watu wake. kila mtu anajali maisha yake na familiya yake. Mungu atawahukumu. by Benjamin from Germany

    ReplyDelete
  49. Hili ni fundisho kubwa kwa kweli, NA HILI NI KOSA LA:
    1. WANDAAJI (KWA KUTOHAKIKISHA RAIA MABARABARANI WANA USALAMA WA KUTOSHA),
    2.WALIOTOA VIBALI (KWA KUTOSISITIZA KWA WAANDAAJI NA KUHAKIKISHA KUHUSU USALAMA KWA RAIA),
    3.MADEREVA WASHIRIKI WOTE NA WADHAMINI WA HAYA MASHINDANO(KWA KUTOHAKIKISHA MASUALA YA USALAMA KWA RAIA BARABARANI YAMEWEKEWA KIPAUMBELE NA WAANDAAJI).

    Hapa inatakiwa hawa wanasheria wetu waliojaa mitaani waungane na wafiwa na kufungua mashitaka (wa sue) dhidi ya hao wote nilowataja hapo juu..... kwanza hapa kuna hela nyingi na pia itasaidia kuwapa fundisho permanent (coz hela zitawatoka) hivyo next time watakuwa makini...

    Mwisho poleni sana wafiwa wote!

    ReplyDelete
  50. unayesema Bongo bado na hurudi ng'o unatakiwa u-click akilini that sentence b4 posting it! anyway I used to think the same too.
    Its true nchi yetu is still in Dark ages ila kama umeshafungua upeo wa mind zako unawasaidiaje wenzako wasiojua hilo; lETS BE OF VALUES not just sitting down making comment za ajabu------- Ajali ni mbaya sana na inasikitisha mno, Poleni wafiwa ndugu jamaa na marafiki. Have confort that wote ni wapitaji katika dunia hii.

    ReplyDelete
  51. Anonymous wa Sun Dec 20, 05:53:00 PM. Its true nchi yetu is still in Dark ages ila kama umeshafungua upeo wa mind zako unawasaidiaje wenzako wasiojua hilo; lETS BE OF VALUES not just sitting down making comment za ajabu------- Ajali ni mbaya sana na inasikitisha mno, Poleni wafiwa ndugu jamaa na marafiki. Have confort that wote ni wapitaji katika dunia hii.
    wale walioumia Get well soon!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...