Naibu Balozi wa Tanzania UK Mh. Chabaka Faraji Kilumanga akiongea wakati wa hafla hiyo
Mwenyekiti wa ATWID Suzana Mzee akihutubia kwenye hafla hiyo
Mbunge wa Viti Maalum Mh. Martha Mlata akitoa nasaha zake
Mbunge wa Viti Maalum Mh. Martha Mlata akitoa mchango wake wa Khanga kwa mwenyekiti wa ATWID Suzan Mzee
Naibu Balozi wa Tanzania UK Mh. Chabaka Faraji Kilumanga na Mh. Martha Mlata katika picha ya pamoja na wana ATWID
Hii ni siku ya fundraising ya Asociation of Tanzanian Women in Diaspora (ATWID) iliyofanyika tarehe 19/12/2009 mjini Reading. Pia ilikuwa sherehe ya kutimiza mwaka mmoja tangu ATWID kuzinduliwa.
Mgeni rasmi alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza bwana Chabaka Faraji Kilumanga. Pia alikuwepo Mbunge wa viti maalum Mh. Martha Mlata.
Kulikuwepo na ngoma za asili zilizochezwa na wana ATWID pamoja na shoo ya watoto.Mwenyekiti wa ATWID Susan Mzee alitoa nasaha zake na kuwashukuru wote waliohudhuria kwa muda wao na michango yao. Zaidi ya paundi elfu mbili (£2000) zilipatikana katika hafla hiyo kwa ajili ya kutunisha mfuko wa ATWID.

Picha na habari zaidi nenda

www.atwid.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mimi ni mwanaume lakini nataka nijiunge na hiki chama ili nipata social networking ya hawa kina mama. Je nitaruhusiwa kujiunga?

    ReplyDelete
  2. hawa ni ma opportunist hawana chochote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...