Uongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi unawataarifu wa-Tanzania waishio hapa mjini New Delhi na majimbo jirani kuwa kutakuwa na Bonanza la aina yake litakalofanyika Jumatano siku ya TISA DESEMBA (Desemba 9, 2009) katika kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika.

Katika Bonanza hilo kutakuwepo na mashindano ya michezo mbalimbali , *Mchezo wa Mpira wa Miguu
*Mchezo wa Mpira wa Wavu.
*Mchezo wa Kuvuta Kamba ( Tag War)
*Mchezo wa Kukimbia mita 100.
*Mchezo wa KIPOFU.
*Kukimbia na Ndimu.
*Mashindano ya kula na kunywa.
*Kuogolea na kusakata Rumba.


Bonanza hilo linatarajiwa kufanyika Nyumbani kwa Balozi kuanzia saa TATU KAMILI Asubuhi. Katika Anuani ifuatayo:

Tanzania High Commissioner Residence,
F-9 Radhey Mohan Drive,
Mehrauli, New Delhi.

Washiriki wa michezo wanaombwa watoe taarifa mapema kwa kiongozi wa michezo na burudani BENARD RUTA kwa ajili ya kupanga timu:
PHONE No- 9910232724.
na Msaidizi wake
CHANIA MUSTAFA:Phone :9910463532
au Makamu wa Mwenyekiti
JANE TWILUMBA ,Phone No: 9650308572.


WOOOTE MNAKARIBISHWA.
Mwenyekiti TASA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kambo's jana nimeshuhudia goba ham ikilazwa tano bila majibu... Je, malengo ya ligi kuu yapo kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...