Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hotuba ya Mwl Nyerere kuhusu Rushwa.

    Kaka Issa Michuzi asante angalau kwa kuweka moja ya ''clips'' za rais wetu wa kwanza. ukijaribu kuisikiliza kwa makini (na hata hotuba zake nyingine) utagundua kuwa..alikuwa mmoja wa viongozi wachache sana duniani alikuwa na ''UWEZO WA KUTHUBUTU'' kutekeleza mambo mengi aliyosema. Nikijaribu kumchambua Nyerere na viongozi waliofuata..kweli ninaona tofauti kubwa sana!! nakubali kuwa Nyerere sio kwamba alifanikiwa ktk kila kitu ila alijitahidi katika mengi ya uongozi wake... Alijitahidi kuwa mkweli ktk yate aliyosema (KUTEKELEZA KWA VITENDO)- tofauti na sasa. ingawa alikuwa mwanasiasa ila kweli aliijali nchi yake tofauti na viongozi wa sasa!!!
    Sasa hivi kinachofanyika ni ''bora liende'' na ndio maana tunaona kila kiongozi anafanya lwake...
    Hivi wadau embu tujaribu kufanya tathmini ndogo isiyohitaji uwe na digirii..ukimchambua waziri mmoja mmoja..halafu angalia tangu amechaguliwa ni nini ''ameifanyia nchi yake kupitia dhamana aliyopewa??..nathubutu kusema kama wapo ni wachache saaaaana!! sasahivi kila kiongozi anaangalia ni wapi pa kuchota palipobaki!!
    Huu ushikaji ndio unaotutesa tanzania!!nasikia sasahivi innandaliwa sera nyingine ''kwa vijana'' sijui baada ya kuona sera ya ''maisha bora kwa kila mtanzania kupitia ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya'' kuonesha kuwa imefeli!!! nadhani hii sera ilikuwa na maana ifuatayo.. ni maisha bora kwa kila kiongozi kupitia ufisadi kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya...

    Serikali ya awamu ya kwanza ilimaanisha ilichosema kwa vitendo... serikali ya sasa.. ni porojo tuu!!!

    Yetu macho hapo mwakani..ila wadau kweli tunahitaji mabadiliko.
    I AM STILL HAVING A DREAM, THAT ONE DAY, OUR GOOD COUNTRY TANZANIA WILL BE LEAD BY TRULY COMPETENT LEADERS!!
    I AM STILL HAVING A DREAM THAT, LIKE WHAT HAPPENED TO OUR NEIGHBOUR, KENYA, WILL ALSO HAPPEN IN TANZANIA..THAT THE ''CCM'' THAT IS SEEN TODAY WILL NEVER BE SEEN ANYMORE!!
    I STILL HAVE A DREAM THAT ONE TRUE COMPETENT AND COMMITTED LEADERS WILL RISE AND LEAD US TO GREEN PASTURES.

    Tafakari...

    Mungu ibariki nchi yangu Tanzania

    DJ

    ReplyDelete
  2. Enzi za Mwalimu, mtu ulijisikia uko nyumbani kikweli "you know what am saying?",yaani ulikuwa unajivunia ni nchi yako,tofauti ya maisha haikuwa kubwa kama ilivyo sasa,enzi za Mwl, nchi ilikuwa ni kweli ya walalahoi,mkulima alitambulika na alijivunia ukulima wake,mi nasema,transition toka Nyerere ingekwenda moja kwa moja kwa JK labda mambo yasingekuwa mabaya hivi;maana JK anajitahidi kusema la ukweli,lakini ni ngumu kusafisha nchi wakati kaikuta inanuka rushwa;atafanya maajabu yepi? anaowategemea wamsaidie serikalini ndo hao; kuna wachache sana wazalendo,na serikali haiendeshwi na mtu mmoja.

    ReplyDelete
  3. Thank you Michuzi for the clip, naomba uwe unazitoa hizo now and then... maisha ya mwalimu ni soma tosha la uongozi bora Africa na dunia kwa ujumla.
    Michuzi nitakuandikia e mail soon kuhusu my ideas...
    unisaidie kwa upande wa nyumbani..
    He was a hero!
    PK

    ReplyDelete
  4. Eti jamani kuna nchi duniani ambamo watu hawali rushwa? Mbona kule India, China, Brazil, Kenya, au hata Thailand, Uingereza na Marekani ripoti za watu kula rushwa ni nyingi lakini nchi hizo bado zinaendelea kiuchumi? Hivi sisi Tanzania kuwa nyuma kiuchumi ni sababu ya rushwa tu au kuna mengine ambayo tunaona haya kuyatamka hadharani?

    ReplyDelete
  5. A man of great integrity, principles, wisdom, charisma and, indeed, sense of humour. I am sure there will be people - high up there - who would listen and pretend they never heard. As the MasterCard ad goes - there are things money simply can't buy. A five storey building in the heart of Dar Es Salaam (Tshs. 5bn), peoples' respect and cheris - PRICELESS. Surely, One can't wouldn't swap the building for respect or would s/he?

    God bless Tanzania.

    ReplyDelete
  6. miaka 2 ...viboko 24...12 anapoingia ...12 anapotoka ili akamuonyeshe mkewe...thats Hilarious!hahahahahaha!
    Mwalimu liked to crack jokes in his speeches,though the message was LOUD & CLEAR.mzee alikuwa strict...mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  7. natamani turudi enzi za mwalimu, nimependa pale aliposema mtoa na mpokea rushwa wote ni wakosaji...nimependa zaidi aliposema pamoja na kifungo pia adhabu ya viboko ilikuwa inatolewa...kumi na viwili wakati mkosaji anaingia gerezani na kumi na viwili wakati anatoka ili akamuoneshe na mkewe! zidumu fikra za mwalimu...!

    ReplyDelete
  8. WAKATI WA MWALIMU KULIKUWA NA ARI YA UZALENDO NAKUMBUKA WATU WALIKUWA WANAFANYA VITU KWA KUJITOLEA, KAMA USAFI WA JIJI, UJENZI WA SHULE, ZAHANATI BARABABA, VISIMA VYA MAJI, ELIMU YA WATU WAZIMA. NAKUBALI HAKUFANIKIWA, LAKINI KWA MTAZAMO WANGU ALIANGUSHWA NA WASAIDIZI WAKE AMBAO WALIKUWA WANAMWIITIKIA NDIYO NDIYO MZEE MBELE YAKE LAKINI WAKIONDOKA WAKUWA MBELE KUIBA PESA ZA UMMA NA UBINAFSI. SITEGEMEI KAMA KUNGEKUWEPO UKARABATI WA SHS BILIONI MOJA WA NYUMBA YA GAVANA!!!! NI UFUJAJI WA PESA ZA UMMA, NI MTINDI MWINGINE WA UFISADI.

    ReplyDelete
  9. what a refreshing feeling to see our beloved father, he loved this country with all his heart, he will never be replaced!
    thank u ankal for this. and thanks to mama Maria as well.

    ReplyDelete
  10. Mwalimu alikuwa mtu safi. Ila mizizi mingi ya Rushwa Tanzania ilianzia kwenye serikali yake....kitu ambacho sikuelewa ni kuwa hivi alikuwa anawaogopa viongozi wake? Mbona kulikuwa na rushwa za ajabu na umasikini mwingi uliletwa na ubinfsi wa viongozi chini ya serikali yake..Kisha akachukua nchi mzee Ruksa ambaye ndiye kabisaa..alichukua hilo tochi la rushwa kwa nguvu zote..!! Namheshimu sana Mwalimu na kazi aliyoifanya ila suala la Rushwa alilishindwa yeye mwenyewe alikuwa mzuri tu wa kuliongelea kwenye radio na magazeti...kama wanavyofanya waliopo madarakani sasa...Lol..!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...