Ndugu Michuzi,
Kupitia mtandao huu wa jamii ninapenda kuwakaribisha watanzania na waafrika wote katika ibada maalumu ya kumaliza mwaka wa 2009 na kuukaribisha mwaka wa 2010.
Ibada hii ya aina yake imeandaliwa na kanisa la Umoja la hapa Dallas likishirikiana na watu mbali mbali katika hili jiji.Kwa kweli hii ni mara ya kwanza kuona kila mtanzania ana hamasa ya kumaliza huu mwaka na Mungu tofauti na miaka ya nyuma ambayo kila mtu alikuwa anamaliza mwaka kwa staili ya aina yake.
Kupitia mtandao huu,tunapenda kuwajulisha wale wote ambao wana ndugu na jamaa katika jiji hili kuwahamisisha kuhudhuria siku hii ya baraka na ya aina yake.
Ibada hii itakuwa siku ya Alhamisi, tarehe 31 kuanzia saa tatu kamili usiku mpaka saa sita usiku tutakapo ingia mwaka mpya wa 2010.Tunapenda kumjulisha kila moja wetu kwamba kuanzia saa tatu kamili mpaka saa nne kamili vinywaji na vyakula vya kinyumbani vitakuwa vinaliwa, saa nne mpaka saa tano ni kumwabudu Mungu tukiongozwa na kundi la kanisa la Umoja, saa tano mpaka saa sita ni mahubiri,maombi na shamrashamra za kuingia mwaka huu wa 2010. Saa sita na dakika kumi awamu ya pili ya chakula itaendelea.Karibuni sana tena sana.
Kwa mawasiliano zaidi;
214 554 7381, 682 552 6402,469 279 1762.
Anuani;Kanisa la Umoja,
12727 Hillcrest Road,
Kwa mawasiliano zaidi;
214 554 7381, 682 552 6402,469 279 1762.
Anuani;Kanisa la Umoja,
12727 Hillcrest Road,
Dallas Texas,75230
Pastor Absalom Nasuwa
Pastor Absalom Nasuwa
we mic u mama.
ReplyDeleteneema