Home
Unlabelled
tunondozzzz...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mh! Jamani nyieeee! Haya Hongeraaaaaa!
ReplyDeletekweli Tz imekwisha, jamani darasa la kwanza mtoto anafanyiwa graduation? sijawai una kitu kama iki dunia nzima, yaani nchi zilizoendelea hazina huu ujainga hata kidogo,hongera sana mtoto lakini siyo kosa lako!
ReplyDeleteHongera Binti Agness, piga shule mpaka kieleweke Mungu akusaidie.
ReplyDeleteLakini, with due respect to Agness, wazazi na waliotuma picha hii, naomba tu kuuliza, Hivi, mlioko Ulaya, Marekani na kwingineko ughaibuni hii tabia ya hadi chekechea kuvalishawa majoho ya kuhitimu masomo ipo? Hivi haya majoho na vikofia (vi-degree) havikubuniwa kwa ajili ya elimu ya juu tu (graduate and post graduate level).
te te te he bongo bwana safi sana! lakini inawezekana kufika kule juu ni kugumu mno ndo maana watu wanawahi tu hizi za hapa na kuweka makolombezwo kibao. sasa darasa la kwanza jamani?!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteEnzi zetu (enzi za mwalimu), watu waliokuwa wanavaa majoho ni wale walio-graduate au in short wahitimu wa elimu ya juu! na ndio hapo joho lilikuwa na heshima yake
ReplyDeleteSo ukienda nyumbani kwa mtu kama ukiona ameweka picha ukutani kavaa joho, basi unaona yes, huyu kapiga shule.
Lakini ciku hizi wapi?? hata tutoto twa chekechea tunavaa majoho.
Kwa mpango huu heshima ya joho iko wapi?? mi naona ni upuuzi mtupu kwa hivi vitoto kuveshwa majoho.
mimi mwenyewe nimesoma hadi darasa la nane (mwaka 1968) huko mpanda na sasa umri wangu ni miaka 50 plus lakini cijawahi kuvaa joho.
Lakini nisiongee sana nikaonekana nina wivu, ila nadhani kulikuwa hakuna sababu ya chekechea kuveshwa majoho!
Mdau
S'wanga
Upuuzi huu na upotezaji wa wakati na pesa
ReplyDeletehizi private school zinatia aibu.
ReplyDeleteWe anon. wa kwanza acha ukiritimba hapa katika glob ya jamii, sio kila kitu hadi kifanyike huko ulaya ndo na sie wa TZ tufanye, ina takiwa tuwe wabunifu kwa mambo yetu wakati mwingine.
ReplyDeleteTulisha ongelea mara kibao kuwa kila mtu ana haki ya kupongezwa kwa kila hatua atakayopiga kwenda mbele, sio tu kwa watu higher education. Tujenge upendo kwa wanetu nao wajidai kwani maisha ni mafupi wandugu.
Mzazi hela ikiota mabawa mtoto aturudi kwenye shule za JK ambazo sehem kubwa walishafuta hata cheti cha STD Seven, kusoma kote miaka saba mtu unatoka bila karatasi mimi binafsi nahisi kunyanyasika.
Hilo joho na kofia ni nguo tu ile wala sio elim wala sio kufaulu ni sawa na nguo yoyote ile inayovaliwa na mtu ili apendeze katika sherehe fulani. Wote wanaovaa hilo vazi hasa magraduate sio wote wamefaulu maisha kuna wengine ni wasindikizaji tu.
Acha watoto nao wajidai na wafurahie maisha nao wajione watu muhimu katika jamii yetu.
HUYO NI USHAMBA NA KUTOKWENDA SHULE! AU USWAHILI TUSEME! YAANI INASIKITISHA! GRADUATE AT 6 YEARS OLD! WAZUNGU WAKIONA HII WATATAPIKA! AKA WANANGU TZ NO! HUKU TUBEBE MABOX, MTOTO TZ AKIPATA KUMUNYO YA KWANZA NI MALOMOZINI, UKUMBI UNAKODISHWA, MATARUMBETA YAANI VURUGU TUPU! HUKU KWATE MWABEBA MABOX MTOTO AKIPATA KOMUNYO YA KWANZA AU KIP[AIMARA ITS A FAMILY ISSUES, TUNATOKA CHURCH, GO SOMEWHERE FOR LUNCH, OR HAVE A LITTLE PARTY AT HOME THATS IT! NA INAPENDENDEZA NA WALE WATOTO WADOGO WANAFURAHIA PIA, SIYP KUWAPEKEKA WATOTO KWENYE MABAA, WAZAZI WANALEWA, WATU WANAVUTA SIGARA ITS A SHAME!
ReplyDeletesiyo ulaya au japan,sisi wengi tumesoma hapahapa tz from vidudu to udsm lakini haya majoho ya chekechea nayaona miaka hii ya sasa,tangu nasoma mpaka mid 2000s sijona haya mambo.hii yote ni kutafuta vishughuli
ReplyDeleteHii nadhani ni njia tu ya kujitangaza kibiashara hamna umuhimu wowote wa kutumia ma-joho. Sijaona huku nilipo kitu cha aina hiyo!
ReplyDeleteMimi niko america na nina watoto lakini sijaona kitu kama hiki,this is a bunch of bull hapa states mtoto akimaliza high school anaenda college ndo anakula tunondo nadhani wadau mnajua kuna kitu kinaitwa prom dance. Hii tabia kwa kweli nikutumia pesa na muda vibaya na kuwadanganya watoto wetu kwamba wame achieve something, which is not bad but unnecessary at that stage.Kwa kweli sijui ni mtoto wa nani sasa hivi amebakia kwenye public primary school huko bongo na haya yote yanatokea kwa sababu ya mlipuko wa hizi english medium schools wakati sie tunasoma there was no such a crap na inasikitisha.Nawakilisha
ReplyDeletemdau USA
mliopo ughaibuni pole kwa mtikisiko wa uchumi..huku hatuja fulia!
ReplyDeletekwani ng'ombe wakiongezeka ni party..
mtoto akimaliza madrasa,kipaimala,komunyo,ndoa,ubatizo n.k ni sherehe!
msituone wivu!
jamani joho ni nini?
si vazi tu!
halina chochote!
kikubwa ni wewe una nini kichwani ndio cha kubishana!
hivyo waacheni watoto watese kwani hali ya uchumi inaruhusu..
lakini enzi za Mwalimu wangelabwa mboko waandaaji wa sherehe,shule,walimu na kadhalika 6
Kutokana na michango ya wadau wengi inaonyesha hii kutoyapa hadhi inayostahili majoho ipo huku Tz tu sijui nchi nyingine za ki-africa. May be nchi zingine zina sheria ya kuyatambua majoho kama vazi maalum kwa wanaohitimu elimu ya juu tu. Kama wanajeshi wanavyokamata-kamata watu wanaovaa mavazi yenye rangi kama combat zao, askari magereza waliwavua live ma-konda walipojaribu kuvaa uniform zinazofanana na rangi ya magwanda yao na kuwapa onyo kali, mamlaka zinazosimamia elimu ya juu zingefanya kitu ili kulinda heshima ya majoho haya na elimu ya juu. Naamini waliobuni hawakubuni kama vazi tu linaloweza kuvaliwa popote na yeyote. Yana muundo,rangi na namna maalum ya kuvaliwa na ndio maana yanatumika vyuo vyote sehemu mbalimbali duniani.
ReplyDeletewe anaesema wabeba mabox tunawaonea wifu, lo nyie kazi kuchangisha vimichango eti greduation ya mtoto ou kipaimara, mnapita kila kona, sasa sama sasa ua nikutumie pound hapa maanake today its a pay day twalipwa kwa week haswa!
ReplyDeleteMheshimiwa Michuzi asante sana kwa kutupasha mengi yanayotufanya wengi tufunguke akili na kujua yaliyo muhimu katika jamii yetu.
ReplyDeleteKwa fikra zangu binafsi mtu au mtoto kufikia hatua fulani ni vizuri kumwekea kumbukumbu fulani inayomfanya afarijike. Lakini kuna mambo yanayoendana na mazingira, nafasi na kiwango kwa waliostaarabika.
Waliobuni joho kihistoria lina maana yake halisi katika falsafa yake. Mimi sijui kama mtoto mdogo wa chekechea anajua maana ya kuvishwa joho kwa mhitimu zaidi ya kupewa part nzuri ya kifamilia na kufahia kula keki na purding.
Watanzania tuna kawaida ya kuiga mengi bila kujua misingi yake, na cha kushangaza tunavuka mipaka ya ukweli na hali halisi ya maana ya yale tunayoiga.
Labda falsafa moja wapo ya kuvishwa majoho kwa wahitimu ni kwamba wanapewa jukumu ya kwenda kulijenga taifa na jamii baada ya mahafali ya chuoni kwa wahitimu baada ya kula nondos.
Sasa kaka Michuzi huyu mtoto mdogo ni majukumu gani anayoenda fanyia taifa na jamii baada ya kuhitimu chekechea zaidi ya wazazi kuendelea kumtafutia shule ya darasa la kwanza? Party ya kuwapongeza na kuwapa moyo ndo lingejenga maana halisi vinginevyo tunafanya kitu kinachowashangaza wengi na hakileti maana muafaka kifalsafa
Nyie bwana,tuachieni tz yetu. Mnajidai oh huku marekani sijui hakuna hili wala lile. Maisha ni mabadiliko, sio lazima kila kianze kwa wazungu. Hata sisi twaweza kuanza, kama hawawezi kuiga ni umaskini wao maanake sisi wamefulia, huku kwetu maisha mswano. Poleni sana wabeba box, hela yenu haiwatoshi msithubutu kuiga.
ReplyDeleteThis is ridiculous na ulimbukeni uliojaa ushabiki wa kishamba kabisa. Joho lina maana kubwa sana kwa wanaograduate na ile kofia yake pia ina maana yake kwa graduates, sio kujivalia tu, rangi za kofia na joho zina maana kubwa sana katika ulimwengu wa graduates wa degrees mbalimbali, sasa wabongo mtoto chekechea, darasa la kwanza sijui anavalishwa joho eti ka graduate, kagraduate kwenye kitu gani haswa wakati bado ananuka maziwa na mkojo, yaani mimi hii kitu inanikera inanikera sana, sometimes i wish Mwl Nyerere angekuwa hai apigie makelele vitu vya thamani kama hivi, sio hio mijizi huko serikalini imekaa tu inajionea sawa, this is a whole bunch of crap!!! Ndio maana mi watoto wangu wacha wasome huku huku majuu maana bongo huo utitiri wa academys uliojaa walimu feki sitaki kabisa, mtu anajua tu kiingereza cha yes and no anaanzisha academy anaiita sijui international school, wizi mtupu!!!!-Mdau Canada.
ReplyDeleteNyie wabeba mabox kama hamna muda na hela za kusherekea achivement za watoto wenu kaeni kimya. Mnaona wivu, donge la nini.Sisi wenzenu bongo kuko tambarare watoto tunasomesha private, tuna hela za kuwapongeza na kila hatua wanayofikia. Msituonee wivu.
ReplyDeleteWewe mdau unayesema unakaa America na hujaona watoto wakitunukiwa nondo wakimaliza preschool, ni America gani mwenzetu unayokaa, for sure unaishi kwenye "HOOD" Mitaa ya wamarekani walala hoi, na watoto wako wanasoma na WANUGU.Kama uongo nihakikishie.
Wewe mdau unayesema "wazungu wakiona", wewe tu ndie limbukeni na mzungu na kumuogopa kwa kua anakubebesha box, Dar tuna mambo yetu hayafatishi ya wazungu tunapongeza watoto watoto wetu kwa matarumbeta na kila kitu, mbona hamtuonyeshi mnavyowapongeza watoto wenu huko ulaya kama wazungu walivyowafundisha. ACHENI WIVU!!!
MICHUZI THIS IS 100% CHILD ABUSE hii ni kutokana na comments za watu japokuwa hata mimi sioni umuhimu wa huto tunondozz. plz plz delete that photo uli watu wasiendelee ku mu abuse mtoto wa watu! mdau UK
ReplyDeletewengine wakisikia ufisadi wanafikiria ni pesa tu! tanzania sasa hivi tumo katika kipindi cha mfumo wa ufisadi na dalili mojawapo ni mafisadi kuwa na pesa nyingi kiasi cha kushindwa kujua wazitumieje. ndipo wanapoibuka wajasiriamali ambao wanawaletea kila kitu ambacho binadamu anaweza kufikiria. majoho ya tunondooz twa chekechea ni mfano hai wa kukidhi kiu ya matumizi ya mafisadi. kumbukeni asilimia 90 ya watoto wa elimu ya msingi nchini fisadiland hawana sare za uhakika za kwendea shule!!!
ReplyDeletekuna faida na hasara. faida mojawapo ya ufisadi ni kukuza ujasiriamali! we mafisadi walete cho chote na kuwaambia hivi ndivyo ilivyo huko ulaya!
Nasema tabia hii inaudhi sana watanzania!!!! vazi hili limeshushwa thamani nchini tanzania kiasi hiki jamani?
ReplyDeletewewe unaesema joho ni vazi tu, inaonyesha hukusoma hadi kufika ku-graduate kikweli kweli. umewahi kumuona mganga wa kienyeji akavaa koti la daktari, au umewahi kufika muhimbili na kumuona daktari amevaa mahirizi na kaptula ya nyasi? umewahi kumuona wapi dereva wa dala dala amevaa uniform za pilot wa ndege? si wote wanasafirisha watu?
ReplyDeleteuvaaji wa joho style hii ni tradition ya wanaelimu duniani kote toka zama za zamani. ni vazi linalothaminiwa na kuheshimiwa mno, sio vazi la kumvisha mtoto anamaliza michepuo. watu huvaa/huvalishwa wanapohitimu masomo baada ya miaka tele ya kubukuwa, sio kwenda michipuo kuimba kwa mwaka halafu unavishwa joho na kuthubutu kusema kuwa mtoto ame-graduate!!!
kama mnataka kusherehekea mafanikio ya watoto wenu anzisheni vazi lenu na sio vazi hili!
JK alisema anataka vijana na watoto katika baraza lake. Haya sasa wasomi ndio hao. Utamuona mstari wa mbele katika baraza la mawaziri 2010. Nyie wengine kalagabaho!!
ReplyDeleteWaacheni Wazazi wafurahie jamani...pengine mtoto huyu kwenye familia ndiye wa kwanza kufikia Darasa la Kwanza...hiyo ndiyo Elimu ya juu zaidi ya wote kwenye familia; sasa kwa nini wasijivunie???
ReplyDeleteHamuwezi kujua...
Wadau tunapotosha maana halisi na heshima ya haya mavazi,....soma hii tafsiri kutoka weekpedia Academic dress or academical dress is a traditional form of clothing for academic settings, primarily tertiary and sometimes secondary education, worn mainly by those that have been admitted to a university degree (or similar) or hold a status that entitles them to assume them (e.g. undergraduate students at certain old universities). It is also known as academicals and, in the United States, as academic regalia.
ReplyDeleteContemporarily, it is commonly seen only at graduation ceremonies, but formerly academic dress was, and to a lesser degree in many ancient universities still is, worn on a daily basis. Today the ensemble generally consists of a gown (also known as a robe) with a separate hood, and usually a cap (generally either a mortarboard, a tam, or a bonnet) which are distinctive to each institution. Academic dress is also worn by members of certain learned societies and institutions as official dress.
Wewe mbeba box unaekaa Marekani kwa taarifa yako watoto wa High school za marekani wakigraduate wanavaa joho, pata uhakika kabla hujatoa comment, hata wa chekechea wanavaa joho inategemea shule gani unapeleka watoto wako.
ReplyDeleteMdau unaeyesema sherehe zako huko ulaya ni family issue, huko ulaya uko wewe na huyo baba uliyezaa naye wengi wenu hata hamjafunga ndoa sasa hiyo family issue unayoipromote hapa ni ipi?? Huko restaurant pia sio mahali maalum pa watoto. kama hamuwezi kuspoil watoto wenu na pay check zenu za kila wiki tuachieni bongo tutanue na watoto wetu.
Hongera sana mtoto Agnes mungu akubariki uzidi kupokea nondo kila level unayomaliza.
mdau wa tue dec 01,7:27:00 pm unaonekana kuna watu wanakufundisha terms za america kama hood na wanugu eeh? huu ujinga hapa america hatu entertain hata kidogo na unashabikia kwa sababu labda maisha ya huku yalikushinda ama walikurudisha kwa ujinga wako mwenyewe the bottom line lazima tuyape hadhi majoho ndo maana unaona hata majaji wanavyovaa tofauti na mahakimu.
ReplyDeleteJAMANI TUWE CRITICAL NA WADADISI. KWANZA KABISA HAYA MAJOHO NI NINI NA MWANZO WAKE ULIKUWA NINI? HAMNA HATA SEHEMU MOJA KATIKA SHERIA YA NCHI YOYOTE ILE INASEMA MAJOHO YANAVALIWA NA NANI NA KWA WAKATI GANI, HIYO NI JUST TRADITIONAL ILIYOKUWEPO TOKA ZAMANI WAHITIMU KUVAA JOHO LAKINI HAINA WALA SHERIA KUWA NI UHITIMU WA NGAZI GANI WAVAE MAJOHO. TANZANIA TUMEZOWEA KUONA TOKAMIAKA YA 60 WALIOKUWA WANAVAA NI WA CHUO KIKUU BASI TUKAONA NI KAMA SHERIA ATI NI WAHITIMU WA DEGREE TU NDO WANATAKIWA KUVAA MAJOHO SI KWELI, HAYO NI MAZOEA YETU TU, JOHO LINAWEZA KUVALIA NA MTU ANAYEHITIMU NGAZI YOYOTE ILE SI LAZIMA DEGREE. NI SAWA NA KUSEMA KUVAA KANZU NI UISLAMU, KWANI SISI WATANZANIA TUMEZOWEA KUONA WAISLAMU WAKIVAA KANZU TOKA ENZI BASI TUKA-ASSUME KUWA NI UISLAMU KUMBE SI HIVYO KANZU NI VAZI LA WATU WA MASHARIKI YA KATI HATA WASIO WAISLAMU WANAVAA. JAMANI TUACHE TABIA YA KUONA JOHO NI KWA WAHITIMU WA DEGREE TU HIYO SI KWELI.
ReplyDeletemh!! humu ndani kuna watu wana midomo mirefu kama chuchungi lol!!
ReplyDeleteWewe mdau hapo juu unayesema marekani hata chekechea wana graduate na kujaa joho basi nakuomba leta picha hapa kwa michuzi uni prove wrong na kama utaweza kufanya hivyo, basi mimi nita retire kuangalia blog ya michuzi.
ReplyDeletemdau USA
Mi la kwangu ni kuwa mbona huyo mtoto kazeeka? Huyu alitakiwa kuwa la tatu au la nne na siyo chekechea
ReplyDeleteMTANUE NA WATOTO WENU WAKATI MNAJAZANA UJINGA TU WENYEWE KWA WENYEWE
ReplyDeleteMhh! kweli waswahili tu tumekosa kazi, hata huo utoaji maoni wetu unazitilia shaka hizo degree zetu na majoho tuliyovalishwa! ..haya yangu macho!
ReplyDeleteOnyo: Toeni hoja kama watanzania na si kila mtoapo hoja muanze na `.....Nimeishi ulaya miaka mingi sijaona hii....` ni upumbavu wa hali ya juu na kuashiria ujinga. mnapotaka sisi tuige wao je wao walimuiga nani? Acheni kutukuza ujinga wa kuishi maisha ya kifahari europe mwishono mnarudi nyumbani unakuwa maskini. pendeni kwenu kwa kutenda sio kutoa hoja tu
ReplyDeleteJAMANI TUTUNZE HADHI YA JOHO, SIYO UNAWEZA KUSOMA JUMA NA ROZA BASI JOHO!!!!!!!!!!!!!! NO.
ReplyDeletehii inaonyesha hata mwenye shule hajagraduate vinginevyo angejua tabu ya kuvaa joho ilivyo, mimi degree ya kwanza na psotgraduate dip sikuvaa mpaka nilipopata mastas ndo nikaingizana kwenye graduation huku mwimbo wa taifa ukipigwa na bendii ya polisi
ReplyDeletenimecheka na izi comment
ReplyDeleteila yooote huu ni ushenzy na utaahira mkubwa na umbumbumbu,afu later mtu aanza ooh hali ya uchumi bongo ngumu hatuna pesa hazikai mfukoni,,,afu mwavalisha vitoto MAJOHO kwanza wanatisha hawapendezi wala haivutii chembe,
pili kupoteza muda,wakati na pesa ungefanyia vitu vingine!!!
michu hatutaki picha za mauzi bloguni km izi
ovyo SANA
Wed Dec 02, 05:12:00 AM
ReplyDeletemdau ni "chuchunge" sema "nge"
This is bullshit kumvalisha mtoto graduation gown eti kamaliza vidud, darasa la kwanza, sijui! Kweli Bongo hiyo gown haina thamani wala maana! PARTY CULTURE IMEZIDI BONGO. Kumbukeni kulijenga TAIFA! Watu wamesahau kujenga taifa maana yake ni nini.
ReplyDeletemh jamani acheni uzalilishaji wa wasomi.yani mnafananisha watoto wa chekechea na wenye degree!!!!!!gepu kubwa sana hapo.joho alilovalishwa huyo mtoto ni uzalilishaji.na mnafanya sasa wasomi kupoteza hadhi yao.maana joho halitakua na heshima tena.mh jamani we mzazi wa huyu mtoto umeenda shule kweli wewe?au umeishia darasa la nne lile la zamani?maana mh sizan kama mtu mwenye akili timamu anaweza fanya huu upuuzi.
ReplyDeletemzazi wa huyu mtoto atakuwa mhaya!!
ReplyDeleteMnaomkandia mzazi wa mtoto huyo eti kaishia darasa la nne la zamani, hivi hujui ni bora yule wa darasa la nne la zamani kuliko huyo graduate wa sasa asiyejua hata kienglish.
ReplyDeleteMnao babaika na wazungu wenu ni huko huko msidhani sie bongo tuna hata shida na hao watu, hatuna muda wakuiga kila upuuzi wao namani, na sio kila kitu wafanyacho wazungu ndo kizuri mbona wanaharibu vingi?
Mnadhani maisha ya wazungu ndo bora kuliko yetu? hapo mmechemka eti mkiwa na viparty ni family issues hamuoni upweke? Ukija masuala ya uvutaji wa sigara hivi ni wapi wanakovuta sigara ovyo kati ya bongo na huko kwenu feki?
Nyie wazungu feki acheni uzambiki kuiga mambo ya kishenzi ya magharibi.
Huo usomi wenu mnaoulilia kila mara mbona utendaji wenu hatuuoni Uozo mtupu maofisini kazi ni ufisadi tu, hata majoho mnayoyalilia bure kabisa afadhali na watoto nao waambulie maana hili vazi limeshushwa hadhi na asilimia kubwa ya magraduate feki feki.
Mnabisha???????? Ukweli mnaujua kabisa! Wizi mtupu
Post nyingi ni za kulaumu,badala ya kumpongeza huyo mtoto.
ReplyDeletetuache hizo wenye visa ni watu.
Hongera mtoto wewe.
Mchumiajuani.
ANON WED DEC 02, 07:04 UMENIFANYA NIRUDI KUANGALIA HIYO PICHA, NANUNUKUU"MI LA KWANGU MBONA HUYO MTOTO MZEE?ALIFAA KUWA DARASA LA TATU AU LA NNE" TEH TEH TEH TEH TEH.....KUNA KA UKWELI FULANI HAPO LOL
ReplyDelete