Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha
baraza la mawaziri ikulu jijini Dar leo asubuhi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Nini kinachojadiliwa kwenye vikao hivi wakati hakuna chochote kinachoonekana chini ya serikali hii. Tanzania inaathirika na tatizo linaloitwa "Failure of leadership", tofauti yetu na Somalia ni kwamba kule kuna mapigano vinginevyo kama ambavyo Somalia haina mfumo wala mwelekeo wowote ndivyo Tanzania ilivyo. Miaka 48 tangu tujitawale lakini hata mfumo wa ukusanyaji kodi, afya, elimu, miundombinu, n.k. hakuna, ni heri mara mia wakoloni wangeendelea kuwepo maana tumethibitisha kwamba hatuwezi kujitawala.

    ReplyDelete
  2. wewe mjinga unayesema bora mkoloni angekuwepo unaonesha unaakili zilizolala,mkolono alifanya nini tz,ameondoka ameacha barabara iko dar mjini na na moshi arusha peke yake,leo barabara inaunganisha nchi kwenye mikoa kibao,inamaana huoni ilichofanya serikali ya awamu ya 4,au ndo roho ya korosho na chuki binafsi za kiafrica unaleta hapa.

    ReplyDelete
  3. ni bora mara mia kujitawa kwa shida kuliko kutawaliwa,ndege umjengee banda na umpe chakula kila siku,lakini siku ukiwacha mlango wazi ataondoka bila kurudi,kwa sababu kutawaliwa ni sawa na ndoa za zamani walizofanyiwa mabibi zetu

    ReplyDelete
  4. Anony no 1 nimekuelewa vizuri sana. Bahati mbaya sana wachangiaji waliofuata hakuna hata mmoja aliyekuelewa. Mimi kama wewe sielewi mantiki ya hivi vikao. Hivi wanaongea nini mbona nchi inaenda kiholela tu? Ipi tofauti ya kuwa na vikao na kutokuwa navyo? In my opinion hata hizo allowances wanazopeana na vikao hakukuwa na haja ya kulipwa kwa ni kumwonea mlipa kodi wa tz ambaye hata mlo mmoja ni kwa kulenga sana.

    ReplyDelete
  5. Kutawaliwa siku zote ni kubaya. Lakini je uhuru una maana gani kwa watanzania wa leo?

    Mimi nadhani hoja ya msingi ni kupima je miaka 48 sasa tangu uhuru nini kimefanyika? Je kilichofanyika kinatosha kuwa kazi ya miaka 48 ya kujitawala? Kama kinatosha, tujipe hongera. Lakini kama hakijatosha tujiulize kwani nini?

    Watanzania wengine ukiwauliza watakuambia hawajaridhika bado na juhudi zilizofanywa kwani nchi ingeweza kupiga hatua zaidi ilivyo sasa kama mambo yanafanywa kwa makini zaidi.

    Haingii akili leo hii wanafunzi tena hapa jijini Dar wanakaa chini kwa kukosa madawati, umeme wa mgao kila mwaka, maji ya shida, n.k hata baada ya miaka 48 ya uhuru.

    Nadhani hii ndio inamsukuma mdau wa kwanza hapa kuuliza wanajadili nini kwenye hivi vikao wakati wananchi wengi bado wanaishi maisha ya taabu.

    Jamani tukumbuke watanzania walio wengi leo hii hawana uhakika kama watakula. Na kama wakipata mlo, mlo wenyewe unakuwa wa kiwango cha chini kabisa.

    Huku vijiji watanzania wanachemsha tu majani wanakula na ugali siku nenda siku rudi. Hata Dar hapa wapo wengine tu wa aina hii. Watu wengi wanakunywa maji ya vidibwi/visimani. Hospitali hakuna, watu wengi wanakufa kwa magonjwa ya tiba rahisi tu.

    Nadhani matatizo haya yanaweza kufanya mtu akatamani maisha mengine, kwa hiyo mdau kusema afadhali wakoloni wangeendelea mimi sishangai sana. Kwani hamjawahi kusikia watu wengine wakisema "AFADHALI WANGEZALIWA KAMA MBWA ULAYA"?

    Matatizo ya maisha yanasababisha mtu kuukana hata utu wake.Sasa kama watu wanaua Albino kwa matarajio ya kupata utajiri hii si tayari ni kuukana utu. Hii yote ni matokeo ya matatizo ya kimaisha.

    ReplyDelete
  6. anon 03:03 acha jazba,barabara zote unazoziona nchini ni za mkolono,serikali haijajenga hata moja wanachofanya ni RESURFACING, hii ni miundombinu yote ni ya mkolono kuanzia maji hadi umeme ndio maana maji na umeme ni ya mgawo kwani idadi ya watu imeongezeka ila huduma ni zilezile, in early 80's barabara zote/mitaa yote dar magomeni/ilala/upanga/o'bay etc hata mikoani, ilikuwa na lami leo hii hujui hata kama lami ilipita except few streets walizo-resurface,kama ulizaliwa mjini miaka ya 50-70's utanielewa kama umekuja au kuzaliwa in 80's DONT BOTHERS ARGUING COZ U DONT KNOW NOTHING PRE/POST COLONIAL.....nasisitiza sipendi wakoloni waje ila tuamke tujiendeleze

    ReplyDelete
  7. Kama unaona kutawaliwa ni madhila kwa nini nyinyi Watanganyika munaitawala Zanzibar.Tuacheni sisi Wazanzbari tuwe na utawala wetu,sio mutatuchagulia viongozi munaowataka nyinyi huko Dodoma.

    ReplyDelete
  8. Ni ukosefu uwezo wa kuchambua masuala ya Tanzania ndiyo unafanya watu wengine kuona kuwa serikali hii hafanyi lolote. Lakini ukweli ni kuwa Tanzania inapiga hatua chini ya Kikwete. Ndiyo bado watu wanamatatizo mengi tuu, lakini njia ya kuyaondoa sio kulala na kulalama kusubiri seikali ukufanyie kila kitu. Wewe unafanyi nini kwa maisha yako mwenyewe? Mimi nafurahishwa na wajasilimali wote wao ndio wanaweza kulalamika kama serikali inawawekea vipingamizi katika ujasilimali. Lakini wewe ukiwa ni mtu wa kusbiri serikali ikutafutie kazi, chakula, na sehemu ya kulala bila ya wewe kuchangia chochote kweli huo ni ujinga wa akili uliokithiri.
    Pato la kila mtazania wakati wa mwalimu Nyerere lilikuwa dola za kimarekani 150 ($150) lakini sasa hivi ni dola za kimarekani 1,400 ($ 1,400), Kenya wao pato la kila mtu ni dola za kimarekani 1,600 ($1,600). Tanzania kwa sasa sio tena kama zamania kuwa ndio nchi ya kutupwa kwa umasiki. Tumezifunika nchi kibao kwa uwezo wa taifa. Na Tanzania inaenda mbele hairudi nyuma. Pato la kila mtu litazidi kuongezeka kama tutaendelea kuwa na viongozi kama Kikwete sio misifa tu lakini nchi inateketea kama ilivyokuwa zamani.
    Tuache kusema kikasuku bila ya kujua kinachoendele katika uwanja mzima wa uchumi duniani. Je unajua kuwa dunia iko katika msukosuko mkubwa wa kiuchumi? Kikwete na timu yake wamewezakuwa kuwa waangalifu kwa matumizi ya serikali kiasi watu wengi hawaoni huo msukosuko. Kuweni wakweli katika lawama zenu kwa Raisi msimlaumu tu ajenda zenu na propaganda za kipuuzi.

    ReplyDelete
  9. JK anauliza. Ni nani huyu anavujisha siri za Baraza la Mawaziri kwa gazeti la Raia Mwema. Mawaziri wote vichwa chini.

    ReplyDelete
  10. Kumlaumu Kikwete kwa matatizo yaliyopo nchini ni sawa na kulaumu ulikoangukia badala ya ulipojikwaa.Nchi imebomolewa wakati wa awamu za pili na tatu, bahati mbaya wachangiaji wengi wa hii mada huwa hawazungumzii hili mbali ya kulaumu serikali ya awamu ya nne ambayo katika uhai wake mfupi imejaribu kuweka mambo sawa ingawa kazi kubwa bado inahitajika.Kumbukeni Richmond, EPA,kuuzwa nyumba za serikali na mikataba mingi isiyo na maslahi kwa taifa vyote hivi vilifanyika wakati wa awamu ya tatu, nani alikamatwa, kushtakiwa au kujiuzulu miongoni mwa vigogo wa serikali wakati huo?, acheni chuki binafsi, kama mlikimbia kuomba ukimbizi nchi za wengine tulieni huko mliko ridhikeni na mnachopewa na hao waliowahifadhi, hamna faida kwa Tanzania.

    ReplyDelete
  11. Mdau MJ zamani bongo ilichagua siasa. Tulikuwa wapiga domo sana, hatuna nguo tunavaa mifuko ya mbolea, unakumbuka vi-sulphate, hakuna sabuni kiujumla matatizo kibao, uwezi kutoka nje ya nchi, waliotoka walienda kusoma nchi za kikomunisti, ilimradi hali ya kufakufa tu na viongozi wote wimbo mmoja tu zidumu fikra sahihi za mtawala na wananchi wanaendeshwa kama kondoo. Hiyo ndio hali ya bongo ninayo ikumbuka mimi enzi izo za hao wanaodai ati tulikuwa na uongozi! Kweli nchi ilikuwa ikitawaliwa kipolisi, mashushu kila kona, kuanzia balozi wa nyumba kumi mpaka juu. Huna uwezo wa kusema yale ya kweli unayoyaona na kufikiria.

    Tumetoka mbali, tusidanganyane eti tulikuwa poa huko nyuma, Mzee Mwinyi lazima tumpe sifa zake kwa kuanza kubadilisha fikra za kimawazo za watu wa nchi hii.

    Zama hizi ni za kiuchumi, kama wewe bado uko katika zama zako za siasa pole sana. Ata Urusi siasa za kuabudu watu ziliwashindwa na wakaporomoka na sasa wanaendekeza uchumi tu. Tazama wachina vilevile.

    Ndiyo Tanzania bado kuna rushwa, umangi meza na matatizo mengine lakini yote haya yataondoka kwa jitihada za mfumo mzima sio mtu au kikundi kidogo cha watu. Bunge, mahakama na serikali ndivyo vinavyounda mfumo wa utawala wa nchi vishirikiane na wanachi kuisukuma Tanzania mbele.

    M/Mungu ibariki TZ.

    ReplyDelete
  12. laiti waliopigania uhuru wangetuona leo tulipo wangejuta kwanini walipigania kuwa huru. nimemnukuu Kipanya, nadhani ukiichambua hii kauli utapata jibu sawia!

    ReplyDelete
  13. tuangalie wenzetu wanachosherehekea siku ya uhuru huwenda tukawa tunautofauti kidogo.

    " Tomorrow, 31st of august we Malaysian will celebrate our independence day. it has been 52 years our country has freed from the colonization. Today, Malaysia has developed rapidly and well known by the world. Our achievements are undeniable and we have become role model in many things. We are now moving towards vision 2020 in attaining the developed nation status.

    Since independence we have attained so many achievements. Nearly forty years ago, we moved very slowly. We don’t have enough expertise among Malaysians to help the government in developing the country. From the past, we learn from mistake. Our government has taken action and did their best to make policies which can ensure our competitiveness in economy for the sake of the people.

    Government also is looked concern in promoting the social welfare where the rate of poverty has decreased drastically. The national education policy has succeeded to form intellectual societies. Since 1960, our local universities have born many experts as well. This achievement has undoubtedly contributed a lot for the development in many fields.

    Independence means not only free from the colonization. it must be defined broadly. Independence also means we are free from corruption, abuse of power, poverty, mismanagement, crime, riot etc. we cannot let this things happen. Independence includes respect for human rights, human dignity and social justice as well. We must uphold the supremacy of the constitution, rule of law and equality before the law."

    ReplyDelete
  14. mdau unatolea mfano malyasia,hao walianza zamani,sisi nyerere ndo katutia ufukara kwa siasa za ujamaa,nashangaa kuna watu wanamsifia nyerere na azimio lake la arusha,uppuuzi mtupu,mungu ampe maisha marefu mzee ruksa,ametutoa kwenye usiku wa giza.

    ReplyDelete
  15. Wadau hapo juu mmeonesha kufunguka kimawazo, kiakili na kujadili mambo ya msingi kwa kina.Mimi napingana na huyo anayetetea mabadiliko kwa kigezo cha barabara. hii sio sahihi kabisa, huwezi ku measure maendeleo ya nchi kwa kutumia kigezo kimoja eti barabara, watu duniani hata kwa mfano wa karibu tuu kama rwnda wanaangalia(miundo mbinu(physical) na Pia Social) yaani afya, elimu, usalama, na kadhalika.sasa, huyu kikwete amefanya nini mpaka sasa hivi kuinua at least kimoja wapo.Hamna hata kimoja, muendelezo umekuwepo kwa vichache vilivyoachwa na waliomtangulia.
    Uwezo wa kuongoza hana, hilo lazima tukubali. vikao kama hivi vinatakiwa viwe vya kitendaji na vipimwe kama ambavyo board ya benkiya kampuni inavyo operate. Tumepanga kuongeza ufanisi katika elimu ya sekondari- walimu watakaofundisha sekondari ni lazima wawe graduates, je tutawalipa competitive salary gani ili sekta iwe attractive, sustainable na yenye tija? laki tano gross? nne u tatu? fedha tutapata wapi? bajeti hii inaweza kukidhi mpaka wapi? utegemezi wa nje ni mkubwa kiasi gani? lengo hili tulifikishe lini na tulipimeje? huoo ni mfano tuu wa mambo yanayotakiwa kuongelewa katika cabinet ambayo hata wananchi wataona impact whether haraka au baadae ila ni translated directly into peoples lives!
    Kucheka cheka, kutokuwa makini, kuwa na marafiki kwenye cabinet ambao hawana uwezo angalau hata basics?! ndio kinachoongoza Tanzania.
    Kwa mtindo huu, mwananchi wa kawaida hawezi kuguswa na uwepo wa serikali fanisi hata kidogo!
    Ni aibu kwa kweli, ila kinachotia moyo ni kwamba, ipo siku things will change kwa sababu uelewa wa watanzania unakuwa na itafikia wakati watasema basi! iwe basi ya mtutu au ya Amani ndio hatuwezi predict kwa sasa.

    ReplyDelete
  16. mtoa maoni namba moja una akili sana tena ningepata e mail yako tungekuwa tunachati ila naomba kaka mithupu akufikishie e mail yangu nayo ni makoyehayes@yahoo.com mimi niko usa na kamwe sitakanyaga tena ardhi ya kiwalani kwani tanzania ni mara mia warudi wakoloni labda tunaweza ona mabadiliko nchi gani tunashindwa hata kujenga kiwanda cha sindano au pini za kufungia nepi za watoto kila kitu tunategemea kuagiza china na nina hakika baada ya miaka mitano mingine bongo itakuwa maskini zaidi

    ReplyDelete
  17. kaka naniihii hao wanaomponda mtoa maoni namba moja wote ni watoto wa mafisadi hivyo wanaishi osterbay na wanakula kuku kwa mlija hivyo kwa bongo ni poa tu ila tunaomba wajue kuwa kuna watanzania hawana hata shilingi mia moja ya aspirini,mfano huku sumbawanga utafikiri tuko serikali ya zambia yaani mkoa maskini kweli

    ReplyDelete
  18. MJ,

    Hizo takwimu zako si zimendikwa tu kwenye makaratasi? umesikia kilwa watu wanachemsha maembe mabichi wanakula, Dodoma watu wanakula ubuyu na sehemu nyingi za tanzania....sasa unasemaje uchumi umekuwa wakati upande mmoja (minority) unakwenda kutibiwa marekani, uingereza, india, regency hsp,aga khan na kwingineko, pia wanakula mpaka vingine wanatupa jalalani, wana nyumba ambazo hata nyingine hawaishi ndani yake, wanatembelea magari ya kifahari,n.k wakati upande mwingine (majority) wanaishi maisha ya kubangaiza na wengine hawana chakula kama nilivyosema awali,wanafariki kwa kukosa matibabu....Jambo ninalotaka kulizungumzia hapa ni kwamba centralization ya uchumi ipo mikononi mwa wachache sana hivyo ile gap ya innequality imezidi kuwa kubwa....sasa usituhadae na takwimu kama hizo...ni vizuri ikatumika commonsense kujudge vitu kama hivi kwani maisha ni emperical something that can be seen and felt......Kwa kawaida matabaka yaliyokuwepo tanzania yalikuwa ni matatu yaani chini, kati na juu sasa yanaelekea kuwa mawili makubwa; haves and have not! Mdau aliyetoa mfano wa tofauti ya somalia na sisi ni mkweli kabisa...but hatuhitaji mkoloni cause kama wanadiriki kututemea mate kwetu je wakitutawala si itakuwa zaidi ya hapo? Tunahitajika vijana tulio na dira na misimamo dhabiti tuchukue nchi wazee na baba zetu wameshashindwa;

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  19. mbona kikwete kafanya mambo ya maana sana tu kwa kipindi kifupi,kitu kama chuo kikuu cha dodoma ni moja ya mambo muhimu ya jk allofanya,haikuwepo hata kwenye ilani ya ccm ya 2005-2010.kile chuo ni kikubwa na kina maana sana kwa watanzania kuliko hata ule uwanja mpya wa taifa,elimu ndo kitu kinawasumbua wa tz sasa hivi,bila elimu ndo matokea ya watu kukojoa juu ya masinki,ajira za kudumu zimeongezeka tz,jk ameingia madarakani tz inapokea watalii laki 5 kwa mwaka,now kunakimbilia milioni karibu kabisa na kenya,ameweza kuwavutia wawekezaji wakubwa wa mahoteli kwa juhudu zake binafsi,ukiangalia ukanda wa waskazini utaona.ajira zimezidi maradufu kwenye utalii,hakuna kiongozi yeyote anaweza kuichukua nchi kama tz akaondoa umasikini chini ya miaka 20,hii nchi,ona nchi kama thailand,bado kuna umasikini wa kutupwa pamoja na maendeleo yote,tatizo ni tulifuata siasa za ujamaaa na ndo zinaoiumiza africa nzima sasa,maana kutoka kwenye ujamaa na njaa kali,ukiingia kwenye ubepari rushwa nilazima itawale,ndo maana matajiri wengi wa dunia wanatoka india na russia,na masikini pia utakuta wanatoka india,na kwa ulaya eastern europe.

    ReplyDelete
  20. uzembe mtupu umekaliwa apo

    wananikeraaaa acha tu...

    ReplyDelete
  21. Ningeomba muende kuchangia pia katika mazunguzo ya Jakaya Kekwete na mzee wa nyika (RK) kwani yanaenda sambamba na hoja zilizojitokeza hapa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...