Snow Crest Hotel
Na Woinde Shizza, Arusha

Rais Jakaya Kikwete ameonya kuwa tatizo kubwa la udokozi wa vijana wa Kitanzania wanaoajiriwa katika mahoteli kunasabababisha wawekezaji wengi katika sekta hilo kuajili watumishi kutoka nje ya nchi

Rais Kikwete alitoa changamoto hiyo wakati anafungua hoteli ya kisasa ya kitalii inayomilikiwa kwa asilimia mia moja na Watanzania ya Snow Crest ya mjini hapa.

“Tumekuwa mahodali sana wa kulalamika ooh wageni wengi wanaajiriwa katika hoteli na kukimbilia katika vyama vya wafanyakazi huku tukisahau kwamba tuna tabia mbovu za udokozi pamoja na uvivu wa kupita kiasi,”alisema Kikwete.

Kikwete alieleza kuwa hakuna mwekezaji wa hoteli aliyeko tayari kufilisika kwa ajili tu ya kuajiri ndugu yake ambaye si mwaminifu mwenye tabia ya udokozi wa mali zenyewe za hoteli na bia za wateja wanaofika kwa ajili ya huduma.

“Nilifungua hoteli moja pale Bagamoyo,lakjini nilipoongea na meneja nikakuta siyo Mtanzania ikabidi nimuulize Mkurugenzi wa hoteli kulikoni naye kaniaambia aliajiri ndugu yake lakini alichomfanyia nusura angefunga hoteli,”alisema.

Rais Kikwete alisema kuwa tatizo linakuja pale unapoajili ndugu yako ambaye ni mdokozi pia inakuwa vigumu kumfikisha katika vyombo vya sheria kutokana na ndugu na jamaa kuingilia kati na hivyo wengi kuamua kuajiri nje ili kuwa rahisi kudhibiti ukiukaji wa maadili ya kazi.

Aidha Rais Kikwete alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya mafunzo ya elimu ya ufundi(VETA) imeanza kutazama ubora wa mafunzo yanayoptolewa katika vyuo vya mahoteli ili kudhibiti wimbi la kuibuka kwa vyuo bandia mitaani.

“Vyuo vipo lakini vingi ni vya waganga njaa,hivyo tumeandaa mchakato huo pamoja na kujenga chuo kikubwa cha utalii pale Dar-Es-Salaam kwa msaada wa serikali ya Ufaransa,”alisema.

Rais Kikwete aliwataka wamiliki wa mahoteli kutopuuza mahitaji ya kuwa na wafanyakazi wenye taalumu hoyo kwani alisema hata kazi ya utandikaji wa vitanda katika mahoteli ina ujuzi wake.

Waziri wa maliasi na utalii Shamsa Mwangunga alisema kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau katika sekta hiyo wameanza zoezi la kuzipanga huduma za hoteli mbalimbali katika madaraja.

Alisema kuwa zoezi hilo lilianzia katika mikoa ya Dar-es-Salaam na Pwani na wanatarajia mapema mwakani kuanza katika mkoa wa Arusha

Akizungumzia sekta ya hoteli Shamsa alisemja kuwa mkoa wa Arusha bado unahitaji hoteli zaidi kwani mpaka sasa ina vitanda 4,189 katika hoteli na sehemu za malazi 150.

“Vitanda hivyo 4,189 ni sawa na hoteli moja tu katika jiji la Las Vegas nchini Marekani hivyo ni vyema wawekezaji wa ndani mkajiotahiti kutafiuta uwezo wa kujenmga hoteli ambazo bado zinahitaji,”alisema.

Mmiliki wa hoteli hiyo Wilfred Tarimo alisema kuwa alifanikiwa kujenga hoteli hiyo yenye vyumba 83 kwa mkopo wa shilingi bilioni nane kutoka Benki ya maendeleo kusini na mashariki mwa Afrika(PTA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kiswahili kibovu sana! waandishi kama hawa inabidi wafungiwe kwasababbu wanaharibu lugha ya taifa.

    Makosa kama haya ingekuwa ni ya English, wengi twangemlaumu na asingepata ajira kwa kutimia lugha mbovu, watanzania inabidi tuwalaani waandishi wabovu wasiojua dhamani ya lugha yetu tamu.

    Hakuna sababu ya kuajiri waaandishi wageni kama wanavyofanya mahotel, bilashaka kuna wa tanzania waandishi wasiowadokozi na wanaoelewa kiswahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...