TAARIFA ILIYOINGIA HIVI PUNDE TOKA READING NCHINI UINGEREZA,ZINARIPOTI KWAMBA SYSTEM NZIMA YA USAFIRI KATIKA JIJI HILO LEO ZILISIMAMA KUTOKANA NA SNOW NYINGI ZINAZOENDELEA KUDONDOKA KILA MAHALA KUZIBA NJIA ZOTE.
MDAU ALIE KUWEPO KATIKA ENEO HILO,ANASEMA KWAMBA HALI HIYO ILISABABISHA MSONGAMANO MKUBWA SANA WA MAGARI AMBAO ULIDUMU KWA TAKRIBANI MASAA ZAIDI 5 HUKU KILA GARI LIKIWA LIMESIMAMA BILA KUSOGEA HATA HATUA MOJA.
MDAU HUYO ANAENDELEA KUSEMA KWAMBA HALI HIYO IMEKUA NI TATIZO KUBWA SANA KATIKA JIJI HILO LA READING KWANI KUTOKANA NA BARIDI KALI NA HALI HIYO MTU UNAWEZA UKAACHA GARI LAKO NA KUONDOKA ZAKO.
TUTAENDELEA KUJUZANA HAPO BAADAE KINACHOENDELEA KATIKA JIJI HILO KWA MUJIBU WA MDAU MWENZETU HUYO AMBAYE KAKUMBANA NA ADHA HIYO LEO HII.
WENYE PICHA NA HABARI ZAIDI MSISITE KUTUMWAGIA.
JE NA WEWE ULIKUMBWA NA MKASA HUU?
JE ULIKUWA WAPI KIMBEMBE KILIPOTOKEA?


Waingereza kila mwaka snow inawashtukiza...leo kutoka Town Center Reading mpaka kitongoji cha Tilehurst safari ilichukua masaa 5 wakati kwa kawaida huwa ni dakika 10..!!
ReplyDeleteNamisi Nyumbani jamani; matatizo kama haya hakuna...lol
acha unafiki wewe anon hapo juu.sasa unaringa nini?kaa kimya huko,jamani jamani nini!skkkysyskk!
ReplyDeletewabongo bwana! Nani kakwambia mwenzako mnafiki? Ukiona una anza haya basi Nenda hospitali.
ReplyDeleteNi kaujumbe tu.
mhh! huko Reading nuksi..mbona nasikia kuna wabongo walio vichaa..wanaongea wenyewe barabarani wengine hawana mahala pa kukaa
ReplyDeleteHivyo huyo mdau mbona analiona suala la barafu kama ni habari mpya hivi? Hii si winter sasa nini cha ajabu mpaka anaamua kutoa tangazo kama vile kuna dharura. Hajawahi kuona barafu. Hivi mimi leo hapa nisambaza habari kuwa jamani jamani siku hizi Dar kuna joto nini cha ajabu? Si ndiyo miezi yenyewe? Hayo ni majira tu. Kiama bado.
ReplyDeleteMhh!! Majuu..... snow! snow!
ReplyDeleteBongo/Dar..... Jua kali! Jua kali!
Jua kali!
wewe uliyotuma hii post na wengine wote ni WAKUJA wazungu wenyewe wanaona kitu cha kawaida ndio majira yake, sio kushangaa kama kitu hakijawahi kutokea ulimwenguni. kuna nchi nyingine majira haya ndio maisha yao vya kawaida sio kulalamika hapa ukienda bongo unalalamika joto.
ReplyDeletemsameheni ndio winter yake ya kwanza, na ndio mara ya kwanza kuona snow, baada ya kutoka kwenye joto,
ReplyDeleteMaisha kitu cha ajabu, hao wa Reading na Washington wanacheza, hiyo hali ya barafu huwa inawatokea once in a blue moon. Ikitokea kazi huwa zina simama, shule zinafungwa na kadhalika, katika nchi za Nordic huku, Sweden, Norway na Finland hiyo ni hali ya kawaida, tena zaidi ya hapo. Kazi huwa hazisimami, shule hazifungwi na hakuna wa kumlalamikia.
ReplyDeleteSerekali inakazi ya kuhakikisha barabara zinafikisha watu kazini no excuse,
Serekali za mitaa zina hakikisha njia za waenda kwa miguu zina fikisha watu makazini na mashuleni.
Wenyewe wanmsemo kuwa "Baridi sio mbaya labda uwe huna mavazi sahihi"
the point is, Reading haijawahi kuwa na snow cha kiwango hiki ata siku moja! swali je ni dali dali za global warming na issue za climate change? Na hiyo ndio theme ya story.
ReplyDeletesawa jamanni punguzeni ubishoo na mabarafu sasa nini maana ya 4 sizon?? lazima kitu kianguke ebo snow snow ebu acheni hizo mbona huko minneapolis wameuchuna tu na miaka yote wanakomaga okay watoto wazuri jamani poleniiiiiiiii
ReplyDeletemdau canada
Watu wana wivu wa kijinga...eti mdau anaringa. Hahaahaa kisa ameona snow!!
ReplyDeleteMiaka 16 niliyokaa Reading haijawahi tokea Snow kama hii, mji mzima ni kama ulisamama na watu wengine kulazimika kulala kwenye supermarkets.
Hicho ndicha cha ajabu kwa hapa Reading, snow ya kawaida huwa inatokea mara moja moja "karibu" kila mwaka.
Sasa sijui hii ni global warming au global freezing; wanasayansi mnajua wenyewe!!
tatizo ni serikali ya uk haina zifaa vya barafu,na ilipita miaka mingi bila basrafu,nakumbuka mwaka jana na barafu ilirudi tena,na gordonv brown akalalamika sana kuhusu kununua vifaa vya kuondoleaa snow,nchi nyengine mbona hayo ndo maisha yao ya kawaida kabisa.
ReplyDeletetangu mjue kuweka post zenu kwa michuzi shida tupu,hio snow wala sio ya ajabu wala nini,huwa inatokea ingawa mara mojamoja,na mimi niko READING mwaka jana na juzi ilitokea hivihivi,unategemea nini winter,haya ndio maisha ya kawaida wakati wa winter.
ReplyDeletewewe anonymous 05:10 am
ReplyDeletenani kakwambia watu ni vichaa hapa Reading?ukiona wanaongea pekee yao sio kama ni vichaa ujue wanaongea na simu kwani simu zipo mfokoni either wanatumia Bluetooth au handsfree.
Eti hawana sehemu ya kukaa tutakaa wapi na mabenchi yote unaambiwa yamejaa snow??
MARRY XMASS AND HAPPY NEW YEAR.
we mdau wa reading acha ushamba. ina maana miaka yote hiyo uingereza hujawahi kutembelea miji inayopigwa snow kila winter. north west north east hata london huwa inapiga sana tu. au umeamua kuwaonyesha tu watu kuwa umeishi sana ukimbizini huko. watu kibao hapa bongo walizaliwa marekani, canada, uk nk wana passport za nchi hizo na uraia lakini wapo hapa wanapiga pesa ka' hawana akili nzuri huko wanakuja na kurudi ka' wanaenda kariakoo vile . michuzi mwenyewe kakanyaga UK mwaka 90 hata kabla hujajua kama utakuja kuijua uk.sasa wewe kukaa hapo miaka 16 tu na kupewa hicho ki-indefinite stay chako usitusumbue leo umeona snow tu basi ishakuwa tabu weka na jina lako basi tukujue.watu tunazijua snow tumezaliwa nazo huko na miaka hiyo ilikuwa snow hasa acha hiyo cha mtoto na tupo bongo tunapiga mavumba na uraia wa marekani na hatufatiliwi na mtu. huko tunakuja bila kuomba visa.
ReplyDeleteRahaa ilikuwa pale mko wawili ndani, hakuna kwenda kazini and kibaridi kunakufanya mlale pamoja siku nzima ... alafu ukute wife hana ketch-Up, raha iliyoje. Nahisi watoto wengi watazaliwa bada ya hii miezi 9 kwisha!
ReplyDeleteMdau: Tue Dec 22, 06:40:00 PM
ReplyDeleteWEWE NDIO MSHAMBA NA TENA BISHOLOLO SANA, WATU WANAZUNGUMZIA SNOW; WEWE OHH NIMEZALIWA MAREKANI, NINA PASOPOTI MBILI, NASAFIRI BILA VISA. NANI KAKUULIZA HAPA!!! UNATIA AIBU.
Haya, wabongo kama kazi kutoa upupu..mnasema wazungu hawashangai hiyo theluji, mnasema mboan ni kawaida, wengine mnasema mbona Nordic countries kawaida. Uhamba tu umewajaa..mbona TV na magazeti hayo ya wazungi ni habari hiyo tupu? Kusema kuwa ni winter mnakosa kuuelewa ujumbe kwa kuwa tu mko Reading, Marekani au kariakoo. Habari ni nini? Ndiyo, kitu kimetokea, kinasemwa. Acha ushamba nyie watu..walioleta picha za Reding na Kisarawe sawa. Angalia magazeti na TV wanaonyesha nini? je ni za Tanzanaia hizo? mbumbumbu tu nyie.
ReplyDeleteMdau Reading
Nashindwa kuelewa baada ya kipindi hiki haya magari yatatembea tena???? hivi engine haiwezi kupata madhara kwa hali hii! inatia wasiwasi. wadau wa Reading poleni sana pia sisi huku tunaungua na joto ile mbaya.
ReplyDeleteMerry Christ-mas and Happy new year!
Anne.