Watu wote mnakaribishwa kwenye kongamano kubwa la uimbaji wa nyimbo za injili litakalofanyika tarehe 1/1/2010 katika ukumbi wa kiroho wa chuo kikuu cha Maryland. Waimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa Marekani na nje, THE MISSION BAND toka Alabama ndiwo watatumbuiza wakishirikiana na waimbaji wengine mbali mbali toka majimbo mengine. Makundi yote ni ya Watanzania waishio hapa Marekani na Canada.
Anwani ya mahali pa ukumbi ni
3621 Campus Dr,
College Park MD 20740.
College Park MD 20740.
Na muda wa tukio ni kuanzia saa 7:00 mchana hadi jioni.
Kongamano hili limeandaliwa na vijana wetu wapiga muziki wa injili waishio Washington DC, Maryland na Viginia.
Si wengine bali ni :-
1. Jacob Merere wa kanisa la The Way of the Cross Gospel Church,
2. Samweli Malonja wa kanisa la The Way of the Cross Gospel Church,
3. Johnson Mzava wa kanisa la United Methodist Church.
1. Jacob Merere wa kanisa la The Way of the Cross Gospel Church,
2. Samweli Malonja wa kanisa la The Way of the Cross Gospel Church,
3. Johnson Mzava wa kanisa la United Methodist Church.
Maombi ya kuombea Taifa Tanzania yatafanyika, Tutauaga mwaka 2009 na kuukaribisha 2010 kwa shukurani. Pia wenye shida mbalimbali wataombewa. Karibuni watu wote tuimbe pamoja na kumshukuru Mungu kwa kutuvusha salama 2009.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu hizi:
Kwa mawasiliano zaidi piga simu hizi:
240 752 5719, 240 706 0351,301 237 7049


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...