WADAU WATUKUFU, HERI YA SIKU YA MABOXI (samahani kiinglishi mie iz noti richebo hivyo kama nimechemsha kutafsiri 'boxing day' naomba radhi na kama itawezekana mdau mwenye kujua tafsiri hiyo msaada tutani).
KAMA AMBAVYO MTAKUWA MMEONA HIVI KARIBUNI KUMEKUWA NA VIDEO KIBAO ZA YOUTUBE KWENYE GLOBU YA JAMII ZENYE MATUKIO MBALIMBALI. KWA TAARIFA NI KWAMBA HII NI KATIKA KUJIANDAA NA MAMBO MAPYA INSHALLAH TUTAPOINGIA MWAKA MPYA KWANI BAADA YA VIFAA KUKAMILIKA LIBENEKE LITAJIKITA PIA KATIKA HABARI KWA VIDEO.
KUTAKUWA NA INTAVYUU NA WADAU MBALIMBALI NA PIA KUONESHA NA KUSIKILIZISHA TASWIRA NA SAUTI KAMA ILIVYO KWA TASWIRA ZA MNATO, HII IKIWA NI KATIKA KUHAKIKISHA MDAU UNAONA NA KUSIKIA KINACHOJIRI.
GLOBU YA JAMII INAOMBA USHAURI,
MAONI NA PIA UKOSOAJI ENDELEVU ILI LIBENEKE LINOGE.
-michuzi
kwa hapo tu blogu ya jamii itakuwa juu kama cnn
ReplyDeleteyaani kwanza kaka michuzi nakupa hongera sana kwa kutupa habari hasahasa sisi tunaokaa ughaibuni tunafarijika sana mimi nakuunga mkono kwa hilo itakuwa bomba sana.tutakuwa tunapata vitu live.
ReplyDeleteAloo Michuzi,
ReplyDeleteAcha utani wakati wa kazi.
Ati English is not Reachable! Wee hujui unagusa hisia za watu kiukweli ukweli?
Michuzi,
ReplyDeleteNimekuwa offended na hiyo statement ya sikukuu ya maboksi , haya ni matusi kwetu sisi wabeba maboksi ughaibuni.
MICHUZI NAONA NA WEWE UNANZA KUWAKASHIFU WABEBA BOX WA MAJUU KIMAFUMBO WEKA WAZI BWANA
ReplyDeletekaka kiswahili chako kigumu hizi ngeli (taswira) mi selewi.Kwe you tu sendi baba,kumraji me chelewi kabchaaaa
ReplyDeleteBOXING DAY SIO SIKU YA "MABOX" KAKA, WACHA KUIFANYA FALA.
ReplyDeleteNI SIKU YA KUFUNGUA ZAWADI ZA KRISMAS NA HII NI KWA SABABU NYINGI ZINAKUA ZIMEFUNGWA KTK BOXES THATS WHY IMEITWA HIVO....
Udumu kwa kuendeleza libeneke. Shida ya kuweka video kwenye globu inatuzuia kuibia kampuni zetu muda kuchungulia habari. Security software zinatupiga ribiti.
ReplyDeleteMTU AMBAYE HAJUI KIINGELEZA NI JOHNI MASHAKA. yeye ndiye kiingereza not richebo kwake
ReplyDeletekaka hiyo imetulia sana. iko bomba go on man.
ReplyDeleteNi mimi mdau unayenibaniaga comments zangu.
boxing day ni siku ya kufunguwa zawadi kwa vile huku ughaibuni wana utamaduni wa kupeana zawadi wakati wa xmas huwa hawafunguwi zawadi hadi siku ya 26/12/---- na zawadi hizi hufungwa ndani ya mabox wanachofanya ni kwamba familia ikapata zawadi toka nje ya familia upokea na kuzibwaga kwenye mti wa mki-xmas au hata baba akiwapa watoto zawadi nao hubwaga kwenye mki-xmas, wanasherekea xmas kwanza then siku ya pili ambayo ni mapumziko wanakaa pamoja na kila mmoja huchukuwa zawadi alizopata na kuanza kufungua na huwa ndani ya mabox ndo maana wakaita boxing day
ReplyDeleteMmnm, Mi siamini!
ReplyDeleteBoxing Day siyo siku ya Kupigana kweli?
Boxing Day= Siku ya ndondi
ReplyDelete