Ankal,
Naomba msaada kidogo toka kwa wadau. Juma la jana nilipata wageni
walikuja kunitembelea Dar.

Ikabidi niwatafutie hoteli za middle-class, yaani hivi vihoteli
vilivyochipuka mitaani vya ghorofa mbili hadi saba na chumba cha
kitanda kimoja huwa kina-range Tshs 20,000/- hadi 35,000/- kwa siku.

Bila shaka wadau mnazijua hoteli za dizaini hiyo.

Sasa tatizo nililolikuta ni kwamba kila hoteli ninayokanyaga wanatumia
maji ya chumvi ya kutoka chini ya ardhi. Haya maji ni magumu, yana
ukakasi na ni kero tupu kuyaoga. Badala ya mwili kutakata yenyewe
yakikutana na sabuni yanatengeneza ukoko ambao unaganda kwenye ngozi,
na hivyo kuleta muwasho kwenye ngozi.

Nilizungukia hoteli saba hivi .. mbili ziko pale Ubungo National
Housing nyuma ya hostel za NBC, kisha nikaenda Sinza City Style Hotel
na vihoteli vingine kwenye ule mtaa wa Mugabe, nikaenda Grand Hotel,
Itumbi na Jangwani pale Magomeni ... kote maji ni hayo hayo ya chumvi.

Hivyo wadau naomba msaada maana siwezi kuzunguka hoteli zote hapa
jijini kufanya hii shopping.

Je ni hotel gani hapa Dar ambayo ina maji safi yasiyo ya chumvi, na
ambayo kwa siku bei ya chumba haizidi Tshs. 40,000/-?

Natanguliza shukrani.

Wenu Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Sasa ewe mdau si wageni wako walishawasili?? unatafuta hotel tena saivi ya kazi gani au ndo yale yale?? Kama unatafuta kwa nia mbaya hata ukikutana na maji ya sukari yatawasha tu....kila la kheri lakini

    ReplyDelete
  2. Anon wa kwanza hapo juu umeniacha hoi kweli. Eti maji ya sukari.

    Lakini nadhani ndugu Mdau angependa kujiandaa ili akipokea ugeni mwingine ajue hoteli gani ya kuwapeleka.

    Binafsi sijalala kwenye hizi hotel za Dar muda mrefu sasa hivyo sijui ipi ina maji safi. Nitafurahi sana kupata data kama alivyoomba mdau.

    ReplyDelete
  3. i know landmark hotel ya sinza, hawana maji ya chumvi, you myt wanna check tht out....!

    ReplyDelete
  4. Sunflowers hotel ipo Sinza hapo hapo!!

    ReplyDelete
  5. Wewe anony wa kwanza ni MPUMBAVU!

    ReplyDelete
  6. Pole sana kwa kutafuta hotel ya kulala wageni wako. Dar Es Salaam ukitaka kupata maji safi yanayotoka Ruvu Chini njoo mitaa ya Mbezi beach, Tegeta, Boko. Lakini mimi naishi Boko kwa hiyo najua Hotel ya Boko Inn View karibu na Kanisa katoliki Boko, Basi Haya Camp site nk.

    ReplyDelete
  7. Hoteli ya NAMNANI--Sinza ni safi maji moto na baridi. Colubus iko maji machafu K/nyama. Rombo Garden View corner ya Shekilango na Morogoro Rd. Mjini jaribu Durban, Harare.

    ReplyDelete
  8. Nenda Silver Sands hotel kama una usafiri. Kama huna usafiri chacharika hapo hapo katikati ya mji.

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu hoteli za aina uliyotaja huwa tunazitumia kwa ajili ya wageni wa from-dar-to-dar au watalii wenyeji.

    Ubora wa maji unaoungelea huwa hatuangalia sana. Tunachojali ni usafi na privacy, kwa kweli.

    ReplyDelete
  10. aaa nyie wamatumbi tabu kweli,hata huko ulaya hakuna maji laini , tena afadhali hayo magumu ya bongo huku maji ya mavi ndio tunaogea na kunywa pia unajua? maji ya huku majuu mengi yanakua recycle ya kuogea kuchambia yote yanasafishwa na kurudishwa tena kuyatumia,waulize hao wageni wako

    ReplyDelete
  11. Tembelea Hotel De mage ipo Nyuma ya Mk kinondoni-iko bomba,au blue rose iko Sinza.Ukishindwa kabisa nenda Moven pick ipo Ohio street,vile vile ukitaka zaidi nenda Sama guest iko mkabala na sisters bar kinondoni mkwajuni maji ni bariiidi.

    ReplyDelete
  12. Mbezi Garden patakufaa.......ila usinitaje....Mr. akijua na ndoa sina..........

    ReplyDelete
  13. Vijihoteli vingi vya Sinza biashara yao kubwa ni short time. Kwa hiyo wateja wao wala huwa hawajali sana hayo maji unayosema ya chumvi.

    ReplyDelete
  14. royal mirage na sleep inn za kariakoo. lkn hawaruhusu pombe wala mademu. kazi kwako.

    ReplyDelete
  15. Sasa tusubiri na matangazo ya biashara maana kila mmoja ataanza kusifia hoteli ya mwajiri wake humu... Mbona sie wa huku uswazi tumeshajizoelea mpaka wachina sasa hivi wanataka kutikomboa na maji yao ya bomba... waache wageni wako walalamike wenyewe sio kuanza kujihami, je wangekuta na mgao wa umeme halafu kuna maji ya bomba ungewaambia maji yate wameyaoga wao ndio tunakosa umeme..?

    ReplyDelete
  16. nenda keko twiga inn

    ReplyDelete
  17. wewe hebu kuwa siliazi, hii taarifa ni ya kweli au maji ya chumvi unamaanisha machangu, maji ya chumvi dar!

    ReplyDelete
  18. Jaribu LandMark hotel ubungo ni safi sana lakini kwa sasa bei sijui huenda iko juu.

    Kama wageni wako watakaamuda mrefu kwa nini usichukue apartment na ukalipia miezi 3?

    Mdau mzee wa New Delhi

    ReplyDelete
  19. Wadau mnaozungumzia maji machafu napenda kuwakumbusha kuwa hivi karibuni NASA wamepeleka mtambo unaogeuza mkojo kuwa maji ya kunywa kwenye international space station.Wadau mnaonaje,hii technology iingie Bongo?

    ReplyDelete
  20. valley view hotel ya jangwani.
    the son of Africa

    ReplyDelete
  21. jaribu kutia iriki hayo maji yatalanika babu wee, kama huamini nenda mombasa au unguja.

    ReplyDelete
  22. Mdau vipi wewe? Unajua siku zote Dar hakuna maji ya bomba, wewe unayatafuta, utayapata wapi DAWASA wamejifia ni maiti kabisa. Suluhisho la tatizo lako ni kuoga kwa kutumia sabuni ya unga FOMA na nyingine. Hizi sabuni zenu za miche hazifai kwa maji hayo. Wewe jaribu halafu utaona ninachokwambia

    ReplyDelete
  23. Jaribu BUMBIRE pale Sinza jirani na Landmark ni sehemu poa.

    ReplyDelete
  24. Mimi nilipokuwa Bongo nilifikia guest moja inaitwa Ascot ipo karibu na magorofa ya Bora Kijitonyama. Maji hayana chumvi, safi,security, Hd ready flat tvs na kunaungo channel zote bure. Shida yao vyumba huwa vinajaa. Bei yao karibu na bure jaribu hiyo ukipata wageni wengine.

    ReplyDelete
  25. Kwanza kabisa lugha uliyotumia ni chafu. Ati unasema vihoteli vilivyochipuka??? wtf! Watu wamejitahidi wazalendo wameweza kuonyesha kuwa nao wamo katika anga za kusaidia wananchi kwa kujenga hoteli poa na bei poa. Wewe kama ni mtzd na ni mzawa na unajua hali yenyewe ilivyo kwa nini unawapeleka wageni wako huko? Hata hoteli hizo unazosema middle class wapiii, hamna kitu. Kwa nini usiwapeleke Sheraton?

    Halafu, unasema maji ni magumu yana ukakasi hivyo huleta muwasho kwenye ngozi???? kama wewe hutumii maji hayo, umejuaje kuwa yanaleta muwasho katika ngozi? Yaani wewe unathamini wageni kuliko wewe mwenyewe! kwa nini usiwapeleke nyumbani kwako kama ni wageni wako? au unafanya mpango wa kuleta watalii halafu unawaweka katika hizo hoteli nini?

    Sielewi wageni wako hao wanatoka wapi? Ukiangalia sehemu kama za magharibi, maji watumiayo ni (recycled water)--- maji hayo yatumiayo vyooni, bafuni, ni hayo hayo yanapelekwa kwenye mtambo yanachujwa halafu yanarudishwa tena unakunywa halafu unapikia nk.

    nakuunga mkono anon hapo juu
    Mon Dec 21, 08:35:00 PM

    Halafu unasema umetembelea hoteli kama saba hivi, kwani umeingia na kuoga katika hizo hoteli zote?

    halafu unamalizia kwa kuuliza
    ----------------------------
    Je hoteli gani hapa Dar ambayo kwa siku bei ya chumba haizidi Tshs. 40,000/-?
    --------------------
    ebo! ?????

    We sema ni yako iikuwa ni kuchafua tu hizo hoteli unazosema.

    Ni mimi

    Mkulima halisi anayependa kutumia hizi hoteli za wazalendo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...