KAKA MICHUZI MAMBO VP?
MIMI NAOMBA KUULIZA SWALI KWA WANAJAMII WOTE WA TANZANIA INAKUWAJE SOMALIA, MAURITIUS NA ETHIOPIA INASHIRIKIA MISS EAST AFRICA WAKATI HIZO NCHI HAZIKO EAST AFRICA? WAKATI EAST AFRICA INAJULIKANA KWA NCHI TANO (KENYA, UGANDA, TANZANIA, RWANDA NA BURUNDI) SASA HIZO NCHI ZINGINE ZIMEINGIA LINI EAST AFRICA?
KAKA MICHUZI NAWAOMBA HAO WAANDAJI WA MISS EAST AFRICA 2009 WAWEKE WAZI SABABU YA HIZO NCHI KUINGIA KATIKA SHINDANO LA MISS EAST AFRICA WAKATI HIZO NCHI HAZIKO EAST AFRICA. HALAFU HADI DAKIKA HII HATUJAONA MWAKILISHI WA TANZANIA. INAKUWAJE?

SALAMU KWA WOTE...
MDAU VIRGIN ISLANDS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. WE NDO KILAZA KWELI, KIHIYO EAST AFRICA, SOMALIA NA ETHIOPIA NI EAST AFRICA, KWANI ZIKO MAGHARIBI YA AFRICA? USICHANGANYE MAMBO JUMUIYA YA EAST AFRICA NA EAST AFRICA NI VITU VIWILI TOFAUTI, KAMA UNAFIKI JUMUIYA YA EAST NI NCHI EAST AFRICA TU BASI RWANDA NA BURUNDI ZISINGEKUWEPO KWA VILE HAZIKO EAST. EAST AFRICA HAINA MAANA YA HIYO JUMUIYA YA KENYA, UGANDA NA TANZANIA, WALICHAGUA HILI JINA KWA VILE HIZO NCHI ZIKO EAST YA AFRICA HAIMANISHI KUWA ZENYEWE TU NDO EAST AFRICA.

    ReplyDelete
  2. wewe anonymous uliyejibu kuwa mstaarabu usiwe pimbi kiasi hicho mshikaji kauliza swali ina maana hajui kwahiyo anahitaji kujua mjibu kisaarabu usitake kuchafua hali ya hewa humu ndani au inakuhusu nini ulifikiri majungu? acha hizo babu huu ni ulimwengu wa kueleweshana lofa wee

    ReplyDelete
  3. MASHIKOLO MAGHENI.

    ReplyDelete
  4. 1. nchi za afrika mashariki zimegawanywa kisiasa na kijiografia. jumuiya ya frica mashariki ni ya kisiasa, ila mgawanyo wa kijiografia una nchi nyingi zaidi ikijumuisha ethiopia, eritrea, sudan nk. Umoja wa Mataifa umegawanya afrika kwenye kanda tano-kanda ya mashariki, kanda ya kati, kanda ya kaskazini, kusini na magharibi. Ukiangalia kanda ya mashariki ina nchi 19. tazama hapa: http://unstats.un.org/unsd/methods/m49/m49regin.htm#africa
    2. pili, michuzi na timu yako ni muhimu mkachuja baadhi ya maoni ambayo hayalengi kusaidia bali kukejeli. Haririni wa maoni hayo. Kila la kheri.

    ReplyDelete
  5. kuna vitu viwili
    1 Geographcal east africa
    jibuti,somalia somaliland,kenya,tanganyika,zanzibar,comoro,nchumbiji,some part of south africa
    2.Political east africa
    mahusiano ya badhi ya nchi kenya,uganda,tanzania,burundi,rwanda,baadae zitakuja congo,zambia,msumbiji ni just uhusiano wa kibiashara

    ReplyDelete
  6. Anon namba moja naomba Mungu akupe hekima.

    ReplyDelete
  7. MIE NAMKUBALI ANONYM WA KWANZA, JAMAA KILAZA KWELI KWELI

    ReplyDelete
  8. michuzi usiishushe sana hii blog,maswali mengine unawajibu juu kwa juu kimyakimya tu japo amesema swali kwa wanajamii wote lakin wewe ungemute.

    ReplyDelete
  9. Nathani imefika wakati watanzania tuelewe maana ya kuuliza swali na si kukurupaka kana kwamba wewe unaelewa kila kitu. Tuwe wastaarabu huo muda unaotumia kuponda muuliza swali ungeutumua kumwelimisha ili kesho nae akuelimishe anachokijua. Ahsante sana kwa wachangiaji wa mwisho kwani busara zenu zitakuwa zaidi ya hapo. thanks again

    ReplyDelete
  10. we anonymous uliyejibu kwanza una akili kabisa.mwenzako kauliza swali halafu wewe unamtukana baada ya kumwelewesha. hivi unafikiri kuwa wewe unajua kila kitu?
    Nyie mliochanbia wa pili na wa tatu Mungu awabariki. Tunahitaji kuelimishana sio kutukanana. Watanzania tujifunza kuwa wastaarabu.
    Mdau Birmingham UK

    ReplyDelete
  11. mdau Solomon Islands, nafikiri umelenga sawia. Kweli kuna kwikwi katika hili. Kwiki inaweza tokana na vyanzo viwili. 1. kiingereza - janga la taifa, na 2. general knowledge - nalo pia janga la taifa! kama hujali sana mambo ya lugha, ni vigumu kujua tofauti ya 'eastern/southern/western-africa ma east/south/west africa..hasa kwa mswahili kwani tofauti hizi si bayana sana kwenye lugha mama..Japo wa-afrika mashariki hatujaufaulu muungano wa ki-utawala (wengine wangalisema wa kisiasa), 'afrika mashariki ni dhana ya kihistoria/kijamii na kisiasa ambayo ina-nasibisha makoloni ya kiingereza/kijerumani ya mashariki ya afrika ('afrika mashariki' si lazima iwe dhana sawa na 'mashariki ya afrika' ama 'afrika ya mashariki')..hivyo kwa haraka-haraka utaona ni dhana yenye kuwakilisha zanzibar/tanganyika & ruanda-urundi (afrika mashariki ya kijerumani)/kenya/uganda. tafautisha dhana hii na ile ya South Africa (nchi moja) na Southern Africa (dhana ambayo inarandana kwa ukaribu na SADC, japo nasi tumo - maajabu!)..unaweza kuona basi kuwa swali lako lingekosa mashiko ingalikuwa watayarishaji wameyaita mashindano haya 'miss eastern africa'(mrembo wa mashariki ya afrika) ambapo kwa mtazamo wa jumla nchi zoote ulizozitaja zinaweza kuingia, na ukifikiria hata Msumbiji pia..lakini hii ni biashara labda 'miss east africa' ina mvuto zaidi ya.... - UzenG!

    ReplyDelete
  12. NDO MAANA KUNA KIPINDI CHA RADIO KINAENDESHWA NA KIJANA FULANI HAPA NCHINI YUPO HPO CHINI INAONEKANA WANAFUMZI WA KENYA NA UGANDA WAKO EXPOSED KWENYE GENERAL KNOWLEDGE KULIKO WAKI-TANZANIA, SIMPLY BECAUSE MANY OF US WE ARE SO NARROW MINDED AND WE TEND TO CRAM WHAT WE ARE BEING TAUGHT INSTEAD OF ANALYSING THEM WHY THEY ARE SO. NAHISI HUYU JAMANI ALISHA SOMA HABARI ZA EAST AFRICA COMMUNITY AKAONA MARA NYINGI ZINATAJWA KENYA, UGANDA NA TANZANIA BASI AKAJUWA EAST AFRICA NI NCHI HIZO TU

    ReplyDelete
  13. Tusimponde sana huyu jamaa kwa sababu hatujui kiwango chake cha elimu inawezekana ni mwanafunzi wa darasa la 6 au saba hii blog watu mbalimbali wa level mbalimbali na umri mbalimbali wanaitumia.

    ReplyDelete
  14. "miss eastern afrika"

    ReplyDelete
  15. mtu akiuliza swali ina maana hajui,na zaidi ya hayo credit kwa muuliza swali maana kauliza kistaarabu sana sasa wewe annonimo wa kwanza kujibu una mkashifu kwa kutojua kwake..elewa kwamba hata wewe kabla ya kujua ulikuwa hujui pia

    ReplyDelete
  16. Watanzania tuwe wastaarabu mtu akiuliza swali mjibu kistaarabu na sio kumkashifu kwa kutojua kwake..ushauri wangu kwa waliomkashifu muuliza swali ni kwamba nawaomba waombe msamaha wa wazi kwa muuliza swali na kwa wadau wote kwa ujumla..
    mungu awasamehe kwa maaana hamjui mlitendalo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...