Habari za kazi ankal Michuzi.
Salaam pia kwa wadau wote wa globu ya jamii.
Mimi ni mdau wa globu ya jamii, na leo naomba kujitokeza kuomba msaada
kwenye tutazz.
Ni kuhusu Christmas hii, mifukoni al-hamdulilah niko njema ... nina
ka-laki tano ka kutumbua. Na ni lazima ka-laki tano kote kaishe kabla
ya Jumatatu. Sasa naomba kuuliza, je hapa Dar wikiend hii ya Christmas makamuzi yatakuwa wapi na wapi?
Niambieni location, time, entrance, na kina nani watakuwepo kutumbuiza.
Especially kama kuna bash yoyote maeneo ya beach ningependa kufahamu.
Hivyo naomba wadau ambao mko informed mnimegee na mimi kwamba wapi
kutachangamka wikiendi hii. Lakini hata kama huna info za beach party
we nimegee tu info zozote ulizonazo.
Asanteni sana.
Mdau TZ Blogger
Salaam pia kwa wadau wote wa globu ya jamii.
Mimi ni mdau wa globu ya jamii, na leo naomba kujitokeza kuomba msaada
kwenye tutazz.
Ni kuhusu Christmas hii, mifukoni al-hamdulilah niko njema ... nina
ka-laki tano ka kutumbua. Na ni lazima ka-laki tano kote kaishe kabla
ya Jumatatu. Sasa naomba kuuliza, je hapa Dar wikiend hii ya Christmas makamuzi yatakuwa wapi na wapi?
Niambieni location, time, entrance, na kina nani watakuwepo kutumbuiza.
Especially kama kuna bash yoyote maeneo ya beach ningependa kufahamu.
Hivyo naomba wadau ambao mko informed mnimegee na mimi kwamba wapi
kutachangamka wikiendi hii. Lakini hata kama huna info za beach party
we nimegee tu info zozote ulizonazo.
Asanteni sana.
Mdau TZ Blogger


We kaka hiyo hela njoo unihonge mimi. Nitakupeleka viwanja vyote vikali.
ReplyDeletewewe bwege wacha sifa zako za kihaya...kama vp chukua familia yako kaipe goodtime Bagamoyo au kwa watoto yatima utapata thawabu sio kujishaua hapa
ReplyDeleteAngalia hiyo lakitano itakua kwa UKIMWI.
Mdau.
Sitakimchezo....
kuna beach party huku manyoko street masaki..yaani kutakuwa na shoo za muziki hip hop na bongo flavor kutoka kwa wasanii maarufu halafu washiriki wote wa miss east africa na mashindano ya visura wa bongo watakuwepo..kumbuka wanawake 53 wanaume 26!!! tuwasiliane
ReplyDeleteOfcourse unampango wa kumaliza laki tano...kwa nn usiangalie hata majirani zako wanaoshindwa kwenda shule au kula kwa tabu hapo jirani kwako.....japo hata kwa elfu tano.
ReplyDeleteMdau mzalendo ughaibuni
wewe huna akili jamaa zako hawana hata pesa ya kula wewe unaleta ujinga hapa sasa nenda katafute ukimwi kwa hizo pesa zako mshambaa mkubwa
ReplyDeleteHIZO HELA ZA KAFARA NINI?MBONA UNAONGEA KILIMBUKENI HIVYO,UTAKUTA MTU KAMA HUYU KAPANGA HATA KWAKE HANA NA NDUGU ZAKE HATA XMAS HAWANA NYAMA.JAMANI KUNA MALIMBUKENI AAAGGGHHHH.WEWE MSHAMBA HEBI TUPISHE SIE.
ReplyDeletewewe mshamba hizo laki tano hazitoshi hapa mjini,labda uende lugoba hukooo
ReplyDeletedah viwanja viko vingi sana vya kukupa mkuu lakini tatizo mfuko wako kaka mdogo sana sasa laki tano si ni drinks tu itakuwa ishakwisha? manake sehemu hizo nazotaka kukupeleka ni za kikweli soda 25,000 bia 100,000 kwa hiyo labda kadundulize mfuko kwanza then tutafute vidume tukupeleke sehemu za malavidavi sio vilaki tano tu unatusumbua watu na ndevu zetu tutoe comments hapa sawa?
ReplyDeleteMshikaji kauliza swali dogo tu, wapi kuna mabembezi na yeye akabembea. Wacheni roho korosho wanoko, kama hujui wapi aende we minya tu, swali halikuhusu. Jamaa wengi wanaonekana wana hasira hapa mtandaoni, au shida? Semeni na shida zenu jamani.
ReplyDeleteKwenye retirement account unangapi?
ReplyDeleteEmergency je? ukivunjika mguu kwenye kuselembuka una ngapi mzee?
kweli nimeamini kuna watu wanaona raha kubezwa!
ReplyDeleteWABOMNGO ACHENI WIVU, JAMAA ANAHELA YAKE KADUNDULIZA ATNUE NINYI MNALETA HUSDA, BWANA WALA USIPATE SHIDA, PALE MBURAHATI KWA KANISA LA MAMA THERESA KUNA BASH LA KUFA MTU, PALE KUNA MADEM KIBAO WANAITWA VIKONGWE NA MAYATIMA WANAHITAJI PESA KIDOGO TU UNAFURAHI NAO WAPELEKEE HIYO PESA WATAFURAHI SANA, POMBE AINA YA UJI WA DONA INAPATIKANA PALE NA MISOSI YA DONA KWA NDODO KIBAO, KAMA HUPAPENDI PALE NENDA MUHIMBILI PALE KAMA FIESTA ANZIA MOCHWALI UTAWAKUTA WATU KIBAO WAME COOL NA TABASAMU MWANANA, HATA MADEMU WAPPIA, JUST GO THERE MEEEEN AND ENJOY YOUR SELF
ReplyDeleteMZEE WA BUNJU
wewe umeshasema alhamdullilah alafu unasheherekea xmax unajua kwamba ukitamka neno hilo hiyo siku kuu inakuwa sio yako.
ReplyDelete