Kibao 'Mke wangu' cha Orchestra Makassay kinasindikiza mada hii
Bwana Michuzi naishukuru sana blog yako kwa kutoa changamoto kubwa kwetu sisi wadau. Hakika kila anaefungua Globu ya Jamii hakosi sehemu yake. Nakupongeza kwa hilo na sishangai wewe kuongoza kwa wingi wa wadau kuliko blog yoyote ingine ya kimatumbi. Hongera sana ankal. Ila leo naomba nisaidiwe kwa hili.
Mimi ni kijana toka Rombo mkoani Kilimanjaro na ni mwajiriwa wa UN system. Umri wangu ni miaka 31. Nimeoa dada wa Kihaya (25 years old) toka mkoani Kagera hivi karibuni, na sasa tupo katika harakati za kujipanga katika maisha yetu mapya ya ndoa takatifu.
Mke wangu hivi majuzi amepata scholarship ya kwenda Uingereza kufanya Masters kwenye Sheria na ni kozi ya miaka miwili. Tuna miezi miwili tuu toka tuoane, na nikicheki mwenzangu anafurahia sana kwenda London kufanya masomo, na sioni kama anaipa uzito ndoa tuliofunga hivi karibuni, na hasa umuhimu wa sisi kuishi pamoja kwanza.
Napenda kuwaambia wadau kuwa mimi kwa sasa sina shida ya pesa na nina uwezo wa kuendesha familia yangu bila matatizo. Mke wangu naye kwa sasa ana kazi nzuri tuu na mshahara wake sio mbaya. Maoni yangu ni kuwa tuzae mtoto mmoja au wawili kwanza, then aende akasome lakini Mhhh mwenzangu naona amepania kuondoka na wala hana mawazo yangu.
Sasa hapa nimeliwa au vipi?? Nimruhusu tuu aende, au nimkomalie na nimsihi asome hiyo masters hapa hapa Bongo? NACHANGANYIKIWA kwani nampenda sana mke wangu. Akiondoka ............ Sijui itakuwaje.
Mimi ni kijana toka Rombo mkoani Kilimanjaro na ni mwajiriwa wa UN system. Umri wangu ni miaka 31. Nimeoa dada wa Kihaya (25 years old) toka mkoani Kagera hivi karibuni, na sasa tupo katika harakati za kujipanga katika maisha yetu mapya ya ndoa takatifu.
Mke wangu hivi majuzi amepata scholarship ya kwenda Uingereza kufanya Masters kwenye Sheria na ni kozi ya miaka miwili. Tuna miezi miwili tuu toka tuoane, na nikicheki mwenzangu anafurahia sana kwenda London kufanya masomo, na sioni kama anaipa uzito ndoa tuliofunga hivi karibuni, na hasa umuhimu wa sisi kuishi pamoja kwanza.
Napenda kuwaambia wadau kuwa mimi kwa sasa sina shida ya pesa na nina uwezo wa kuendesha familia yangu bila matatizo. Mke wangu naye kwa sasa ana kazi nzuri tuu na mshahara wake sio mbaya. Maoni yangu ni kuwa tuzae mtoto mmoja au wawili kwanza, then aende akasome lakini Mhhh mwenzangu naona amepania kuondoka na wala hana mawazo yangu.
Sasa hapa nimeliwa au vipi?? Nimruhusu tuu aende, au nimkomalie na nimsihi asome hiyo masters hapa hapa Bongo? NACHANGANYIKIWA kwani nampenda sana mke wangu. Akiondoka ............ Sijui itakuwaje.
Nipeni mawazo wadau.
Naanza kujutia ndoa.
NISAIDIENI
Mdau wa Rombo


Acha ubinafsi wako wa kichanga, ungekuwa wewe ungempa tu taarifa na kujiondokea ila kwa kuwa hukupata wewe unataka kumbania mwenzio. Alokwambia watoto wanakuja utakavyo nani?? Ni maajaliwa ya Mungu. mwache shemeji akasome
ReplyDeletewewe nondo zinazotundikwa hapa kila siku huogopi??
ReplyDeleteacha mawazo ya kishamba wewe huyo mwanamke akishazaa swala la kusoma halitakuwepo tena, watoto na shule, weyeeee??
acha ubinafsi scolarship ni bahati ya kipekee ikipita imepita
ukiruhusu ujue umewaletea watu huku kuna watu wanavishawishi vya ajabu usiwe bwege shauri lako kwanza fikiria watu wangapi waliokuja kusoma halafu wakarudi kula vumbi na wangapi wamebaki huku
ReplyDeleteKama ana scholarship ya uhakika unaweza kubahatisha tu kumuachia kwenda. Bibie anaweza kuwa na furaha sana kwani hiyo labda ilikuwa ni dream yake kubwa katika maisha and I can relate with her. Maisha yako kwanza, mume, mke hivyo vipo tu kila siku.
ReplyDeleteMara nyingi watu hubadilika tabia wanapokuwa nje na hii kwa kiasi kikubwa huwa inachangiwa na hali ngumu ya maisha kwenye nchi za watu. Watu inabidi kufanya sana kazi lakini kama wako ana scholarship hiyo haitakuwa tatizo.
Mwisho inategemeana na malengo yake binafsi je anategemea kurudi? Huwezi mzuia na maisha yake so lililobakia ni kumuomba Mungu wako.
Olae, nikuta habari? Kuaminiana ndio msingi bro!
ReplyDeleteHapa inaonesha hujiamini... Issue ni nini haswa? Miezi miwili? Watoto? Au kumuamini Koku?
Inabidi umuamini mwenzio hadi alikoroge...
Mama akipata nafasi akapige shule...akirudi 27 mnaijaza dunia na mtamudu maisha kwa ubora zaidi.
Recently married...
pole sn mdogo wangu kwakuwa na mawazo mengi ya kuijali familia yako,umeonyesha ni jinsi gani unamjari mkeo na kutaka kulinda ndoa yenu.kwenda kusoma siyo chanzo cha migogoro wala kukukimbia unge pokea habari hii kwa mikono miwili na furaha kubwa kwa mkeo kubahatika kupata scolarship.miaka 2 siyo mingi yule ni mtu mzima anajua nini anachoenda kukifanya,muamini wala usiogope unacho takiwa kukifanya ni kumbembelea unapokuwa na muda hata yeye anaweza kuwa anakuja nyumbani kila kunapokuwa na mapumziko ya kitabu.mwache akasome
ReplyDeleteKama umefikia kuuliza swali binafsi kama hilo hapa, basi u r not man enough.
ReplyDeleteChagamsha baraza hiyo
ReplyDeleteacha ubinafsi bro, hiyo ni bahati yake.icitoshe jiamini kwani mpaka amekubali kuolewa nawe anakupenda, sasa mashaka ya nini? what is yours cant be taken, so relax and just pray for your mamaaa to succeed in her studies. ni hayo 2.
ReplyDeleteaah umeibiwa wewe, tafuta mwingine achana na Koku,UK kusoma hatarudi na masters mbili, yaani husband na shule,kiss her goodbye
ReplyDeletebwashee uskonde mruhusu shemeji aje achukue nondo yake..shaka na woga ondoa kabisa..cha muhimu mawasiliano. akishakata ticketi tu tuwasiliane ili nimpokee kwa mikono miwili,shaka ondoa mwenyeji kapata na atakuwa kwenye mikono salama.email yangu ni mduanzi@hotmail.com.
ReplyDeleteraia mwema mr mduanzi
Pole sana, ila kawaida tuu, cha msingi ni bado mkeo hata akirudi, jiangalie wewe mwenyewe kwenye kioo huna vimeo, sasa wenzio wakikusaidia huku ulaya unalalamika nini, cha msingi elimishaneni kuhusu kinga na acheni kudanganyana na wekeni malengo ya baadaye, wivu muhimu lakini maisha ndivyo yalivyo, wacha shem akapige shule! Ila seriously ni hard time ila jaribu kuwa positive!
ReplyDeleteKama unapesa ya kutosha basi hata kumtembelea haitokuwa tatizo mangi wewe. embu acha ushamba elimu kwanza watoto baadae. Kumbuka kwenda kusoma na wewe sio unang'ang'ana na maduka na biashara mbuzi.Acha kokushomile akasome na aje kuwa mama bora.
ReplyDeleteKOZI YA MASTERS YA MIAKA MIWILI, SIJUWI LAKINI MASTERS NYINGI ZA UK NI MWAKA MMOJA HASA ZIKE ZA KUFUNDUSHWA DARASANI, NA ZA RESEARCH NYINGI HUWA MIEZI 18, PAMOJA NA HAYO HAPO PAGUMU SANA, TENA SANA KUTOLEA MAAMUZI AU MAWAZO. LAKINI NINGEKUWA MIMI KWA SASA KULIKUWA HAKUNA MUHIMU SANA WA YEYE KUNDOKA, KANISANI WALISEMA HUYU NI MKEO AU MMEO KWA RAHA NA SHIDA, MKALA NA KIAPO JUU YA HILO, THIS IS VERY TRYING AND COMPLECATED, SIDHANI KATIKA UMRI WAKO UTAKAA TU BILA KUFYATUA BUNDUKI HADI MWENZIO WAKO ARUDI, IT IS A FAT OF LIFE PAMOJA NA UKIMWI NI NGUMU, NA HUO UTAKUWA MWANZO WA KUTETEREKA, EBU ONGENI VIZURI NA MMOJA, I MEAN ONE SHOUL GIVE IN FOR THE SAKE OF THE MARRIAGE.
ReplyDeleteNIMEONA WANAWAKE KIBAO HAPA WAMEKUJA NA NDOA ZAO WAKAZITUPA HAPA NA KUOLEWA UPYA NA HAWAJARUDI TENA NA SASA NIRAIA WA HAPA, NA HUYO BINTI MBICHIIIIIII INATAKA MOYO KUVISHINDA VISHAWISHI VYA HUKU, JAMAA ATAMWINGILIA NA GEAR YA KUMPATIA MAKARATASI, ITAKUWA VIGUMU KUYAKATAAAAAA.
ReplyDeleteNdugu yangu, Maisha ya wawili ni matamu sana.Mkeo kupata scholarship ni jambo zuri tena la bahati kubwa sana maana ni watanzania wengi wanatafuta na hawapati. Ninachokushauri muache akasome kama ni mke wako ataendelea kuwa mke wako maisha yako yote. Ila kama aliolewa na ww kwa sababu unafanya kazi United Nations basi jiandae kwa litakalotekea hapo baadae. Cha msingi hapo ni shule na akiludi itakuwa ni msaada siyo kwako tuu bali kwa watoto mtakaowazaa hapo baadae. Hata hivyo miaka miwili si mingi kama vile wewe unavyodhani. Nakutakia maandalizi mema ya mkeo kwenda shule.... MTIZAMO WAKO IWE NI MAENDELEO YA FAMILIA YENU NA SI KUFIKILIA UPANDE MMOJA TUU.
ReplyDeletedamn mwanamke mwenyewe ni koku babu umeriwa akiondoka tafuta jikolingine kabla hujajipiga kitanzi
ReplyDeleteUnataka kuleta mambo ya mfumo dume hapa, eti kumzuia kusoma nani kasema una mamlaka hayo? Ujue kuwa hata kama mmeoana ni lazima mpeana nafasi pia, ama sivyo hata wewe utasuffocate ndani ya hiyo ndoa ukianza kubanwa kama nywele kwenyey kibanio. Kwani alokwambia kipato kikubwa ndio mwisho wa elimu ni nani? Au una inferiority complex unaona kuwa akienda kusoma basi atakuzidi elimu na huwezi kumbana utakavyo au ataweza ku argue na wewe kisawasawa? Maana mie sioni tatizo lako kwa kweli, kama unasema kuwa huna tatizo la pesa tabu iko wapi na dunia siku hizi ni kama kijiji, waweza amua kila baada ya miezi mitatu uko naye huko masomoni umeenda kumpa sapoti na kuondoa msongo wa mawazo.
ReplyDeleteAu ingekuwa wewe ndo umepata hiyo scholarship ungemuuliza mara mbili mbili kuwa uwenda au ubaki TZ kwa sababu mnataka kutafuta mtoto au ungendelea tu na mipango yako ya masomo? Ukitujibu haya tunaweza kujua kuwa uamuzi wako ama unatokana na concern yako ya kuanza familia au mfumo dume ambao unaona mwanamke hafai kujiendeleza kazi yake ni kuzaa na kulea watoto. Kwanza ndio kwanza ana miaka 25, anaweza kuzaa akiwa 27 wakati anamaliza shule ni suala la kupanga tu kwani hakuna mwanamke aliyeshindwa shule kwa sababu ya mimba.
Hata ukimzuia vipi, mafisadi wakimtaka huna ubavu wa kumlinda hata kwa masaa mawili; watammnanihii na wewe mwenyewe ukimsindikiza bila kujua.
ReplyDeletePia vishawishi haviko UK pekee, tena huko nyumbani ndio viko vingi sana hasa kutoka kwa mafisadi papa na nyangumi,
Mwachie Koku aende masomoni, nina imani hata akivunja amri ya sita atafanya kwa siri na wewe hutajua.
Ndugu yangu ndoa ni kuaminiana, na pia usisahau Elimu ni ufunguo wa maisha na kumuelimisha mwanamke utakuwa umeielimisha jamii! Wangapi wanaitaka hiyo chance ya kupata scholarship na hawaipati? Huyo mwanamke kama ana nia ya kukuacha sio lazima awe mbali, akiwa na nia hiyo atakufanyia hata akiwa hapa. Kwa hiyo mi nakushauri mruhusu kwa moyo mmoja aende masomoni huku mkiweka mawasiliano mbele. Sababu kuu ya kukushauri hivyo kuwa kwanza ukimzuia akazaa kwanza ni kwamba habari ya kusoma imekufa, na wewe usitake habari ya kusoma ife sababu elimu hiyo hiyo ndio itawasaidia na kuwapa changamoto watoto wako pia. Pili kama ataamua kukushiti akiwa huko ndiyo utajua kuwa alikuwa hakufai hata akiwa hapa, sababu angekuwa hapa halafu akawa anakuzunguka kwa nyuma wewe ufahamu kinachoendelea anaweza kukuletea hata maradhi.
ReplyDeletehapana ubishi unampenda sana KOKU! ni kweli ukimruhusu aende masomoni nafasi ya kubanjuliwa ni kubwa mno. kwa vile una pesa nyingi ningekushauri usimyime nafasi yake ya kusoma. ili kuhakikisha KOKU anaendelea kuwa wako tu nawe uambatane naye - tena itakuwa ni vizuri unamsaidia kupika na kufua, kusafisha nyumba wakati yuko darasani. KOKU atakuwa wako milele!
ReplyDeleteOrchestra Makassy - Mke Wangu
ReplyDeleteMwishimiwa sikiliza huu wimbo utajua ufanye nini sawa mwanakwetu
Nenda (Orchestra makassy youtube)
www.orchestramakassyyoutube.com
Walasaaam.
Kikombe cha chai wanatumia watu wengi hotelini . Baada ya kutumiwa, kinaoshwa, mteja mwingine anakuja kukitumia bila kusikia kinyaa.
ReplyDeleteSasa wewe Mangi miaka miwili, hata kama wa-UK watatumia, akija sina wewe unaendeleza.
HABARI NJEMA SANA HII..NINA MIAKA KAMA 3 BILA KUWA NA DEMU WAKIAFRIKA ....MKUU NAOMBA UMWACHE AJE BINTI YAWEZA KUA NDIYO BAHATI YANGU....NIMEMISS SANA VYA NYUMBANI...PLS PLS PLS MWACHE AJE SHULE KAKA.
ReplyDeletemuache akasome kaa ujue hata angekuwa hapo dar bado koku ni lazima awe na koku mwenzie kwani hiyo ni jadi ya kwetu BK.hivyo itanibidi niwe mchoo juu kwani akija tu huyo nitakusaudia kumtunza.mtu mwenyewe wee mangi mambo mengine huyajui ya kwetu BK.mangi toka lini akajua malavidavi?
ReplyDeleteMhh miaka 25 sio mchezo...Mkubwa mimi nitakutunzia nipo hapa hapa LONDON kama vipi wewe nipe jina lake na shule ambayo atakayosoma nitakutunzia...ila fahamu kwamba kama anakuja U.K atakuta vishawishi tu na lazima atagongwa miaka 2 mingi sana na hasa kwa miaka kama ya huyo mke wako!!
ReplyDeleteNamkaribisha
SALI SANA ASIKUTANE NA RWEYEMAMU HUKO HEE, UTAKUWA UMELIWA. MAANA ATAJISIKIA KAMA YUKO KURE NYUMBANI, NA KAMA HUNA MASTERS AKIMALIZA YAKE ANATAFUTA MWENYE NAYO NA UKIZINGATIA WARE WATU WA BK WANAZO TATU TATU, NA PHD JUU
ReplyDeleteMuache akasome pia akiwa masomoni anao uwezo wa kukuombea viza kama mume wake uwende kama ni miaka miwili sio mingi hawamnyimi viza ya kukutana na husband sawa usijali hayo ni maisha yenu nyote muhimu uwaminifu.
ReplyDeleteaaaaaaah,
ReplyDeleteankal huu mwimbo haupendezi tena bila kusema "ntakujengea nyumba kama Kilimanjaro, utakula wali chapati pilau vinachacha," hebu mzee Makassy aurekodi tena properly,
ndo umaarufu wake huo wimbo,ah!
so dissapointed!!!
Aise Bwashe'
ReplyDeleteakija tu ulaya,jiandae kuacha kazi uje utunze ndoa na kufagia barabara za uk.
ukimuacha aje ulaya,jua atarudi na expirience ya WaGhana WaNigeria,na Mandingos,
Ulipokuwa unafunga ndoa hakukwambia kuwa anasubiria scholarship,kwani angekuwa mchumba asingeondoka,angesubiria ndoa,sasa ndoa anayo,anajua keshaolewa and akirudi ndoa ipo palepale,
wewe hesabu maumivu ya roho,else chukua likizo ndefu kazini kaishi naye ulaya,
nimeishi uk for 10yrs naongea from experience,ukiitaji msaada zaidi sema nikupe know how ya maisha uk kwa mademu
POLE SANA
Mzalendo
Dogo acha Mkeo akasome maana nondo ni muhimu mno miaka miwili kitu gani...!! Unaogopa kuchapiwa asa si bora huko mbali kuliko hapahapa town...! ELIMU NI BORA kisha NDOA INAFUATA.Ukimkomalia ndio utajuta kwanini ulioa...!!
ReplyDelete"Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa." (Kumbukumbu la Torati 24:5-5). Tafakari chukua hatua.
ReplyDeleteukimruhusu aende ndoa itakuwa imefikia mwisho. mwambie asome hapa bongo aking'ang'ania kwenda ujue hana mapenzi ya dhati na wewe na akiondoka ni bora uoe mke mwingine kwani amini hatarudi. kwani huko aendako kuna mafisi yenye tamaa na wake za watu.
ReplyDeleteWE KUBWA JINGA MUACHIE SHEMEJI AKASOME.
ReplyDeleteKAMA ANAKUPENDA NA MNAPENDANA NDOA ITAENDELEA. ANAWEZA KURUDI NYUMBANI AKIMALIZA MASOMO AU KUBAKI LONDON NA KUKUFUATA WEWE KUUNGANA NAYE HUKO.
POLE NDUGU YANGU.
Oh my GOD! hivi wewe unampenda kweli huyo dada? it seems wewe ungeenda ndo ungeharibu,JIAMINI KAKA.
ReplyDeleteJust let her go to do the masters. Its a once in a lifetime chance and remember the saying - if educate a woman, you educate a whole generation. You should have known that where your wife comes from, they have high education aspirations - all the Drs and Profs etc. If you have the money as you claim, you can visit her frequently within those two years so that both of you don't get tempted to commit adultery. She has a good job and a husband to come back to, why would she want to stay in UK afterwards? HAVE FAITH
ReplyDeleteKaka pole sana. Mimi nakuelewa sana wasiwasi wako, na ni vizuri kuwa na wasiwasi. Mimi kwa sasa niko UK na i can tell you that you have a big dillema. Kwa sababu hicho anachotaka kufanya shemeji ni muhimu sana kwa maisha yake lakini pia ukae ukijua possibility ya yeye kufanya mambo mengine katika hicho kipindi cha miaka miwili huku UK ni kubwa sana. I mean anaweza asiachane na wewe lakini kuliwa ataliwa tu kaka. Maisha huku bila mwenzi kuwa karibu hasahasa kwa akina dada tena kama ni mzuri, ni magumu sana. Anaweza akafanya hivyo bila hata yeye kupenda sometimes lakini hali halisi itamfanya. Hiyo inabidi ukubaliane nayo tu. Ukubwa dawa kaka, inabidi ndani ya moyo ujue hilo lakini umeze kimyakimya. Pole sana ndo ukubwa huo.
ReplyDeleteShimboni Massawe, hivi unatafuta matusi kweli au. kama ni mkeo si ulimuoa ukiwa na mali basi kama mali zingekuwa ndo zilizomleta Kokubanza asingethubutu kutaka shule, huyu alikupenda kwa dhati. Kaka yako nasema muache shemeji akasome kwani kama ni kushughulikiwa hata hapa Tz watu watamnanii. Halafuuu, si mlisema mtapendana kwa shinda na raha, sasa hii ndo shida yako vumilia na endelea kumpenda acha ufala. unajifanya bonge la beki basi usiende kazini ili ukabe alaaaaaah!!!???. Nakushauri kama presha imezidi acha kazi ukaishi nae UK si ulisema pesa unazo?
ReplyDeleteUMELIWA BABAKE AKIENDA LAZIMA ATAOLEWA NA DUME JINGINE WEWE JITAYARISHE KUOA MWINGINE BABAKE.
ReplyDeleteBrother Michuzi weka na ule unaosema MUME WANGU umepata bwana tajiri shahada ya masomo watupa baada ya siku mbili wapika wali,chapati,vyote vya chacha mume haonekani.
ReplyDeleteWasalaaaam Hillary
Mangi oko. sikiliza bwana msee huu ni ushauri toka kwa ndugu- nduguyo, nenda nae huko ulaya kwa huo mwaka mmoja na akimaliza rudi nae kwa maana aisee jamaa huko ni wabaya sana mangi wanachukua na kula kondoo na mkia wake bila masiara eti.Pia shule na mimba zinaendana pamoja watu wengi wanasoma shule na mimba, kama huwezi kwenda pachika na aende salama, itakuwa nafuu kwako.Wacha wakuite majina yoyte wanayotaka wewe angalia upande wako kuwa greedy with ur soulmate no matter what.Mimba,Mimba,Mimba,Mimba hoye mangiiiiiii.
ReplyDelete