Shule ya Msingi Rwamlimi iliyopo Musoma Mjini inasikitika kutangaza kifo cha Mwalimu mwenzao Mwl Dalphone Lameck kilichotokea katika hospitali ya Bugando leo tarehe 28/12/09.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Rwamlimi –Musoma. Marehemu ameacha Mke na watoto.
Marehemu Mwl Lameck katika uhai wake alishika nyadhifa tofauti hasa ualimu mkuu katika shule zifuatazo za msingi Nyakato, Nyasho, Rwamlimi zilizopo Musoma Mjini.
Habari ziwafikie ndugu wa marehemu popote pale walipo,Walimu wote waliowahi kufundisha nae ,wanafunzi wote waliofundishwa nae wakatika wa uhai wake,Majirani na marafiki wote pale Rwamlimi Musoma bila kuwa sahau washiri wote wa kanisa la wasabato Rwamlimi na Nyakato
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
-Amen
RIP Mwl Lameck Etunga, tunakukumbuka sana, hasa kwa utunzi wako mahiri wa nyimbo pamoja na ngojera!
ReplyDeleteUmetutoka kimwili lkn kiroho huko pamoja nasi!
frm Germany
Tutamkumbuka sana hasa katika fani yake ya kiswahili.Pia wanafunzi waliofundishwa nae,wekeni majina.
ReplyDeleteBwana alitoa na Bwana ametwaa,ulale kwa amani Mwl.Lameck
ReplyDeleteNakukumbuka sana,hasa ulipo kuwa mwl.mkuu shule ya msingi nyakato mwaka 1991,nami nikiwa mmoja wa wanafunzi wako wa darasa la saba,ukiwa na mwl.Karugila wa somo la hisabati na marehemu somo la english.
POLEENI WOTE MLIOGUSWA NA MSIBA HUU,NA MUNGU ATAWATIA NGUVU NA UVUMILIVU.
MAGESA,CJ TANGA