Pastor Malisa


Kwa niaba ya kanisa la Umoja la hapa Dallas,ninayoheshima kuwajulisha watanzania wote kwamba, mtumishi wa Mungu PASTOR MALISA kutoka Tanzania atakuwa mgeni wetu siku ya Jumapili tarehe 6.12.09 (12.6.09) kuanzia saa kumi na moja na nusu jioni.
Mtumishi huyu amekuwa akitumiwa na Mungu sehemu mbali mbali duniani kwa njia ya kipekee kabisa iliyoambatana na ishara na miujiza mingi.Kwa muda mrefu sasa Mungu amekuwa akimtumia huyu mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kuleta uamsho katikati ya watanzania walioko huku Marekani.
Kwa sasa Pastor Malisa anasimamia kanisa huko Minnessota huku akizunguka sehemu mbali mbali ambazo Bwana amemuagiza kufungua watu ambao wamefungwa katika vifungo mbali mbali vya shetani.

Kutokana na umuhimu wa siku hii, ninaomba kila moja atakaesoma tangazo hili amjulishe mwenzake.Mbali ya huduma ya neno la Mungu kutakuwa na maombezi mbali mbali pamoja na ushauri wa kiroho kwa atakaehitaji.
Wako katika kazi ya Bwana
Pastor Abisalom Nasuwa
Mahali;Umoja International Outreach Church
12727 Hillcrest Road,
Dallas,
Texas 75230
Simu: 214 554 7381,682 552 6204
Email:Umojachurch@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ningeomba Mhe Pastor Malisa ashauriwe kutumia hiyo "miujiza" yake kutokomeza mafisadi nchini tanzania yanayozidisha dhiki kwa waja wa Bwana.

    ReplyDelete
  2. Anony Sat Dec 05, 05:19:00 PM acha jazba kaka-Mafisadi wataisha tu.

    Umeniua mbavu man.

    Hata hivyo u got a big point
    Miujiza tunahitaji sana bongo ikiwamo kwa poor people na wasiojiweza, wagionjwa wanaokosa tiba hospitalini nk

    Sometimes inanifanya niamini maneno ya Yesu juu ya manabii wa uwongo " wengi watakuja kwa jina langu".

    Kwanini ghafla tu bongo isiwe New york? Ama Dodoma ikawa DC, na Arusha kuwa Vegas? Moshi iwe London na Morogoro Iwe Frank-foot mwanangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...